Tuchangiane uzoefu katika malezi: Malezi yako yalikuwaje, unahisi yamekuathiri, ungependa kulea watoto wako kama ulivyolelewa?

Malezi ni njia ya ukuzaji, ni kama kumea. Matokeo ya kilichomea kinatokana na jinsi kilivyomeewa. Hata nyasi zinazotunzwa na binadamu na zile zinazojiotea kumea kwake zinategemea na hali ya uhusika. Zile ambazo zitakazomea vizuri zinategemea mazingira yake, eidha, binadamu amezitunza kwa uzuri ama mazingira yamekuwa rafiki mzuri kwa zile nyasi na kinyume chake ndivyo vivyo hivyo.

Halikadhalika na malezi kwa watoto. Mzazi ana haki zake kwa mtoto na mtoto ana haki zake kwa mzazi. Muhimu ni kutambua nyakati kama ya kuwa mkali uwe mkali, ya kuwa msikilzaji uwe msikilizaji na kama ni suala la kuelekeza uwe muelekezaji na uwe mvumulivu. Pasipo kusahau jamii nayo ina nafasi yake ya malezi, kuna tofauti kati ya mazingira ya Kimara na Kinondoni.
 


Umenena vizuri mkuu...🙏🙏
 
Mkuu hearly usipite tu

tupatie uzoefuu wako pia,labda kutokana na malezi ulioyapitia ua hata Rafiki zako wa karibu au hata unavyolea watoto wako(kama unao) unaonaje malezi yako yanwafanya wanakuwa watu wa namna gani?
Miss Blu G

Naomba upokee salam zako toka watu wa ukanda ule. Wamekumiss sana.

Tukirudi kwenye mada.

kwa mtazamo wangu suala la malezi ni complicated sana. Jinsi wazazi/walezi mnavyo behave ndani ya familia , mna mchango mkubwa sana katika kum shape huyo kiumbe mdogo. Pia jamii inayomzunguka mtoto ina ushawishi mkubwa katika kumtengeneza huyo mtoto.

Ieleweke kwamba watoto hawarithi maneno wanayoambiwa bali tabia wanazoziona. Kwa hiyo ukuaji mzuri au mbaya wa mtoto utategemea ni tabia zipi au vitu gani ambavyo amekuwa akiviona katika utoto wake.
 
Katika ubora wako Best. Bila ya shaka huu ni uzi bora wa 2019 sidhani kama kutatokea uzi mwingine bora kama huu mwaka huu.

Ila uache kupotea sana humu. Watu wenye busara na hekima kama wewe wanahitajika sana humu, hata kama ni majukumu lakini bado unaweza kuweka masaa machache ya kuja kuweka hekima na busara zako humu.

Jioni njema BG 🌹🌹🌹

 
Unajua mtoto anayoyaona ndiyo anayoishi nayo. Inawezekana mtoto akawa si wako lakini akarithi tabia yako. Siamini kama kuna tabia ya urithi wa ki DNA, ninachoamini ni kwamba mwenendo wa matukia ambayo anayelelewa ndiyo yaliyomzunguka basi naye huyaiga, na msukumo zaidi utatokana na yule mchunga jinsi atakavyomchunga.

Ndivyo ninavyoielewa dhana ya kurithi( kwa muktadha wa hii mada lakini)
 
I love my mom,never raise her hand kutupiga...sio kama wamama wengi wanoko...lol!..nitatumia the same approach kulea wanangu...no kiboko na Maisha yanasonga… I LOVE YOU BECKY...
 
Reactions: BAK
Mimi nimelelewa katika misingi mizuri kimaadili,. Mama yangu alikuwa mkali sana nikikosea ama nikiwa mvivu kufanya kazi.. Though kuna muda alikuwa akinidekeza maana mtoto wa mwisho ni wa mwisho tu.
Japo sijawahi aswa na wazazi wangu kuhusu mambo ya wanaume..
Maybe sababu Maisha yangu muda mwingi nilipenda kukaa mwenyewe.
Nimekuja kuambiwa na dada yangu kwa njia ya story za kawaida napo ni mara moja tu kipindi naenda kuanza kidato cha kwanza

Maisha yangu muda mwingi nilipenda kukaa nyumbani, si mtu wa kujichanganya na watu.. Na si kwamba nilikuwa nazuiwa.. Ni mm tu nilijizoeza na nikazoewa hivyo.
Hii imeniathiri japo si sana maana nashindwa kabisa kujichanganya na watu.

Nimejikuta muda mwingi nautumia kuwa mwenyewe na kufanya ibada na shughuli zangu nyingine

Wanangu nitawalea katika njia ipasayo,
Sehemu ambayo nahisi wazazi wangu walipwaya, nitajitahidi niongezee kwa wanangu.
Sitawaachia sana wala kuwabana sana.
Ntakuwa mpole pia mkali sehemu inapohitajika kufanya hivyo.
 
Tabia ya kurithi ipo ila ngoja nikupe mfano watoto wawili wa baba mlev,mmoja anaweza kuwa Mrefu km baba yake Mmoja sio mrefu.Kwanini hilo linatokea??kama tunarithi kupitia vinasaba??

Wengi wao ni wanaiga matendo ya wazazi wa baada ya kuzaliwa.Ni ukweli kwamba mzazi Ana uwezo wa kumuambukiza feelings mtoto,ukiwa na furaha mtoto akiwa karibu yako atakuwa na furaha bila hata kusema neno,hivo hivo ukiwa na huzuni,malaya,mkorofi, kiburi.Mtoto haitaji kujifunza kiburi Ni akiwa karibu na wewe tu karibu anabeba hisia zako za kiburi na majivuno mda wote..

Hapo tunarud kwenye ile ile point ya mwanzo mtoto Anaangalia matendo yako na hisia zako basiii maneno hana habari nayo..Una mood gani ukiwa mbele yake?ukiwa na hasira unafanyaje?ukiwa na furaha unafanyaje?mwanamke akipita mbele yako unafanyaje?
 
MALEZI NI MAPANA SANA KWA KWELI KUTOKANA NA JAMII NYINGI ZILIZOPO ULIMWENGUNI KUWA TOFAUTI PAMOJA NA HAPA NCHINI KWETU PIA. MALEZI HUAMBATANA NA HISTORIA NA NDIO MSINGI MKUU. HISTORIA NDIO HUFUNUA ANZIKO LA FAMILIA, KOO, KABILA, TAMADUNI, DINI NA SHERIA ZA JAMII NZIMA HUSIKA YA MAHALA FULANI (MF: TAIFA). KWAHIYO LAZIMA TUKUBALIANE KUWA JINSI TUNAVYORITHI NDIO TUNACHOFUATA MARA NYINGI ZAIDI KATIKA SHUGHULI ZETU ZA KIBINADAMU KILA SIKU NA PIA MABADILIKO HUPATIKANA KUTOKANA NA HISTORIA YENYEWE.

KWAHIYO MALEZI NI TUNU YA URITHI AMBAYO MTU HUSIKA ANAJIFUNZA KATIKA FAMILIA ALIYOTOKA, KABILA LAKE, DINI YAKE NA JAMII YAKE KIUJUMLA. MFANO MASWALA YA HASIRA, MAJIGAMBO, UCHAPAJI KAZI, STAREHE, KUJIUA, UKATILI, UNYANYAPAJI NA MENGINE MENGI.

KWA MALEZI HASA YA FAMILIA KUNA CHANGAMOTO NYINGI SANA HASA ULIMWENGU WA LEO, ILA NAPO HISTORIA YA NYUMA KULIKUWA NA CHANGAMOTO ZAKE PIA. KINACHO TOFAUTISHA UWINGI WA CHANGAMOTO NI IDADI YA WATU WA SASA NA ZAMANI, WATU WA SASA NI WENGI ZAIDI WANAKUMBWA NA KADHIA YA MALEZI KULIKO IDADI NDOGO YA WATU WA ZAMANI. UNAWEZA KUFUATILIA TAKWIMU ZA SENSA KUJUA ZAIDI.

MALEZI YA FAMILA HUTAFSIRIWA KWA FAMILIA MOJA MOJA, KWAHIYO HIZI FAMILIA HAZIWEZI KUWA SARE KATIKA HUDUMA, TABIA, UONGOZI WA FAMILIA N.K. KWAHIYO KILA BINADAMU ANAYEZALIWA KWENYE FAMILIA HUSIKA ANAWAJIBU WA KUJIONEA YALIYO SAHIHI NA YASIYO SAHIHI KWENYE MALEZI YAKE ILI KULETA MTAZAMO TOFAUTI PINDI ANAPOANZISHA FAMILIA YAKE BAADAE. JAPO BADO ZIPO CHANGAMOTO ZA UKABILA, UDINI NA MIENENDO YA JAMII INAVYOTAKA PAMOJA NA SHERIA ZILIZOPO KITAIFA KWAHIYO HUTIA UGUMU KWENYE KUBADILISHA MITAZAMO ILIYOPO. MFANO MASWALA YA NDOA, MALEZI YA FAMILIA, ELIMU YA UJANA, HAKI ZA KIJINSIA N.K

MALEZI KATIKA FAMILIA NI SWALA LA WAZAZI/ WALEZI NA WATOTO KWA PAMOJA. CHANGAMOTO ZA KIMALEZI NI PANA SANA ILA WANAOUMIA KWA ASILIMIA KUBWA NI WATOTO. MAUMIVU YA WATOTO HAWA YANAWEZWA KUSABABISHA MATUNDA MABAYA SANA KATIKA VIZAZI VIJAVYO.

MFANO WA MAMBO AMBAYO YANAENDEKEZA MALEZI MABOVU KWA MTAZAMO WANGU NI KAMA IFUATAVYO, UKIJUMUISHA JAMBO MOJA WAPO ULILOGUSIA MTOA MADA;
1. KUGAWANA MAJUKUMU YA ULEZI KULINGANISHA KIPATO (KIUCHUMI) KATI YA WAZAZI/WALEZI.
2. KUTOKUWA NA USHIRIKIANO WA WAZAZI KATIKA MAMBO YA KIFAMILIA HADI KUAMBUKIZA WATOTO.
3. KUTOKUWAPA WATOTO HAKI YA KUSIKILIZWA WANAPOKUWA NA HISIA JUU YA MAMBO YAO.
4. WAZAZI/WALEZI KUWA NA UKALI SANA USIOJENGA FIKRA ZA WATOTO VIZURI.
5. WAZAZI/WALEZI KUWA NA UPOLE ULIOVUKA MPAKA KUFANYA WATOTO KUJISAHAU.
6. WAZAZI/WALEZI KUKAA MBALI NA WATOTO, LABDA KIKAZI,KIBIASHARA AU SITOFAHAMU BINAFSI.
7. WAZAZI KUVURUGA NDOA ZAO WENYEWE KWA VITENDO VYA USALITI, UHAWARA N.K
8. WAZAZI KUFARIKI GHAFLA NA KUACHA PENGO KWA WATOTO CHINI YA WALEZI WASIO WAZURI.
9. WAZAZI/WALEZI MATENDO YAO HUAMBUKIZA WATOTO, MF; ULEVI, UZINZI, MAPIGANO N.K
10. WAZAZI/WALEZI KUENDELEZA MILA NA DESTURI ZISIZO KUWA NZURI KWA WAKATI ILIOPO, MF; UKATILI, USHAURI N.K
11.WAZAZI/WALEZI KUSHIKILIA MAMBO FULANI YA KIDINI YASIYO KUWA NA MASHIKO KIMALEZI, MF; UNYANYASAJI, USIKIVU, MSAADA, UPENDO N.K
12. WAZAZI/WALEZI KUTOA UHURU ULIOPITILIZA KWA WATOTO WAO NA KUTOA MIANYA IYAKUJA KUWAPA SHIDA WAO WENYEWE NA JAMII KUWAREKEBISHA. MF; UTANDAWAZI
13. WAZAZI/WALEZI KUTOFANYA KAZI/KUJI SHUGULISHA KWA BIDII NA KUACHIA WATOTO KUKIMBIA HALI DUNI NJE YA JAMII.
14. WAZAZI KUPATA WATOTO WALIKUJA DUNIANI BILA MATARAJIO YAO MAALUMU NAKUWEPO MAMBO YA LAANA AU MIKOSI.
15. WALEZI WALIOKOSA UPENDO WA DHATI KWA WATOTO WALIOACHIWA NA MAREHEMU NDUGU/MARAFIKI ZAO.
16. WAZAZI/WALEZI KIPINDI CHA NYUMA WALIPITIA MALEZI MABOVU NA PIA KUAMBIKIZA HALI HIYO KAMA MATOKEO KWA WATOTO WAO PIA. (MTOTO WA NYOKA, NI NYOKA).

NB: NINGEPENDA NIISHIE HAPA NA PIA SIKUTAKA KUFAFANUA SANA NADHANI NIMEGUSIA TU MADA, ILA SIJAPONDA WALA KUKATAZA DINI, SHERIA AU TARATIBU ZA MILA FULANI. CHA MSINGI TUWE NA HOFU JUU YA MATOKEO MABAYA YA MALEZI KWA WATOTO, KUWA NA HOFU NJEMA YA MUNGU, KUELEWA VYEMA MILA NA DESTURI NZURI NA MBAYA, KUFAHAMU NA KUHESHIMU SHERIA ZINAZOLINDA HAKI ZA WATOTO.

PEACE & LOVE
 
PERSONALLY NISINGEPENDA MALEZI NILIYOPITIA WATOTO WANGU NAO WAPITIE, NA IMANI KWA KILA MTU ITAKUWA VIVYO HIVYO KWANI NYAKATI ZA KIMAISHA ZINATOFAUTIANA. KILA UZAO UNA MAPITO YAKE NA WAJAO MBELENI YAO PIA YAPO MENGINE MAPYA WATAKUMBANA NAYO. KWAHIYO NI KUBOBEA ZAIDI KATIKA MAWASILIANO NA VIZAZI VYETU VIZURI KWANI TAARIFA SAHIHI KATIKA MASWALA SAHIHI NI TIBA KWENYE MDA SAHIHI WA MAMBO YANAVYOKWENDA.

I COULD ENCOURAGE WALE NA MIMI AMBAO BADO HATUJAANZISHA FAMILIA NA WALE AMBAO MATHALANI WAMO NDANI YA FAMILIA ZAO TUWE TUNAFANYA TAFITI ZA MABADILIKO KWENYE ULIMWENGU WETU NA KUAANDA TAARIFA SAHIHI KATIKA KUJENGA JAMII BORA. FAMILIA IKIWA BORA NA JAMII/ULIMWENGU UTAPA SULUHU, KWA SABABU MALEZI NA MIFANO HUANZIA HUMO.
 
Nachukua strengths ktk malezi yangu ya utoto naachana weakness. Binafsi hii ni kipindi cha kusahihisha makosa na kujenga kizazi bora zaidi cha baadae.
 
asante sana mkuu Hammaz kwa maelezo bora sana

Lakini mkuu unadhani wewe binafsi utu wako ulivyo leo ni matokeo ya vile ulivyolelewa au kiasili tu wewe uko hivyo? ungpenda watoto wako uwalee kama ulivyolewewa? unahisi kuna vitu vinamiss katika malezi yako?
 
Malezi yalikua mazuri labda kuboresha vichache

Still, perfection cannot be attained
Sure mami uko sawa kabisa

huwezi pata perfection mahali poopote leo

But nilitaka leo tulijadili hili na tuone limekaaje as nimekutana na visa vingi kuna watu hata kuchangamka kwwako ni shguhuli,ukiuliza unakuja kaumbiwa viboko vilizi,kufanyishwa kazi ngumu na nyingi utotoni

hivyo nikawa najiuliza ikiwa kuna watu ambao wanahisi nyutu zao zimeathririwa eiza chanya au hasi kutokana na malezi waliyoyapitia na ikiwa wanatamani kuwale watoto wao kama walivyolelewa au wanatamani kubadilisha kitu katika melzi yao
 
Ah asante sana kwa salamu mkuu Diaspora Jay nimezipokea kwa mikono miwili kabisa

uko sawa kabisa mkuu watoto wengi huiga kile ambcho wazazi wao hufanya

lakini mkuu kuhusiana na vile wazai wanawatendea watoto wao unadhani inaathiri shaping ya mtoto?achilia mbali watoto kuiga wanachokiona?

mfano wazazi kukosa muda wa kuspend na watoto wao,fimbo za kupita kiasi,kupuuzia maendeleo ya mtoto n.k

na vipi kuhusu wewe binafsi mkuu unadahni utu ulionao umetokana na malezi uliyopewa au umerithi tu?na je ungependa kule wattoto wako kama ambavyo wewe ulilelewa?
 
Shukrani sana mkuu BAK am humbeled kwa kweli

Mkuu kuna wakai Maisha yanatuchanganya mpaka basi yaani unapotea weee mpka ukiingia tena JF unaanza upyaaa unajiona mgeni kabisaaa

Ntajitahidi mkuu kupitia pitia licha ya mchanganyiko wa Maisha
 
Reactions: BAK
ujue nini mkuu Hammaz mi sio mtaalamu wa mambo hayo ya kibaolojia na sayansi kwa jumla,lakini huwa nasikia wanasema kuna tabia za kurithi,sasa swali linakuja utu wa mtu unatokana na tabia za kurithi au hasa malezi anayopewa na wazazi wake?
 
I love my mom,never raise her hand kutupiga...sio kama wamama wengi wanoko...lol!..nitatumia the same approach kulea wanangu...no kiboko na Maisha yanasonga… I LOVE YOU BECKY...
Hongera sana mami Rebeca 83 kwa kuwa na mama mzuri na kuwish ulee watoto wako kama mama yako alivyokulea,ni ishara kuwa ni malezi bora sana

lakini mami unahisi kuwa malezi ya mama ya bila kiboko hata kidogo yamekuathiri kwa nama yoyote ile?au yamekujenga ukawa na utu Fulani labda mzuri au mbaya,labda kama kuwa na upendo au kuwa mdekaji au kuwa mwenye huruma n.k
 
Asante sana Saint anne kwa ushuhuda wako

umesma mile hali ya kupenda mwenyewe kukaa peke yako imekuathiri na umesema hukuwa ukikatazwa ila nini we mwenyewe ulipenda

so hapo hakuna nafasi ya malezi ya baba na mama

mfano mami kwenye kipengele cha kutoaswa kuhusu wanaume unadhani imekuathiri utu kwa namna moja ama nyingine?

unadhani kuna aina Fulani nyingine ya malezi ambayo mama na baba walikupa imeathiri utu wako mpaka sasa?

mwisho mami naomba nikutakie kila lakheri katika malezi yako,na kama ulivyosema ni kweli kabisa palipotokeza gap tusiruhusu gap tena litokee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…