GE2025 Tuendelee kushiriki mchakato wa uchaguzi mkuu ili tupige kura za uchafuzi mkuu wa taifa letu!!?

GE2025 Tuendelee kushiriki mchakato wa uchaguzi mkuu ili tupige kura za uchafuzi mkuu wa taifa letu!!?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Joined
Apr 8, 2023
Posts
43
Reaction score
29
Kushiriki Mchakato wa Uchaguzi kwa Mtanzania yeyote si jambo linaloepukika hasa kwa sababu huu ni msimu na wakati hasa wa uchaguzi, na kusema kweli kila siku ya kila wiki, ya kila mwezi, kwa kila mwaka tunafanya uchaguzi kwenye mambo mengi; isipokuwa uchaguzi Mkuu wa Taifa letu ilipaswa kuhitimishwa kwa "kupiga na kupigiwa kura" kuchaguliwa na watu kuwa kiongozi wao kwa hiyari ya wapiga kura; hata hivyo kwa hali ilivyo (walau kwa maoni yangu) kwamba unaridhika ama huridhiki, unakubali ama vinginevyo, Utatiki ama unasubiri mageuzi, bado unaendelea kushiriki "Mchakato wa Uchaguzi" maana yote hayo ndiyo hasa yanayokamilisha Mchakato wa Uchaguzi.

Hata hivyo, wakati huo taifa lilipokuwa likiendeshwa kiungwana na kwa vile hoja ndiyo hasa nguvu ya waungwana, hakuna namna tungefanya kana kwamba hakuna hoja za msingi kutoka upande wa upinzani dhidi ya uchaguzi maana ziko na zingepaswa kushindwa kwa hoja bora zaidi badala ya rungu, lakini yaonekana kila siku tunakwenda mbali na uungwana, sasa tunashindanisha hoja na rungu.

Pia kwa vile nadhani kiwango chetu cha uchanganuzi wa masuala kimeshuka na bado tuko kwenye kile mimi hukiita kwa kikoloni (mnisamehe), "the damning down of ideas" kila ukisema "Upinzani" , tunawaza rangi za nguo, kijani khaki, zambarau, njano na nyinginezo, lakini upinzani ni zaidi ya rangi za nguo zenu, sema hoja hiyo hamuitaki kwa dhana kwamba nyinyi mlio na "uchaguzi" wa rangi za nguo, mna akili na haki zaidi kuliko wale tulio na "uchaguzi" wa kutojipambanua na rangi za nguo zenu, bali rangi za bendera ya taifa letu. Mungekubali kufungua macho ya bongo zenu kidogo tu, mungegundua kwamba sote tunashiriki "uchaguzi" ila nyinyi wenzetu mnalazimisha tushiriki "uchafuzi" wa utaifa wetu kwa mahaba ya rangi za nguo zenu. Huo utakuwa "uchafuzi mkuu", lakini Uchaguzi unataka hiyari, siyo maguvu wala ghiliba.

Ebu tujadili hoja kadhaa. Utaratibu ndani ya Kijani unataka "mgombea" agombee, na hata tunapotumia "utamaduni" wa kwamba mgombea aliyekwishagombea na kuongoza kipindi kimoja "apewe fea", bado tunakuwa tunamzungumzia mgombea aliyekwishafuata utaratibu wote na "kuthibitisha kugombea" ikiwamo kupata udhamini kutoka kwa wenye vazi wenzie, na kupigiwa kura, na ndipo kupewa kupepea bendera ya rangi yetu. Sasa huyu tuliyemteua mara hii alijaza fomu za kuomba udhamini wa kugombea kuwa Rais wetu!!? Sina chuki wala ugomvi naye, nashiriki tu "mchakato wa uchaguzi" kutokea tu huku ubanangani kwetu kwa hoja za kibanangabananga wala msinijali!! Kama hakuwahi, bali alipata nafasi ya kuwa Rais wetu kwa "kudra", basi ama tukubali kwamba arejeshwe kwenye mchakato, aombe kutathiminiwa na wanachama wenzake, achakatwe, kisha agombee, ama tukubali kwamba sasa katika zile "Sheria na kanuni zisizoandikwa", na zisizotekelezwa "sisisi", basi kumbe "kudra" ni sehemu ya Sheria hizo. Tukikubaliana hivyo, tutakuwa tumeanza kusogea kwenye uchaguzi badala ya uchafuzi, vinginevyo, tuendelee kushiriki Mchakato wa Uchaguzi ingawa hatutachagua ama kuchaguliwa ingawa hata baadhi yetu wanaweza kupiga kura. Tutachafua, kuchafuana na hata kuchafuliwa kwa kufanya Uchaguzi wa kuendesha uchafuzi mkuu wa Kaya yetu.

Kama tunachagua kuwafunga makanwa wale wanaosema yale tusiyotaka kuyasikia, kama tunaamua kwamba tuwapige wanaoshindana nasi ilhali tumewafunga mikono na miguu na bado tujisifu kwamba tunatarajia "ushindi wa kishindo", kwanini tunapoteza muda na fedha zetu kwenye kufanya viini macho vya uchafuzi kwa jina la uchaguzi!!? Yaani sasa tunatafuta "teknikalitizi" na bado tuna ujasiri wa kuendelea na Mchakato wa Uchaguzi kwa njia ya ghiliba namna hii!!? Ni kwa sababu tunaamini kwamba watu wetu ni wajinga kabisa, au ni kwa vile tunatafuta namna ya kupata usingizi baada ya uchafuzi mkuu kwa kujiambia "Taifa lilishiriki Mchakato wa Uchaguzi" hata kama mioyoni tutakuwa tunajua kwamba tulifanya uchafuzi na kuacha kando uchaguzi wa watu!!? Haya, tuendelee kushirkishana mchakato wa uchaguzi kwa vile hakuna uchaguzi kwenye hilo, iwe kwa kusikia, kuona ama kushiriki kusema au kutenda matendo na maneno ya ama uchaguzi au uchafuzi, bado tutakuwa tumeshiriki Mchakato wa Uchaguzi ingawa tunafahamu sote kwamba mwisho wa siku hatutafanya uchaguzi hata ingawa tutapiga kura; tutakuwa tumeshiriki Mchakato wa Uchaguzi kwa kupiga kura za uchafuzi mkuu wa Kaya yetu.

Ha ha ha ha ha!!! Sina nijualo Nanga miye, nawaza tu kibanangabananga na hizi ni salaam nawasalimia.
 
Back
Top Bottom