witnessj
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 28,704
- 47,260
Wee jamaa kichwani kwako kumejaa busara tupu yaan...Ukombozi wa maisha yako utaanza pale utakapojua kuwa wewe ndio nahodha wa jahazi la maisha yako.....umakini na umahiri wa kupiga makasia ndio vitakufikisha pwani salama!!!.....
Maoni ya watu na utashi wa watu wengine haviwezi kuyaongoza maisha yako vyema pasi na busara zako kwenye kufanya maamuzi na kuwajibika na matokeo ya maamuzi yako!!!....
Hatupo duniani kuwafanya watu wafurahie Matendo yako bali kwa wewe kuwa makini na matendo yako yasije kuyaangamiza maisha yako!!!....
Think big take control of your destiny
Kudos mkuu