Tuendako hali inatisha. Sasa maharage yanakimbilia kilo moja elfu 4 (4,000)

Tuendako hali inatisha. Sasa maharage yanakimbilia kilo moja elfu 4 (4,000)

Duh kwahio haya mambo ya uhaba wa Mvua na Ukame ni mambo mageni ? , Kwamba Mvua na hizi tabia nchi sio za kutegemea ?, Kwanini Serikali isijitayarishe for the worse ?!!!

Ndugu yangu, unakuwa kama huijui serikali yetu ya mavieitiiii...

Inachoweza kukuhakishia wewe ni kukupiga tu siasa za "tunajenga mazingira ya kilimo tija...", "tunatoa mwanya kwa wakulima....", "tutatoa ruzuku..." n.k
 
Dah kuikweli Hali ni mbaya kila kitu kinapanda Bei tunakoenda hata Kodi za pango zitaongezeka ....hapo hapo unakuta majitu yanajipitisha Mara hela ya ulinzi shirikishi Mara hela ya taka siku....wanaowatuma siku watakuja waokote mizoga yao mtaani ...watu wamechoka
Utakuwa unakosea sana
 
Ndio nimekwambia hatuwezi wote tukawa wakulima tunategemeana, ni sawa na wewe uzungumzie ubovu wa elimu au gharama kubwa za ada za shule halafu et suluhisho uwaambiwe ukawe mwalimu ili ufundishe vizuri na kwa ada nafuu au ukizungumzia gharama kubwa za matibabu uwambiwie ukawe daktari.
Thought 👏👏
 
Shida imeanzia mbari. 2010 Rais Kikwete aliingiza Mahindi sokoni , hifadhi ya taifa ya chakula, Tena mahindi yale mengi yalitolewa kwa wenye viwanda vya kusaga vikubwa na kuelekeza Bei.

Kwa kiasi kikubwa Ili leta nafuu kwa mwananchi.

Kumbuka uwezo wa hifadhi ya taifa kipindi ilikua 200,000T kwa mwaka 2005 kufika 2015 ilikua 400,000,T nahaokua ya biashara . Baada ya hapo niwakala wa chakula sio hifazi Tena .Tani za mahindi alizo acha KiKwete ziliuzwa Zimbambwe 2017 na baada yahapo bodi yamazao mchanganyiko ilinunua mtama kwa maeneo unako sitawi na mpunga kwa baazi ya maeneo. Tayali tulisha poteza akiba ya nafaka mhim.

Mother alifanikiwa Kununua mahindi msimu ulio.
Msimu huu Sina hakika kama amenunua japo Bado sitoo Zima mzigo. Anasikilizia kuona Khali inaendaje watu wasije kufa kwa njaa.
Baazi ndo nini?! Hivi mlisoma Shule gani ninyi vila.za?! Ni Baadhi✓
 
Kulima kwenyewe mbolea bei juu, waiivisha walanguzi wanaenda kulangua unazani nguvu tena zinatoka wapi? Vijana nao wanakimbilia mjini kutembeza karanga ,mara soksi unazani analima nani huko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimempa ushauri afanye option nyingine zaidi ya maharage sababu zipo mboga bei nafuu zaidi ya maharage...
Mchicha fungu mia tatu, bamia fungu mia tano, dagaa robo kilo elfu mbili,tena hizi unakula hata siku tatu kama unapiga mix ya dagaa, mchicha, bamia, nyanya Chungu na mazaga zaga mengine.
 
Kuna ambao tunapenda maharage. Options zipo lakini kupanda kwa bei lazima kusemwe.
Je na hizo Options nyingine zikipanda bei itakuaje? Kila chakula kina umuhimu wake
Option ni kila mtu mwenye walau kieneo kidogo alime bustani ndogo, na wengine wenye uwezo walime mashamba nje ya miji wanakoishi. Huu muda wa kwenda gym [emoji3571] au ma bonanza watu wautumie kwenda kibaha, Mkuranga na kwingineko watafute mashamba walime jamani.
 
... kuna mtu ana watoto 10 na wake wanne karne hii? Kuna mahali pana biashara ya kuuza watoto?
Umewahi kufika kwenye vijiji walipo wasukuma huko Katavi mkuu? Hao 10 ni kidogo
 
Yote haya, tunayataka sisi wenyewe watanzania, na bado, hali itakuwa tete zaidi ya hii.
 
Option ni kila mtu mwenye walau kieneo kidogo alime bustani ndogo, na wengine wenye uwezo walime mashamba nje ya miji wanakoishi. Huu muda wa kwenda gym [emoji3571] au ma bonanza watu wautumie kwenda kibaha, Mkuranga na kwingineko watafute mashamba walime jamani.
Wote tukilima kazi nyingine nani atafanya? 😅
 
Back
Top Bottom