Hivi inaonekana hii michezo ya Bahati Nasibu inalipa sana kwa wale ambao wamewekeza pesa zao katika mchezo husika.
Lengo la Kutaka Kuandika Uzi Huu ni kutaka kujua ni Hatua gani watu wanaowekeza Pesa zao kwenye Michezo kama BIKO na TATU MZUKA hufuata maana wanatengeneza faida kubwa sana ndani ya mda mfupi.
Mfano kwa hesabu ya kawaida Endapo kila siku wakawa wanacheza watu kama laki moja kwa kadilio la chini la watu Kwa shilingi 1000 wanakuwa wametengeneza kama million 100 kwa maana hiyo kwa wiki wanakuwa na million 700 ambapo wao mshindi wa pesa nyingi hutoka kila mwisho wa wiki ambapo hueza kushinda million 80-100
Nawashindi wa kila siku ndani ya wiki hawawezi shinda zaidi ya million 50
Kwa maana hiyo na baada ya kodi ya serikali faida ambayo inaweza baki kwa kadilio la chini ni kama million 300
Hasa Ndugu zangu ni hatua zipi inatakiwa ili uwezewekeza pesa huku kwenye TATU MZUKA na BIKO maana kuna faida
Asanten