Pre GE2025 Tufanye Midahalo kuhusu itikadi za kisiasa nchini au mafanikio ya Rais Samia Awamu ya 6

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Wafuasi wa Rais

Senior Member
Joined
May 31, 2023
Posts
151
Reaction score
147
Mdahalo uwe live hapa hapa JF. Jukwaa la kisiasa la JF sasa liwe la midahalo ya kisiasa hapa nchini Tanzania.

Mada mojawapo kati ya hizi mbili, au zingine vile mtakavyoona:

1 - Itikadi za kisiasa ubaya na uzuri wake.

Sisi kama Mtandao wa Wafuasi Binafsi wa Rais yaani President Supporters Network (PSN) hatukubaliani na itikadi za kisiasa. Hazina tija kwenye ulimwengu wa siasa za kisasa. Zimepitwa na wakati.

Zinasababisha uhasama usio na tija na mgawanyiko kwenye jamii. Kwa maneno mengine husaidia kuondoa uzalendo wa kitaifa, umoja na pia hupovusha fikra.

Tunakubaliana na tunaamini kwamba Rais ndio kila kitu bila kujali chama chake cha siasa; yaani hakuna sababu ya kuwa na itikadi za kisiasa. Rais akishachaguliwa kila mmoja awe nyuma ya Rais kumsaidia kwa ajili ya Taifa letu wenyewe.

2 - Mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan, phD akiwa kama Rais wa Taifa letu.

Yapo mengi mazuri sana aliyofanikiwa. Kama Wafuasi Binafsi wa Rais tunakiri pia kuwa baadhi ya watendaji wake walimuangusha aidha kwa bahati mbaya ama kwa sababu hawana weledi wa kazi waliyopewa. Lakini mara kwa mara akiwabaini anawaondoa haraka sana.

Ila kwa ujumla wake, anafanya vizuri sana kiasi kwamba tuna nguvu kubwa mno ya kufanya midahalo na yeyote yule kwa sababu facts zipo na zinajieleza zenyewe.

Sasa, tunaomba midahalo ya mara kwa mara kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Unaweza kuwasiliana na Mratibu wa Wafuasi Binafsi wa Rais kwa ushirikiano zaidi.

Mleteni mpinzani yeyote yule anayepinga mafanikio ya Rais. Mleteni mwanasiasa yeyote yule anayeamini katika itikadi za kisiasa. Tutawaumbua.

Karibu pia tuwasiliane kwa njia ya private message (pm).

Mratibu Mkuu,
Mtandao wa Wafuasi Binafsi wa Rais (PSN),
Mobile: +255 (0) 675 777 162.
Email: presidentsntz@gmail.com
 
Hana mpinzani kabisa na ndie mwanamke mwenye kundi kubwa la machawa wakiume dunia nzima, yupo vizuri mno kwa kwel.
1722005490234.jpg
 
Umasikini umetamalaki huko vijijini nyie mbakuja na swagwa za kijinga jinga hapa
 
Ni kweli kabisa , picha mbaya inatengenezwa na hawa machawa.
Hapa kwetu kumsema mtukufu rais ni uhaini..ila deep moyoni siku akirudi H.E Magu au Mwal Julius nitawapigia, mambo hovyo kabisa ila uhuru tunao kwenye bendera.
 
Mimi nafikiri kumtukuna kiongozi sio busara ila kumkosoa ni sawa kabisa hauwezi kubalika na kila mtu.
 
Kumkosoa mtukufu ni kumtukana...kuna huyu aliyesifu bao la mkono pasi kujua bao la mkono halitii mimba! You no wat am seying
 
Kuna mjadala,miradi ya JPM ilitengeneza ajira na inapokamilika imetengeneza ajira na tumeona mfano kwenyw SGR ,stend na masoko.
Sasa Mh kuruhusu mifuko ya hifadhi kujenga Kenya jengo la ghorofa mimi naona haipo sawa,inapeleka ajira kule.
pili dunia inatutegemea kwa makaa ya mawe sisi tunahangaika na wauza mkaa na wakata misitu,ni vyema makaa ya mawe tueleweshwe na sisi watz tuanze kutumia na tutunze miti yetu.
ukipita na treni unaona imebaki vimiembe na vimiti vidogo dogo,baada ya miaka 20 hatutokuwa na miti.Tueleweshe jinsi ya kutumia hii nishati tuokoe nchi.
Kwa taarifa tu,Ukrane wamegomea mafuta na gesi ya Russia na wanaagiza makaa ya mawe yetu kwa kupitia Kenya.Kenya ndio anasomeka kama nchi inayo export kiasi kikubwa kwenda Ukrane,sisi hapa dar hatujui kutumia.
 
Mtaukubali ukweli au mnasaka kuwateka watu tu, kwenda kuwangoa meno na plaizi.
 
Back
Top Bottom