SoC04 Tufe njaa kwa kulinda misitu? mkulima na kiongozi katika hili Nani asikilizwe?

SoC04 Tufe njaa kwa kulinda misitu? mkulima na kiongozi katika hili Nani asikilizwe?

Tanzania Tuitakayo competition threads

ZAKAYO MATHIAS

New Member
Joined
Nov 20, 2023
Posts
2
Reaction score
0
Tufe njaa kwa kulinda misitu? mkulima na kiongozi katika hili Nani asikilizwe?
Katika maisha ya sasa na siasa mwanasiasa anasimamia Sera za nchi mkulima anavunja Sera za nchi kumlisha mtunga sera za nchi nikiwa na maana kwamba mwanasiasa au kiongozi yeyote anasimamia Sera za nchi na kumnyima Uhuru mkulima kulima sehemu ambazo zimeachwa Kama hifadhi ya taifa. Ijulikane kuwa kabla ya watu kuongezeka sehemu nyingi zilikuwa Ni misitu minene ongezeko la watu limepunguza misitu minene hiyo kuonekana katika mazingira yetu na utumiaji wa vifaa vya kisasa na mbinu duni za uandaaji wa mashamba umepelekea mashamba mengi kukosa rutuba ya kutosha kustawisha mimea Jambo ambalo limepelekea wakulima kuvamia baadhi ya maeneo ya hifadhi kupata ardhi yenye rutuba ili kulisha nchi lakini wanaopambana kututafutia chakula katika nchi yetu wamekuwa wakitesha na kupewa adhabu Kali sana juu kulima au kutafuta chakula maeneo ya hifadhi je Nani tumsikilize unga ndani huku tunanjaa?? Au tutoe unga kidogo ili tushibe kwanza kulinde unga uliobaki au Nini kifanyike? Maana mkulima anapambana kutafuta chakula na mwanasiasa au kiongozi anasimamia sheria za nchi je? Tusikilize sheria za nchi tufe njaa au tushibe na kuwa na sehemu ndogo ya hifadhi? Kila upande uko sawa kusimamia sehemu yake lakini mkulima anasimamia sehemu yake Hana mtetezi nani asimame kusimamia wakulima na kuwawezesha kulima sehemu nyingine zenye rutuba na kuongeza chakula nchini? Kiongozi anaweza asiwe mkulima chakula anachokula kila siku kinatoka kwa Nani ? Tuseme kinatoka dukani Nini kisichotoka toka aridhini ukiachana nyota na mbalamwezi mawingu na vitu vingine vyote vilicho chini ya jua vinategemea aridhi kwa 98% Ni chakula gani kisichotoka aridhini? hapo ndipo utagungudua kuwa aridhi ndio kila kitu. Mkulima Tena kukata mkaa bila kibari Ni kosa kisheria, huyo mwanasheria anayetumia mkaa ameutoa wapi? Mkulima asilime wasiolima wale chakula wapi au tufe njaa? Jiulize pia upate wazo Nini kifanyike katika nchi yetu.
 
Upvote 4
Back
Top Bottom