Nimekuwa Tanzania kwa mwezi mmoja na ndiyo nimerudi kwenye kazi yangu hapa Texas, USA. Kuna kitu nimeona Tanzania ambacho nafikiri ni vizuri kubadilika
Lazima wananchi wajue jinsi na vitu vya kulalamikia. Tufundishe wananchi kulalamikia vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wa serikali na sio vile vilivyo nje ya uwezo. Hivi ni vitu ambavyo wananchi wanatakiwa kulalamika
1. Maji safi. Hakuna sababu ya maji bomba kuwa machafu. Hili liko ndani ya uwezo wetu sasa cha kushangaza wananchi wengi badala ya kulalamikia maji chafu wanawasaidia serikali kusema eti " ni bora sisi tuna maji kuna wengine hawana maji kabisa" Hii sio sababu ya msingi kwa sehemu zenye maji yanatakiwa kuwa safi na salama. uwezo tunao.
2. Uchafu wa mazingira. Hakuna sababu ya mji kuwa mchafu. Uwezo wa kusafisha upo, nia ya kusafisha ipo sasa ni kwanini kuna tabia ya kutupa tupa uchafu ovyo.
Wananchi wanalalama kwa miradi na vitu ambavyo ni vikubwa badala ya kuanza na vitu vya msingi kwanza.