Tufungue Ukurasa Mpya: Tujifunze siasa za Kenya. Leo Uhuru anampigia kampeni Odinga

Kenya wako kwenye right direction ...... wakati wao wanajitahidi kuungana kwa kila namna huku kwetu CCM anatafuta namna ya kutugawa ili waendelee kubaki madarakani.

Kitu ambacho CCM hawaamini ni kuwa wanaweza kushinda bila wizi wa kura .......!!
 
Tatizo siyo vyama vya siasa.
Shida kubwa ni watumishi wa uma na vyombo vya dola ambao kisheria hawatakiwi kuonesha upendeleo wowote wa kisiasa, lakini wanafanya wazi bila kujali katiba wala sheria.
Utaratibu wa kuwashughulikia hao wanaovunja katiba na sheria wakiwa ofisini ndiyo utatatua hiyo changamoto.
 
Una umri gani kijana? Hivi unazijua siasa za Kenya kweli? Yani wao ndio wamejifunza kwetu kwa taarifa yako nadhani miaka Ile wanauana ulikuwa bado unanyonya ndio maana umeweza kudhani siasa ya Kenya ni ya maana.

Hao hao wanaopigiana kampeni walisababisha kuuana kwa ukabila , uliza kitu inaitwa Mungiki bwana mdogo, uliza Rails alivyosababisha mauaji.

Raila hakuwa wa kuingia ikulu kabisa Ila ukabila unamsumbua mkalenjin kajikuta anatengwa bila sababu.

Hebu fuatilia siasa za Kenya vizuri it's always about ukabila mzee unapofika Kama hakuna nguvu ya pesa ujue umekwisha.

Sasa ndio tujifunze kwa hao wapuuzi??? Give me a break.
 
Mimi nazungumzia siasa za leo sio za mungiki au unataka tusubiri tupitie siasa za mungiki tuuane ndipo tujifunze.
 
Mimi nazungumzia siasa za leo sio za mungiki au unataka tusubiri tupitie siasa za mungiki tuuane ndipo tujifunze.
Sasa unadhani Kenyatta amemsapoti Raila kwa kupenda???? Huoni kwamba amemgeuka Ruto ambaye alimpa sana support walipounganisha vyama na kuform Jubilee?

Leo mtu aliyekuwa wapiga kura kwa makubaliano ya kwamba ukimaliza muda wako utampa support unakuja kumgeuka unaona ni sawa?

Raila na Uhuru have never been friends na hata mauaji yalipotokea causative ni Raila mwehu yule na huu umoja wao umekuja kiusaliti sana kwa Ruto.

Hatuna Cha kujifunza Kenya aisee. Na hata siasa za leo unazosema bado zimejaa ukabila mkubwa sana.
 
La kujifunza ni kuwa, In politics there are NO permanent friends and no permanent enemies.
 
La kujifunza ni kuwa, In politics there are NO permanent friends and no permanent enemies.
Labda hii ambapo hatuna haja ya kwenda mbali huko Kenya wakati hapa bongo muvi za wanasiasa wetu zinatosha kujifunza .

Angalia leo Lowassa na JK , angalia Kafulila, Moses Machali, Dr Mashinji, Nassari nk ukiongeza na Covid 19 ambavyo leo wameungana kuwa CCM supporters nk.

Yani Kenya huwa sielewi kwa nini tunaikweza nao wanatuona Kama watu wa mkoani jinsi tunavyoisujudu bila sababu.
 
 
Wao ndo walijifunza kwetu baada ya makamanda kumchagua Mzee Lowassa kuwa mgombea wao wa urais baada ya kumtukana kwa miaka kadhaa.
 
Siasa za Kenya ndizo bora kwa sasa Africa
 
Zimebaki siku chache tunzeni hii quotes mlete mrejesho.Ipo hivi duniani nzima ikiwemo serikali zote za duniani zipo chini ya nguvu za mamlaka ya watawala wa ulimwengu usioonekana, chochote kabla hakijafanyika ktk ulimwengu wa macho tayari kilishafanyika au afikiwa ktk ulimwengu usioonekana.
Uwe unataka utaki unakubali ukubali sisi sote tunaongozwa na nguvu zilizo nje ya uwezo wetu ambazo zipo ktk ulimwengu wa siri.
Kama serikali tu inawatambua wazee mfano wazee wa Dar ukadhani ni wazee as wazee sababu ya mvi au umri upo nyuma upo wrong,wale ni watu wazito Sana katk ulimwengu ulionekana wapo physical kuwakilisha wakuu wa ulimwengu usioonekana.
Ni SAwa na vatican, vatican si kama vatican ni zaidi ya vatican,thus wakuu wote wa duniani bila kujali dini ni lazima wasalute kwa Pope. Raila Odinga alimshinda UHURU uchaguzi uliopita akawa ajakubaliana masharti ya wakuu wa dunia thus akachezewa mchezo akapewa UHURU, Then anaitwa akaitwa akayakubali masharti thus anachukua this time hata Kenyatta analijua hili ndo maana kaamua kuwa upande wa Raila.
Kwann kambi ya Raila itashinda.
1.Wakenya wamechoka kutawaliwa na kabila/ ukanda mmoja miaka yote, wanataka kubadilisha ladha.
2.Kambi ya Odinga ni strong Ina wagombea smart na wameshauzika miaka mingi sana yaani Odinga na Martha Karua kuliko kambi ya Ruto pia ni wanasiasa mahiri na ni wachapa Kazi wakenya wanaona watavusha na sio ile kambi ya mafisadi.
3.Kambi ya ODIMA yaani Martha na Odinga Ina makampeni meneja smart na makini Sana kuliko kambi ya Ruto.
4.Ruto anajibomboa mwenyewe kwa kauli zake za chuki na visasi na ukosefu wa nidhamu.
5.Ruto ana visasi hana utulivu wa akili yaani sio matured and civilized enough kuongoza nchi,kiburi mjuaji mapepe yaani saikolojia yake haijabalance bado kulinganisha na Odinga,pia ni dictator hofu atawaletea machafuko wa Kenya.
6.Wakuu wa duniani hawawezi ruhusu hayawani aingie ikulu, Kenya ni muhimu Sana kama base ya kucontrol East, and Central Afrika ikiwemo Ghuba ya Aden. Utulivu wa Kenya ni muhimu Sana kwa interest zao.
7.Katika ulimwengu usioonekana wao chaguo lao ni Odinga kwa maana ni rahisi kumcontrol kinyota na sio Ruto yeye hayupo kabisa kwenye radar zao.

Wiki ijayo sio mbali tunzeni post hii.RAILA AMORO ODINGA ndie next president wa Kenya.Upige kura usipige kura tayari wakubwa wa Dunia walishapanga Odinga
 
UHURU anaijua siri ya Dunia Ruto anakimbiza upepo
 
Kiongozi wa CCM hata awe Rais mstaafu hawezi kuthubutu kumpigia kampeni mpinzani - hajipendi ? awaulize kina EL na mdogo wake Sumaye yaliyowakuta.

Mfumo wetu hauruhusu demokrasia kama hii kufanyika, mpaka tutakapokubali kubadilisha katiba vinginevyo tusahau kufikia level ya wakenya.

Wakenya wanajitambua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…