Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeuliza kwani lazima tule maharage?
Nitolee upumbaavu wako nenda kalime, kwani neno langu ni sheria?Jinga ww kwahy wote wakifuata huu ushauri wako hao wajinga wenzako watanunua wap muwe mnatumia akili
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna ambao tunapenda maharage. Options zipo lakini kupanda kwa bei lazima kusemwe.Nimempa ushauri afanye option nyingine zaidi ya maharage sababu zipo mboga bei nafuu zaidi ya maharage...
... kuna mtu ana watoto 10 na wake wanne karne hii? Kuna mahali pana biashara ya kuuza watoto?Hatari na nusu mwaka huu chupi lazima zivuke imagine una wake wanne na watoto 10 halafu huna mishe za kueleweka lazima usaidiwe kutoa dozi maana nguvu za mashaka.
Kuna ambao tunapenda maharage. Options zipo lakini kupanda kwa bei lazima kusemwe.
Je na hizo Options nyingine zikipanda bei itakuaje? Kila chakula kina umuhimu wake
Duh kwahio haya mambo ya uhaba wa Mvua na Ukame ni mambo mageni ? , Kwamba Mvua na hizi tabia nchi sio za kutegemea ?, Kwanini Serikali isijitayarishe for the worse ?!!!Hatuwezi kuzuia kupanda bei ya vyakula, hata serikali haiwezi kuzuia kwa kuwa uzalishaji umeshuka kutokana na uhaba wa mvua, hata serikali hai...
Individually tuna wajibu wa kujisaidia ila Serikali pia watumishi wetu tunaowalipa inabidi waje na njia mbadala...,Sasa sisi kama walaji yatupasa tutafute vyakula mbadala tu hakuna jinsi...
La hasha nunua stock nyingi weka ndani wakati ambao bei ni nafuu, lakini hatari ya kustock vitu vikavu muda mrefu ndio hiyo nilitaja uwezekano wa kula sumu kuvu...
Wewe akili zipo sio wale wanaolazimisha bidhaa ishushwe bei kwa kufunga mipaka bila kumjali mwenye bidhaa.Duh kwahio haya mambo ya uhaba wa Mvua na Ukame ni mambo mageni ? , Kwamba Mvua na hizi tabia nchi sio za kutegemea ?, Kwanini Serikali isijitayarishe for the worse ?!!!
Individually tuna wajibu wa kujisaidia ila Serikali pia watumishi wetu tunaowalipa inabidi waje na njia mbadala...,
Mfano kuhakikisha kuna maghala hence storage ya kutosha kunapokuwa na over supply (mfano mwaka juzi tu wakulima wamekosa soko kwa kuwa na bidhaa nyingi hadi kuozea mashambani) hence kipindi hicho wangenunua kwa bei nafuu na kuyahifadhi kipindi hiki kwenye scarcity wakatoa mzigo ili kubalance bei.....
Sasa kama hawawezi kufanya hata hili wapo pale kufanya nini ?, Mfanyabiashara yupo pale ku-make as much profit as possible huwezi kumtegemea...
Tule Mboga za majani mchicha haujapanda bei Bado
Mchele umeshuka Bei huku Tandika kilo-moja 2400/ 2200 unapata so ukitaka nunua chakula nenda sokoni Mkuu
Pia hapo nyumbani waambie waishi kwa bajeti kula maharage kila siku sio chakula Bora hata mchicha
Malalamiko, lishwalishwa hawakuishinikiza serikali kununua kwa bei nzuri wahifadhi ili mkulima asipate hasara wanatokwa na mishipa bei ikiwa nzuri tu.(mfano mwaka juzi tu wakulima wamekosa soko kwa kuwa na bidhaa nyingi hadi kuozea mashambani)
Mnajitahidi sana kumtetea mama yenu sisi yetu macho.Shida imeanzia mbari. 2010 Rais Kikwete aliingiza Mahindi sokoni , hifadhi ya taifa ya chakula, Tena mahindi yale mengi yalitolewa kwa wenye viwanda vya kusaga vikubwa na kuelekeza Bei.
Kwa kiasi kikubwa Ili leta nafuu kwa mwananchi.
Kumbuka uwezo wa hifadhi ya taifa kipindi ilikua 200,000T kwa mwaka 2005 kufika 2015 ilikua 400,000,T nahaokua ya biashara . Baada ya hapo niwakala wa chakula sio hifazi Tena .Tani za mahindi alizo acha KiKwete ziliuzwa Zimbambwe 2017 na baada yahapo bodi yamazao mchanganyiko ilinunua mtama kwa maeneo unako sitawi na mpunga kwa baazi ya maeneo. Tayali tulisha poteza akiba ya nafaka mhim.
Mother alifanikiwa Kununua mahindi msimu ulio.
Msimu huu Sina hakika kama amenunua japo Bado sitoo Zima mzigo. Anasikilizia kuona Khali inaendaje watu wasije kufa kwa njaa.
Wapo wengi tu kama wewe una nguvu za kiume za mashaka sema tuje tukusaidie endapo kama una hitaji watoto wengi.... kuna mtu ana watoto 10 na wake wanne karne hii? Kuna mahali pana biashara ya kuuza watoto?
Kwa akili yako ilivyo ndogo unafikiri waathirika wa huu mfumuko wa bei ni kwa wenye familia kubwa pekee.Kama mwanafunzi au bachela alikuwa anaweza kuishi kwa 4500/= kwa siku, sasa inabidi awe na bajeti isiyopungua 8000/= sababu chakula kwa mama ntilie sio buku jero tena na kipato chake hakijaongezeka.Mnapoambiwa mzae kidogo mnaiambia serikali na kutukana mabeberu eti mnatafuta soko la ndani.
Wenye familia ndogo hata hawawaz kuhusu msosi,
Endeleeni kuleta vibarua duniani.
Ukila kachumbari na mboga za majani ndio balaa kwa madawa....nyanya, kitunguu, spinach, mchicha...balaa tupu. Mpaka pilipili wanaweka mbolea na wanapiga dawa.Kula kitu kingine mkuu si lazima maharage.
Kwanza ulaji wa mara kwa mara wa hayo mazao makavu kunaleta udumuvu, mengi huwa na sumu kuvu na madawa ya uhifadhi nafaka.