Wote nii mashuhudaa wa taarifa za mapinduzi ya kijeshi sehemu mbalimbali duniani hasa Africa kwa nyalati za sasa.
Binafsi nimekuwa najiuliza haya mapinduzi huwa yanafanyikaje ili hali Jeshi huwa lina askari wengi tena katika sehemu mbalimbali za nchi.
Kwa mfano, kikosi au vikosi katika mji mkuu wa nchi vikoamua kuasi, vikosi katika maeneo mengine ya nchi vina nafasi gani katika kuzima uasi?
Kwa maneno mengine, inawzekana vipi uasi ufanywe na kikosi au vikosi vichache then Jeshi lote mara moja liwe chini ya kiongozi mmoja wa haya mapinduzi?
Na zaid huwa inawezekana vipi wanajeshi wa vyeo vidogo tu kupindua serikali?
Kwa mfano, Samweli Doe aliongoza uasi akiwa na cheo kidogo to tu cha Sergeant.
Mwenye uelewa atusaidie.