Tufahamishane kuhusu engine exhaust (mngurumo)

Tufahamishane kuhusu engine exhaust (mngurumo)

Ukaridayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2012
Posts
515
Reaction score
476
Hbr zenu,

Kuuliza si ujinga ndugu wana JF hasa ktk hili jukwaa letu la magari na vyombo vya usafiri..

Hivi hawa watu wanaobadili muungurumo wa gari zao mathalani IST unaweza kukikuta kinatoa sound/muungurumo mkubwa kama zile za team teza ama team subaru huwa wanazifanyaje?

Je hivi inawezekana tukafanya ule muungurumo wa cruiserV8 kwenye Premio, Yaani premio ilie kama V8??

V8 kwa upande wangu huwa inanivutia sana ule muungurumo wake, wakati mwingine huwa nadhani muungurumo nao una nafasi yake ya kumfanya dereva azidi kuihisi gari yake pindi aendeshapo (mzuka).

Hizo vurugu za kubadilisha hizo exhaust zinafanyika wapi kwa hapa dar??

Nini madhara yake ikiwa muungurumo utabadilishwa!

Nawasilisha.
 
Ah wapi.

Ule mlio huwezi install kwenye vitu vya ajabu ajabu maana unatoka kifuani mwa gari sio puani kama zile takataka zinazofungwa kwenye alteza.
Mkuu,
Ina mana kwa kifupi haiwezekani?

Kuweka mlio mzito kwenye gari ndogo?
 
Hahaha koo mkuu nyingine znabana pua sio. Actually napenda muungurumo wa vx v8 likiwa silencer ule wa kupanda na kushukaa
Unajua likiwa silencer halitofautiani na mlio wa scania ikiwa silencer.
 
Binafsi mimi matoleo yote ya Vx kuanzia 80,100,200 series nayapenda tu kwa sababu ya ile sauti yake kama ya ndama dume
 
Inawezekana kabisa kila gari mlio wa engine ukitoa muffler zina milio karibu inafanana kutokana na ukubwa wa engine kwenye maffler ndio kuna tune ya mlio wa gari kutokana na pendekezo la mtengenezaji sasa wanaobadili milio hubadilisha muffler au exahaust pipe yote na mlio huchange
 
Unajua likiwa silencer halitofautiani na mlio wa scania ikiwa silencer.
Mashine ya V8 inanivuruga sana my mind,, likinguruma ama ukilikuta linapanda mlima mdogo kwenye rough road ndiyo utalipenda kabisa...

Wakati mwingine nilifikiri labda mufler yake ndiyo inayofanya hivyo?

Hatari yake halipatani na mafuta ya kidebe.

Maili 13 kwa lita 4.7 duuu!!!
 
Inawezekana kabisa kila gari mlio wa engine ukitoa muffler zina milio karibu inafanana kutokana na ukubwa wa engine kwenye maffler ndio kuna tune ya mlio wa gari kutokana na pendekezo la mtengenezaji sasa wanaobadili milio hubadilisha muffler au exahaust pipe yote na mlio huchange
Hamisha v8 kwenda kwenya Carina
 
Kuna jamaa wapo kijitonyama ndio wanafanya hio kzi
 
Cruiser ule mlio ni MATATA SANA, ile exhaust ni kama inapiga kamluzi flani hivi AMAZING na ukija kwenye injini especially zile za diesel huwa zina mlio WA KIBABE yani ukiusikikia unajua kabisa MWANAUME WA SHOKA kaingia. Za petroli naziona ziko silence sana japo sijawahi kusikia mtu akii Rev mashine yake.
 
muungurumo upo katika Range Rover utadhani kundi la nyuki linapita walikaa sana chini hiyo ni moja ya mimi kulipenda lile dude..
 
Binafsi mimi matoleo yote ya Vx kuanzia 80,100,200 series nayapenda tu kwa sababu ya ile sauti yake kama ya ndama dume
Aisee hakuna mlio mtamu kama wa landcruiser 80 then inafuatiwa ile ya land cruiser 100. Huwa unanifanya nitamani kumiliki ile gari kwa namna yeyote. Nakumbuka kipindi niko mdogo mzee alikuwa anapush lc 80 mpya ya ofisini kwao SUA. Ile mashine ilikuwa manual with diesel aisee acha tu. Tulikuwa tunapiga nayo tours as well kama kwenda kijiji n.k.
Alikuwa anaipiga chafu mbaya yani ina mzuka balaa kipindi akipangua gears wakati ana reverse na kuipa acceleration. That was when i started knowing and liking land cruisers. Aisee cruiser 80 ina mlio mtamu sana. It sound like a beast a real rugged suv!

Land cruiser 200 imepooza sana yani ipo kishoga sana esp. body design ingawa engine lake kubwa.
Kwenye tune department ndio kabisa wamefeli mno. It doesn't even sound like a v8.

They have just ruined the reputation of it i hate 200s! At least ya 2016 iliokuwa facelifted ndio kidogo inashawishi ila bado mlio "F"
 
muungurumo upo katika Range Rover utadhani kundi la nyuki linapita walikaa sana chini hiyo ni moja ya mimi kulipenda lile dude..

Range Rover yenye muscles ni ile classic ya mwaka 1988 labda.
Ikifuatiwa na ile vogue P38 na vogue ya 2003.
Zilizofatia zote hewa tu in terms of tune ya exhaust.
 
Aisee hakuna mlio mtamu kama wa landcruiser 80 then inafuatiwa ile ya land cruiser 100. Huwa unanifanya nitamani kumiliki ile gari kwa namna yeyote. Nakumbuka kipindi niko mdogo mzee alikuwa anapush lc 80 mpya ya ofisini kwao SUA. Ile mashine ilikuwa manual with diesel aisee acha tu. Tulikuwa tunapiga nayo tours as well kama kwenda kijiji n.k.
Alikuwa anaipiga chafu mbaya yani ina mzuka balaa kipindi akipangua gears wakati ana reverse na kuipa acceleration. That was when i started knowing and liking land cruisers. Aisee cruiser 80 ina mlio mtamu sana. It sound like a beast a real rugged suv!

Land cruiser 200 imepooza sana yani ipo kishoga sana esp. body design ingawa engine lake kubwa.
Kwenye tune department ndio kabisa wamefeli mno. It doesn't even sound like a v8.

They have just ruined the reputation of it i hate 200s! At least ya 2016 iliokuwa facelifted ndio kidogo inashawishi ila bado mlio "F"
Embu rudi tena ukasikilize mlio wa cruiser lc200 series diesel na hiyo lc80 series diesel. Ukisikiliza jibu baki nalo moyoni maana najua utaona noma kukubali mziki wa lc200.
 
Back
Top Bottom