Huyu atakuwa Mmama wa bongo movie kwani mimi Mama yangu hajawahi kuniambia haya hata siku moja, ni mke wangu tu huwa anakuwa na maneno machache uliyo andika humu so I guess katoa kwak au huko mitaani. Nikichelewa kurudi nyumbani utamsikia kakulisha nini leo? Simjibu kwani najuwa anamaanisha nani n nini lengo lake. Akiona sina jibu ananifuata chumbani na kunisachi change, akikuta hakuna utamsikia yaani baba wewe huna hata huruma, hela zote umemuachia yeye? Yaani ni full vituko....nikila na kuita watoto tule wote utamsikia, unawaitia watoto ili ukale kule? Yaani hapa sina hata hawara na sijafikiria kuwa naye kwani nampenda sana mke wangu ila vituko vyake tu ni muziki shinda Twanga Pepeta na ndicho kitakachonikimbiza kwake.