Tuburudike na kujifunza kwa vituko na tabia za wanyama, ndege na wadudu

Tuburudike na kujifunza kwa vituko na tabia za wanyama, ndege na wadudu

Kuna thread wamejadiliwa njiwa, najihisi kuvutiwa nao....natamani kuwafuga, ila sasa kwamba hawapendi kelele.....mi mbona nna kelele na hawa watoto humu ndani watakaa kweli njiwa au ndio day 1 tu wataumia masikio wakimbie.
Kuna nyimbo zinaimbwa "Njiwa bora kumuuwa kuliko kumsaliti..."Eti kila njiwa anakaa na dume mmoja tu mpaka afe.Hivi ni kweli?.
Kuna kijana wangu mmoja amewafuga sana.Alichoona yeye ni kuwa njiwa akitotoa anatotoa mmoja dumu mmoja jike sijui ndio hawa huoana au vipi.
 
KUKU ANAKULA VITU VYA SUMU NA SISI TUNAMLA
Kuna nyimbo inasema ukichunguza anachokula kuku basi hutomla.Ni kweli kuku ni moja ya nyama tamu sana na yenye kujenga mwili.Lakini kuku anakula wadudu wenye sumu kali ambao kama tukiwala sisi binadamu hata kwa bahati mbaya tunaweza kufa mara moja,Mfano kuku anakula vinyoka vidogo na pia anakula mijusi,Hii mijusi ndio moja ya vyakula vyake anavyovipenda sana,Akimuona atafukuzana naye kwa juhudi sana,Ajabu mara akishamla na ukaamua kumchinja ili na wewe umfanye kitoweleo basi kule tumboni humuoni na nyama yake inabaki na utamu ule ule.
Mwangalie huyu akimeza nyoka mzima mzima.Ndio maana bibi yangu hali kuku mpaka achinjwe asubuhi kabla hajatoka bandani.

Siku izi watu wanakula ma broiler tuh hata hayaezi kula mijusi hayo makuku
 
Kuna thread wamejadiliwa njiwa, najihisi kuvutiwa nao....natamani kuwafuga, ila sasa kwamba hawapendi kelele.....mi mbona nna kelele na hawa watoto humu ndani watakaa kweli njiwa au ndio day 1 tu wataumia masikio wakimbie.

[emoji81][emoji81]itakua we ni wale wamama kila mda unakemea vitoto kwa utundu wao[emoji75] njiwa hawaezi kuvumilia makelelee yako watasepa tuh
 
Mbuzi anatabia fulani hivi ya uchokozi, yaani sehemu ambayo umemkataza ndiyo hiyo sehemu atataka kwenda ili mradi tu aone utamfanya nini... Lakini pia Mbuzi wao, huwaonyesha hata wanyama wenzie dharau, anajiona yeye ana uspecial hivi.

All in all napenda sana life style yao Mbuzi, nawapenda pia wanafurahisha sanaa. (Video sina)
Tena ukutane na vimbuzi viko kama Vilast born vikorofii na hamna kitu unaweza kuvifanya🤣🤣🤣
 
KUOGA MUHIMU HATA KWA NDEGE.LEO NIMEKUTANA NA KUNDI LA KUNGURU WANAOGA
Leo muda mfupi kabla ya magharibi kuingia kulinyesha mvua kidogo na maji yakafanya kidimbwi.Muda si muda kikaja kikundi cha kunguru kuaoga .Nusu wanakunjua mabawa na kupiga mbizi na wengine wanalinda halafu inakuja zamu yao.Walioga na kujisuuza takriban robo saa hivi.Halafu haooo....Nasikitika sikuweza kuwapiga picha.
Karibu iwapo una taarifa zaidi za kunguru.

View: https://www.youtube.com/shorts/ntiULVy6-38
 
Mbuzi anatabia fulani hivi ya uchokozi, yaani sehemu ambayo umemkataza ndiyo hiyo sehemu atataka kwenda ili mradi tu aone utamfanya nini... Lakini pia Mbuzi wao, huwaonyesha hata wanyama wenzie dharau, anajiona yeye ana uspecial hivi.

All in all napenda sana life style yao Mbuzi, nawapenda pia wanafurahisha sanaa. (Video sina)
Mbuzi anasema ilikuwa Jana!hakumbuki ya Leo!
 
KUNGURU WANAIJUA MANATI.NAJIULIZA WALIIONA WAPI
Hapa nyumbani nimeishi na kunguru wawili wasumbufu kwa zaidi ya miezi sita.Wanakwapua na kuchafua mazingira kila siku.Hata nikiokota jiwe nikawatishia hawatishiki na wanarudi baada ya muda mfupi.
Sasa nikaamua nisiwatishie tena bali niwatafutie silaha nitakayoweza kuwafikia kwa ghafla ambayo ni manati.Siku nilipoingia nayo ndani nikawaonesha na kuwaambia mumeiona hii.Halafu nikainyuuwa kama nataka kurusha kijiwe kwayo. Ndio ikawa siku ya mwisho kuwaona.
 
Mkuuu hii ni kweli mm home nafuga kuku,kunguru walikuwa wanaiba sana mayai Kuna mwamba akaniambia tafuta manati weka juu ya mlango,
Uwezi amini huwa wanapita Kwa mbali lkn hawasogei eneo langu.
 
Mkuuu hii ni kweli mm home nafuga kuku,kunguru walikuwa wanaiba sana mayai Kuna mwamba akaniambia tafuta manati weka juu ya mlango,
Uwezi amini huwa wanapita Kwa mbali lkn hawasogei eneo langu.
Kilichonifanya nikanunue manati ni ile jeuri yao.Kila nikiinua mkono kutishia kuwapiga wanasogea tu.Hata ukipiga mayowe wanakuzomea.Nikaona nitafuta kitu kitakachowaendea kwa kasi.Muuzaji wa manati ndio akajiongeza kunishawishi kuwa hii wakiiona tu wanakimbia.Nikahakikisha nilipofika nayo nyumbani.Mpaka leo kimya kabisa.
 
PUNDA HUONA WACHAWI
Ukitaka kufika miji ya mbali kwa haraka unapanda ndege za abiria.Ukitaka kuona wanyama maporini unapanda magari maalumu ya kukupeleka huko.
Ukipenda kutembelea kijiji chenye wachawi wengi basi panda punda kwani ndiye anayefaa zaidi kwa safari hizo.Punda ni zana maalum tulizoumbiwa binadamu kuwakwepa wachawi maeneo tunayotembelea.
Muda wote punda huwa anawaona wachawi na muda mzuri kumtumia ni usiku.Kawaida mtu ndiye anayemuongoza punda kufuata njia anazotaka.Ikifika usiku basi lazima ukubali kuongozwa na punda kufika unakotaka.
Mara punda anapowaona wachawi masafa ya mbali mbele yake au sijui anasikia harufu zao mwanzo basi punda husimama ghafla na hubadili njia.Ukiona hivyo hupaswi kumshurutisha njia unayotaka wewe.Ukifanya ukaidi anaweza akakubwaga chini au akapinda kukurudisha nyumbani.
1696138758270.png
 
Back
Top Bottom