Tufute mfumo wa vyama vingi kibaki kimoja, Demokrasia siyo saizi yetu

Kwani unadhani wanapenda Uwepo wa vyama vingi !? Ijapokua vyama vyote vya upinzani ni matawi ya ccm kwaajili ya kuwaonyesha wazungu kuwa nchini Kuna Uwepo wa democracy..

Ccm hawataki Uwepo wa vyama vingi ila ndio hivyo watafanyaje wanaogopa kupigwa sanctions na wazungu

Punguza propaganda na unafiki
 
1.Tuna tumia muda mwingi kubishana kuhusu itikadi za vyama badala ya mustakabali wa nchi yetu. Mwaka mzima ni vyama, vyama ...upuuzi
2.Tunaumizana sisi kwa sisi kisa tu tumetofautiana vyama, kuna watu wako magerezani na wengine wamekufa au kujeruhiwa sababu ya vurugu za vyama.
3. Kila anayeingia madarakani anawaza namna ya kumdhibiti mpinzani wake badala ya kuleta maendeleo kwa nchi yake.
4. Kwa mfumo tulio nao ni rahisi kutengeneza watu wanaotumika kwa faida ya nchi nyingine ili kulinda maslahi ya pande mbili, maslahi ambayo hayana tija kwa wananchi
5. Tunatumia gharama kubwa kutoa ruzuku kwa vyama, hiyo pesa ihudumie wananchi.
6. Kwa nchi zinazoendelea, demokrasia ni mtego. Ni namna rahisi ya mataifa makubwa kuweza kucontrol mataifa madogo kulingana na maslahi yake. Usipoendana nao wanamsapoti mpinzani wako then you are out.
7. Hii imefanya kuwepo na mfumo mbovu, wa uchaguzi, mtu mzima kala suti yake safii, ila ni mwizi wa kura. Kama kuweza kuiba kura atashindwa kuwaibia wananchi? Mwizi ni mwizi tu. Tunajidharirisha.
8. Huu mfumo hauendi na tabia na hulka yetu, ambayo ni wivu, umimi, ubinafsi, uchoyo n.k kumbuka mpaka sasa kunafamilia zinalisishana, mtu tatu ziko kwenye top leadership, rejea kula za maoni
Tutengeneneze chama kimoja kitakacho jikita katika kuleta maendeleo,
Mwenyezi Mungu awape pumziko la milele ndugu zetu waliofariki katika vurugu za vyama, R.I.P Akwirina,Mawazo, Mwangosi na wengineo
Walioko magerezani wakawe huru.
Waliopotezwa wakapatikane
Majeruhi wakapate kupona
Amina.
Wewe unaonaje? Toa maoni yako

Punguza propaganda na unafiki. Akili zako zimefungwa kwa CCM ndio maana unaona vyama vingine havistahili kuwepo. Mbona Zambia, Botswana, Ghana, Zambia, Kenya, Gambia, Nigeria, wameweza?.
 
Wazo zuri sana,
ila Lissu atakuja kukufundisha kifungu cha sheria a, be, che, de, kutoka Wapi sijui.
"watoto wangu wako marekani mke wangu yuko ulaya Belgium, na mimi niko ukonga.😁"
Tuna demokrasia👊.

Punguza unafiki. Shida yako unahangaika na Lissu baadala ya issues. Mbona Samiah, Mwinyi na Kikwete familia zao ndio zimehodhi siasa za CCM ila inahangaika na mke wa Lissu na watoto ambao wanaishi nje kwa usalama wao.
 
Ni sawa kabisa,
Mkewe na wanae tuwaache wapate kilicho bora.
but uroho wa madaraka umemrudisha hapa.
Huyo toka miaka gani sijui kawa mbunge wa huko Singida amefanya nini?

Hivi unajua kilichompeleka Lissu ulaya?. Tatizo mnajisahulisha. Lissu kulalamika kuhusu usalama mkawa mnadhihaki nyie CCM , mwisho akapigwa risasi akapona. Kwa usalama akaenda kutibiwa Kenya, Kenya ndio wakamrefer ubelgiji. Hivyo akawa anapata therapy ya mguu wake huko ubelgiji. Ina maana asingepigwa risasi asingeenda Kenya then ubelgiji.

Shida wewe umejaa ubinafsi na uccm. Unaumia Sana Kwa Lissu kufanya siasa dhidi ya CCM ila haumii kwa familia tatu za Marais kuhodhi siasa za nchi. Narudia Tena punguza unafiki.
 
Punguza propaganda na unafiki. Akili zako zimefungwa kwa CCM ndio maana unaona vyama vingine havistahili kuwepo. Mbona Zambia, Botswana, Ghana, Zambia, Kenya, Gambia, Nigeria, wameweza?.
Wameweza kufanya nini?
Unaongelea kenya? Kenya ipi hii yenye maandamano mwaka mzima?
Toka nje ya hilo box
 
1.Tuna tumia muda mwingi kubishana kuhusu itikadi za vyama badala ya mustakabali wa nchi yetu. Mwaka mzima ni vyama, vyama ...upuuzi

2.Tunaumizana sisi kwa sisi kisa tu tumetofautiana vyama, kuna watu wako magerezani na wengine wamekufa au kujeruhiwa sababu ya vurugu za vyama.

3. Kila anayeingia madarakani anawaza namna ya kumdhibiti mpinzani wake badala ya kuleta maendeleo kwa nchi yake.

4. Kwa mfumo tulio nao ni rahisi kutengeneza watu wanaotumika kwa faida ya nchi nyingine ili kulinda maslahi ya pande mbili, maslahi ambayo hayana tija kwa wananchi

5. Tunatumia gharama kubwa kutoa ruzuku kwa vyama, hiyo pesa ihudumie wananchi.

6. Kwa nchi zinazoendelea, demokrasia ni mtego. Ni namna rahisi ya mataifa makubwa kuweza kucontrol mataifa madogo kulingana na maslahi yake. Usipoendana nao wanamsapoti mpinzani wako then you are out.

7. Hii imefanya kuwepo na mfumo mbovu, wa uchaguzi, mtu mzima kala suti yake safii, ila ni mwizi wa kura. Kama kuweza kuiba kura atashindwa kuwaibia wananchi? Mwizi ni mwizi tu. Tunajidharirisha.

8. Huu mfumo hauendi na tabia na hulka yetu, ambayo ni wivu, umimi, ubinafsi, uchoyo n.k kumbuka mpaka sasa kunafamilia zinalisishana, mtu tatu ziko kwenye top leadership, rejea kula za maoni
Tutengeneneze chama kimoja kitakacho jikita katika kuleta maendeleo,

Mwenyezi Mungu awape pumziko la milele ndugu zetu waliofariki katika vurugu za vyama, R.I.P Akwirina,Mawazo, Mwangosi na wengineo
Walioko magerezani wakawe huru.
Waliopotezwa wakapatikane
Majeruhi wakapate kupona
Amina.
Wewe unaonaje? Toa maoni yako
Hujaweka faida na hasara za mfumo huo unaosema nini kifanyike
 
Binafsi naona tuwe na chama kimoja,hivyo tu. Nikimaliza kibarua changu nitarudi kwenye faida na hasara za kila mfumo.Pia nimeweka uhuru kwa mtu yoyote kutafakari nini cha tofauti kinaweza kufanyika.
 
Kwani hayo mavyama kuna anayeyataka? Tatizo ni mikataba ya kimataifa ambayo ni lazima
 
Punguza propaganda na unafiki. Akili zako zimefungwa kwa CCM ndio maana unaona vyama vingine havistahili kuwepo. Mbona Zambia, Botswana, Ghana, Zambia, Kenya, Gambia, Nigeria, wameweza?.
Hizo nchi hazina tofauti na Tanzania katika ujinga
 
Shida ni kuwa na mifumo ya utawala rigid. Tunajua kabisa tunazidiana uwezo ila ukiambiwa mpishe mwenzio tunaleta ubishi na u babe. Mchawi wetu ni tabia zetu ambazo Bado hazijatahiriwa
 
Binafsi naona tuwe na chama kimoja,hivyo tu. Nikimaliza kibarua changu nitarudi kwenye faida na hasara za kila mfumo.Pia nimeweka uhuru kwa mtu yoyote kutafakari nini cha tofauti kinaweza kufanyika.
Binafsi mimi sikupungi ila naona mfumo sio shida shida ni waatu hiyo ndio root cause.

Unajua mwizi ni mwizi tuu hata uwe mfumo wa chama kimoja au viwili,
 
Demokrasia ya chama kimoja nayo inawezekana. Watu watatu au zaidi wa chama kimoja washindanie ubunge udiwani na urais.
 
Back
Top Bottom