Tufanye Mahesabu ya waliojiandikisha kwa Uchaguzi Mkuu: 37.7M - 35.3M = ?

Tufanye Mahesabu ya waliojiandikisha kwa Uchaguzi Mkuu: 37.7M - 35.3M = ?

OleWako

Member
Joined
Sep 7, 2021
Posts
25
Reaction score
73

Watu Milioni 2.6 Zaidi? Hebu Tuchambue Kwa Kina..​

Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) ilitangaza kwamba jumla ya wapiga kura 37,655,559 wamejiandikisha kwa uchaguzi mkuu ujao. Kwa mujibu wa Sensa ya 2022, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ilihesabu kuwa Watanzania 35,341,132 waliokuwa na umri wa zaidi ya miaka 14. Kwa mantiki hiyo, hao ni watu wenye sifa ya kupiga kura mwaka huu.

Hii inaacha pengo la watu 2,314,427.​

Wametokea wapi hawa watu?

Tujaribu kuweka muktadha kwa makadirio:
Ninachofanya hapa ni kutumia makadirio ya takwimu (si rasmi wala kisayansi) ili kujaribu kuchakata pengo hili la zaidi ya watu milioni 2.3. Lengo si kusema haya ndiyo majibu sahihi, bali ni kusaidia kuweka picha kamili ya kile kinachojitokeza.

Je, Sensa ya 2022 Ilikosea au vipi?
Watu wa NBS wanasema walifikia asilimia 99.99 ya kaya zote Tanzania (UNFPA).
Kwa kiwango hicho cha mafanikio, kaya zilizokosa kuhesabiwa ni takriban 93,627.

Sasa tukikadiria ni wangapi kati ya hao walio na umri wa miaka 15 na kuendelea, tunapata watu wapatao 257,247.

Kwa hiyo makadirio ya kosa la juu kabisa kutoka sensa ni takriban watu 260,000.

Vipi Kuhusu Vifo?

Kiwango cha vifo mwaka 2023 kilikuwa 5.791 kwa kila watu 1,000 (World Bank). Tukikokotoa kwa kutumia kiwango hiki, watu takriban 700,000 ambao wangekuwa na umri wa kupiga kura mwaka huu wanaweza kuwa walifariki kati ya 2022 hadi Julai 2025.

Tukifanya Hesabu:
Tukipunguza waliokufa (~700,000) na error margin ya sensa (~260,000) tunabaki na takriban milioni 34.9 wenye sifa ya kupiga kura mwaka huu.

Lakini bado orodha ya wapiga kura ya INEC inaonyesha milioni 37.7.
Bado tunatafuta watu milioni 2.6.


Vipi wakuu, sensa ilikuwa bovu au wapishi wameshaanza kupika?
 
Sensa ya 2022 chini ya Anna Makinda haikufanyika kwa ufanisi. Watu na nyumba nyingi hazikufikiwa. Wafanya sensa hawakuambatana na viongozi wa nyumba kumi. Walikuwa pekee yao, hakuna mwenyeji wa kuwaonesha wakazi wa maeneo husika. Walikuwa wakikuta nyumba zimefungwa, wenye nyumba wameenda kutafuta riziki, nyumba na wakazi wake hawakuhesabiwa. Hakukuwa na jitihada za kurudi tena au kuwapata wakazi hao.

Watu walijitokeza wengi kwenye daftari la mpiga kura siyo kwa lengo la kupiga kura bali kwa lengo la kupata kadi ya mpiga kura ambayo kwa sasa ina hadhi kupita hata ile kadi ya NIDA kwa matumizi. Na kwa kuwa zoezi la kupata kadi ya mpiga kura lilichukuwa siku nyingi kwenye kila eneo (wiki mbili) ukilinganisha na siku moja ya zoezi la sensa, watu karibu wote wa umri wa miaka 18 na kuendelea waliweza kupata hizo kadi ambazo ni kadi mbadala ya zile za NIDA ambazo upatikanaji wake ni kizungumkuti.

Hivyo idadi hiyo ya kwenye daftari la mpiga kura ndiyo sahihi ila waliojiandikisha kwenye daftari hilio kwa nia hasa ya kupiga kura hawazidi nusu, hiyo nusu nyingine imejiandikisha kwa nia ya kupata kitambulisho cha kielectronic.
 
Back
Top Bottom