Tuelimishane: Mapinduzi ya kijeshi hupangwa na kufanyika vipi ili hali majeshi huwa na vikosi vingi tena sehemu tofautitofautoi za nchi?

Tuelimishane: Mapinduzi ya kijeshi hupangwa na kufanyika vipi ili hali majeshi huwa na vikosi vingi tena sehemu tofautitofautoi za nchi?

Status
Not open for further replies.
Kwahiyo kiongozi wa kiraia anaweza kupanga mapinduzi ya kijeshi?
Hata si kiongozi tu, Pius Rugangira (Uncle Tom) alikuwa mfanyabiashara na ndio alifadhili jaribio la mapinduzi ya Nyerere la mwaka 1982.
Yeye alikuwa hataki ujamaa na alijua huo mfumo ni wa kimaskini
 
Wote nii mashuhudaa wa taarifa za mapinduzi ya kijeshi sehemu mbalimbali duniani hasa Africa kwa nyalati za sasa.

Binafsi nimekuwa najiuliza haya mapinduzi huwa yanafanyikaje ili hali Jeshi huwa lina askari wengi tena katika sehemu mbalimbali za nchi.

Kwa mfano, kikosi au vikosi katika mji mkuu wa nchi vikoamua kuasi, vikosi katika maeneo mengine ya nchi vina nafasi gani katika kuzima uasi?

Kwa maneno mengine, inawzekana vipi uasi ufanywe na kikosi au vikosi vichache then Jeshi lote mara moja liwe chini ya kiongozi mmoja wa haya mapinduzi?

Na zaid huwa inawezekana vipi wanajeshi wa vyeo vidogo tu kupindua serikali?

Kwa mfano, Samweli Doe aliongoza uasi akiwa na cheo kidogo to tu cha Sergeant.

Mwenye uelewa atusaidie.
Unajua Code X wewe?
Turn it to Blue for the litmus Red
 
Ni kwamba Wote mnajaribu tu Kubashiri majibu, ila ukweli haupo Ivyo Kuna Mengi huwa yanafanywa kupitia ngazi Mbali mbali za Kiusalama kunakuwa na Mkono wa Baraka kutoka kwa wana Usalama Waaminifu Wenye Nguvu kutoka Sekta Nyeti zote za Usalama wa Nchi.

Wale wanaotumia Njia ya Jeshi Huwa wanafanya ivyo sababu Jeshi ndo Wenye Dhamana Ya kulinda Mipaka Ya Nchi na Nchi. Ila zipo Njia Zaidi za Mapinduzi ikionekana Rais aliyepo anaelekea sipo moja wapo Ni Iliyofanyika hapa kwetu.

Wangeweza kutumia Njia ya Mapinduzi ya kijeshi Ila Ingejenga Mbegu mbaya hapo Mbeleni Kwani ingekuwa ni Suala endlevu ila ikaamulika kutumia Njia isiyo na mbegu mbaya Hapo Mbeleni hata kama WanaNchi wataijengea mashaka!

Naomba nisifunguke Zaidi ya hapo. Ila Ukweli ni kwamba Mapinduzi mengi huwa yana Baraka kutoka Sekta zote za Usalama wa Taifa husika
 
Kuna mdau mmja kasema hapo kwamba Mwendazake alikoswa koswa.mara 2 kama Kina Nyerere nadhani hii huenda ndio imepelekwa marekebisho ya sheria ya idada ya usalama kuwa chini ya ofisi ya Rais yaani kuongeza role ya Rais hapo ndani.

Intelligence ikifeli hakuna stability ya Nchi.
Intelligence ni veins na capillary.... unaweza kuudhibiti mfumo na intelligence ika comply.....
 
Mapinduzi ya Africa Huwa ni upuuzi kuliko faida Wala hawapindui Kwa maslahi ya Nchi Bali ya kwao.

Mfano hapo Niger huyu Kiongozi wa Mapinduzi alimegewa ubuyu kwamba Rais anapanga kumpiga Chini kumbe akamuwahi Sasa huu ni upuuzi wanaoshangilia Huwa ni manyumbu wasioelewa wanachoshangilia.

Kiufupi Wanasiasa wanaweza furahia hasa wa upinzani wakidhani kwamba wanaweza pata fursa ila ni ngumu.

Pia angalia Egypt baada ya Upinzani kushinda na Jeshi haliwataki wakaipundua hivyo hivyo na MiyMar
Kama ilikuwa ni yeye kupigwq chini, kwanini Jeshi zima limekubali haya yatokee? Je, si labda kiongozi wa kiraia aliekuwepo alikuwa hakubaliki mpaka Jeshini?
 
Kama unaonegelea mapinduzi ya Afrika magharibi, yanasabishwa na ubaguzi wa ukabila tu. Hakuna zaidi.

Na mapinduzi yote ya Afrika ukiyatazama utaona yamesababishwa na ubaguzi tu, hakuna zaidi.

"Divide and rule" inatumika na tunaotumika kupinduwana kuuwana na kuchukiana ni Waafrika wenyewe kwa ujinga wetu.

Na Tanzania mbegu za ubaguzi zimeshaanza kupandikizwa, kwa kasi sana.
Mapinduzi ya Nigeria hasa ndio yana udini na ukabila. Wote wale kina Sani Abacha, Babangida, Yakubu Gowon, Buhari na wengine walifanya mapinduzi kwa fikra za kidini na kikabila ndio maana Nigeria ilipata mapinduzi mara nane.
 
Kama ilikuwa ni yeye kupigwq chini, kwanini Jeshi zima limekubali haya yatokee? Je, si labda kiongozi wa kiraia aliekuwepo alikuwa hakubaliki mpaka Jeshini?
Inategemea na structure ya Uongozi wao Hadi kumpata hiyo nafasi.

Sasa kama yeye anasikilizwa zaidi unategemea nini? Pakistan Kwa Mfano Imran alivyopinduliwa kwani hakubaliki?
 
Kuna mdau mmja kasema hapo kwamba Mwendazake alikoswa koswa.mara 2 kama Kina Nyerere nadhani hii huenda ndio imepelekwa marekebisho ya sheria ya idada ya usalama kuwa chini ya ofisi ya Rais yaani kuongeza role ya Rais hapo ndani.

Intelligence ikifeli hakuna stability ya Nchi.
Kwani mkuu usalama wa taifa ilikuwa wizara ya mambo ya ndani hapo kabla?
Yote yaleyale, Cuba ile DI yao iko chini ya wizara ya mambo ya ndani na imefanya missions nyingi sana duniani na imezuia mapinduzi mengi na makini ya majaribio ya kumuua Fidel Castro.
 
Pamoja na mambo mengine ni aina ya watu unaowapa vitengo nyeti how Royal they are kwako na structure ya hiyo intelligence Yako bila kujalisha Iko chini ya nani..

Inaweza Kuwa chini ya Wizara Fulani yet Kuna ma informer wanaoripoti otherwise Kwa Rais kuwa monitor so hakuna kitu mtafanya.

Weak ,corrupt intelligence ndio xinasananisha hayo.
 
nafikiri ni jinsi walivyounda majeshi yao.... Lakini kwa nini, wanajeshi wengine huwa hawajitokezi kupinga..Nafikiri , hapa kuna ukosefu wa mawasiliano, wanakuwa hawajui waliofanya haya ni akina na wana nguvu kiasi.
 
Wote nii mashuhudaa wa taarifa za mapinduzi ya kijeshi sehemu mbalimbali duniani hasa Africa kwa nyalati za sasa.

Binafsi nimekuwa najiuliza haya mapinduzi huwa yanafanyikaje ili hali Jeshi huwa lina askari wengi tena katika sehemu mbalimbali za nchi.

Kwa mfano, kikosi au vikosi katika mji mkuu wa nchi vikoamua kuasi, vikosi katika maeneo mengine ya nchi vina nafasi gani katika kuzima uasi?

Kwa maneno mengine, inawzekana vipi uasi ufanywe na kikosi au vikosi vichache then Jeshi lote mara moja liwe chini ya kiongozi mmoja wa haya mapinduzi?

Na zaid huwa inawezekana vipi wanajeshi wa vyeo vidogo tu kupindua serikali?

Kwa mfano, Samweli Doe aliongoza uasi akiwa na cheo kidogo to tu cha Sergeant.

Mwenye uelewa atusaidie.
Kuna Wakati mkiwa na Matatizo halafu akaja mtu akawaambia "shetani naweza kutatua tatizo lenu, hata kama Imani yenu iko juu mtakubali tuu"

Kiongozi wa Nchi unafanya mambo ya hovyo, wanaokulinda unakuta wa uwezo na ufahamu mara10 zaidi yako lakini wanaamua kulinda viapo vyao

Unaharibu maisha Yao na wategemezi wao

Yaani Taifa linapokuwa kwenye mtanziko mkubwa wahanga wa kwanza ni wale wanaotegemea mshahara kwa sababu macho ya yamii yake yote yatageukia kwa mwenye Ahueni

Hivyo unakuta mlinzi anaanza kuishi kwa stress ya kulea Familia nyingi mtaani ambazo ugumu wa maisha unesababisha wewe Kwa kushindwa kusimama na kulinda maslahi ya Taifa Zima

Kibaya zaidi, unaanza kutumia walinzi Hao Hao kubadili katiba ili utawale milele

Kwa maana hiyo akitokea mtu akasema ana njia ya kuondoa obstacle hiyo ataungwa mkono tuu

Wakati wa kutangaza kumpindua na kueleza kwa kina kwanini mmefikia hatua hiyo na nini kinafuata utapata uungwaji mkono kila kona
 
Katika zile nguzo5 , nguzo mbili tu ndio zinafanikishs jambo la aina hiyo.
Siri na ujasiri.

Katika ile timu ya uongozi wa kama kuna mwenye tabia za kuonekana anasaport utawala unaoumiza watu.

Basi hata angekua jeneral basi kitu chakwanza anaongezewa ulinzi maalum na wiki hiyo anajikuta ulinzi anaopewa haruhusiwi kukutana na kiongozi yoyote mwingine.

Waliobaki wanatulia..

Asubuhi kukicha viongozi oote wa vikosi wanapewa amri ya kulinda sehemu zote muhimu bila kuruhusu mtu kutoka, ukiinga kutoka huruhusiwi.

Bandari, ikuru, viwanjawa vya ndege mipaka bank kuu nk.hivyo ni amri inahusisha jeshi zima, mbaya zaidi wale wa vyeo vyachini siku hiyo watapewa maelekezi (amri) wa tatekeleza bila ya kujua wala kuhoji .

Wakihakikisha sehem zote zinalindwa kwa amri maalum kuna timu na kiongozi anaetangaza mapindizi watakua tayari kwenye kituo cha redio chs taifa.

Wanannchi mtashangaa vituo vyoote vya redio na televission zinaimba wimbo wa taifa tayari kwa jeshi kutangaza dhamira.

Wakimaliza viongozi oote wa kiserkali wataitwa kujisalimisha sehem wanayotaka na ukibisha wakikufuata kitachokukuta usimulaumu mtu.

NB. mapinduzi kwa dunia ya leo mapinduzi hakiwezi kua kitendo cha kudumu kwasababu, utakua umekiuka sheria na mikataba ya umoja wa mataifa .lakini pia muungano wowote wa nchi ya inavunjika.

Kwa mfano ukifanya mapinduzi africa.ujue umoja wa africa unakutenga tayari.ndio maana unaona wakishapindua wanaruhusu uchaguzi mwingine kwa haraka ikiwezekana.hivyo tunakoelekea mapinduzi ya hivyo yatakoma.
 
nafikiri ni jinsi walivyounda majeshi yao.... Lakini kwa nini, wanajeshi wengine huwa hawajitokezi kupinga..Nafikiri , hapa kuna ukosefu wa mawasiliano, wanakuwa hawajui waliofanya haya ni akina na wana nguvu kiasi.
Wenzio wanawahi kushika kwenye mpini wewe wa kwenye makali utapinga saa ngapi? Kuna mtu anataka kufa kirahisi hivyo?
 
Kwa kifupi

Mapinduzi ya Kijeshi mara nyingi huwa na mazingira ambayo asilimia kubwa ya Jeshi huwa wapo tayari kuyaunga mkono.
Ikiwa sivyo lazma jaribio lifail.
Nchi nyingi tu majaribio hufail,au likifanikiwa na hakuna consensus ndo inakuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe. Mfano wakati wa Magufuli majaribio yamefeli Mara 2 japo haikujulikan sana
Mie huwa ninajiuliza,hivi wewe ulizaliwa kwa kipitia tundu gn?
 
Kuna Wakati mkiwa na Matatizo halafu akaja mtu akawaambia "shetani naweza kutatua tatizo lenu, hata kama Imani yenu iko juu mtakubali tuu"
Kiongozi wa Nchi unafanya mambo ya hovyo, wanaokulinda unakuta wa uwezo na ufahamu mara10 zaidi yako lakini wanaamua kulinda viapo vyao
Unaharibu maisha Yao na wategemezi wao
Yaani Taifa linapokuwa kwenye mtanziko mkubwa wahanga wa kwanza ni wale wanaotegemea mshahara kwa sababu macho ya yamii yake yote yatageukia kwa mwenye Ahueni
Hivyo unakuta mlinzi anaanza kuishi kwa stress ya kulea Familia nyingi mtaani ambazo ugumu wa maisha unesababisha wewe Kwa kushindwa kusimama na kulinda maslahi ya Taifa Zima
Kibaya zaidi, unaanza kutumia walinzi Hao Hao kubadili katiba ili utawale milele
Kwa maana hiyo akitokea mtu akasema ana njia ya kuondoa obstacle hiyo ataungwa mkono tuu
Wakati wa kutangaza kumpindua na kueleza kwa kina kwanini mmefikia hatua hiyo na nini kinafuata utapata uungwaji mkono kila kona
Mapinduzi ni uhaini na njia ya kienyeji ya kuchukua madaraka na Iko kinyume na Katiba ndio maana inapingwa all over the World.

Na lengo la kutengwa na kuwalazimisha kurudi Kwenye mstari kwamba watu mkipata Cha moto mtapata akili.

Mwisho mapinduzi mengi yameleta hasara kuliko faida ndio maana tunayalaaani
 
Pamoja na mambo mengine ni aina ya watu unaowapa vitengo nyeti how Royal they are kwako..
Muhimu ni kufuatilia sio kuamini watu tu. Kufanya ufuatiliaji na kuwa very fast kufanya maamuzi, mapinduzi yanatokea ndani ya masaa machache zile movements za mwanzo zikijibiwa ipasavyo unazima jaribio.

Kwanza majeshi huwa hawapendi kupigana yenyewe kwa yenyewe, unless yawe yamegawanyika kimakabila na kidini. Kule Nigeria ndio ilikuwa inakuwa Rais kabila la Igbo anaweka General na Lt. General na kujaza Major Generals & Brigedia Generals wa kabila lake kisha anachanganya na wa makabila mengine vilaza wale ndio mzee wasio na uwezo hivyo watakuona Mungu mtu kwa kuwaokota. Mfano mchukue Mwijaku mpe ukuu wa wilaya hata ukimwambia vua nguo tembea uchi kwenye kampeni anaweza. Sasa huyo anakuwa mwaminifu sana haijalishi Rais unawachukia watu wa Kigoma kiasi gani, anajua wakija wao yeye hana vigezo kiuhalisia hivyo atatemwa.

Kwenye majeshi yenye umoja, hawapendi kugombana hivyo huwa wanaenda upande utakaoonekana kushinda. Pale Urusi mwaka huu wakati Wagner wanaenda Moscow majenerali wa Urusi na vikosi vyao ni kama walipooza wakisoma response ya kwingineko mpaka vikosi vikaanza kuongezwa kutoka military districts nyingine na mpaka mwisho Rais wa Belarus akafanya makubaliano na Prigozhin. Majeshi ya Ufundi yalikuwepo ila sasa unaenda iunga mkono serikali kumbe majenerali wenzako wamekula njama kuikataa, unakuwa hujui hivyo unasikilizia upepo usije achwa kwenye mfumo au ukawa overpowered kwenye mapigano.
Jaribio lilikuja kuzimwa masaa kadhaa baadae na sababu lilikuwa nje kabisa na mji mkuu ila lingekuwa Moscow palepale mapigano makubwa zaidi yangetokea.

Gadaffi alifanya mapinduzi kwa namna hii, alikuwa ni Kanali akafanya mapinduzi majenerali wakadhani ni mmojawao kafanya hivyo wakasita kupigana. Hakutangaza kwanza maana wangejua ni yeye Kanali wangejiamini kumzuia. Yakawa yamepoa ndio akajitokeza. Wanapeana codenames hujui nani anaongoza, na Kanali anayeongoza anaweza jifanya yuko chini ya Jenerali fulani kwa kuwadanganya. Unakuta serikali inabaki na trust issues, umuagize Major fulani akaweke vikosi television ya taifa au naye ni miongoni mwa wanaoasi.
 
What if msuya diwani ..Anyway ina maana bi mkubwa hakuwa comfortable kufanya nae kazi akiwa bigboy wa special branch akaamua kumstep off the throne?
Sasa Kuna Rais Huwa anafanya kazi na watu ambao sio yeye kawaweka? Unless awe alikuwa na uhusiano mzuri Toka kitambo yaani mnafahamiana vizuri japo sio guarantee maana Kuna watu wamepinduliwa na rafiki zao.

Lazima niweek watu naowaamini na ambao tunaweza kuwa kwenye mlengo mmja.

Pia unaweza Kuta wewe unaamini itikadi hii yule anaamini vinginevyo Sasa hapo kutakuwa na Ugumu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom