Tuheshimiane

Hivi unapompa mtu namba yako ya simu what do you expect? Kwamba atai-save kwenye simu yake kama pambo?
 
aisee

mlipeana namba kwenye thread?
 
Mimi binafsi mtu akinipigia simu kwa mara ya kwanza baina ya saa tatu na nne usiku nitamuelewesha kistaarabu kuwa mimi sipokei simu zaidi ya saa tatu usiku kwa hiyo siku nyengine asinipigie wakati huo

Akinipigia kwa mara ya kwanza zaidi ya saa nne usiku nitamuuliza kama kuna dharura (neno la kwanza nitakalosema kwenye simu) kama hakuna dharura nitamwambia (sio kistaarabu sana) kuwa asifanye tena hivyo kwa kuwa sitapokea

Akipiga zaidi ya tano usiku nikipokea na kumuuliza kama akijibu si dharura, namrarua sawa sawa
 
Gee sasa huyu bidada sijui anaona aibu au anaogopa kumwambia jamaa....
 
Kule kwetu tunasema "anayapenda na kuyaendekeza" :]
Inawezekana kabisa sababu ukimpa mtu namba yako ya simu you'll have to expect chochote sasa asipomwambia huyo mtu msimamo wake ndio hapo tuna-conclude hapo kwenye blue
 
kwa mtaji huu ur msg haijawa derivered kwake, ila msikilizie uwezi jua yawezekana yuko serious na izo calls zake na ikawa ndo ulopangiwa na mola awe jamaa yako wa karibu aswa apo roho yako itakapo mdondokea pia

kumbuka kwamba nimesema hajui status yangu

huwe serious na kutoa namba ya simu, hasa kwa jamaa wenye wake, waweza kuta mwenzio amezamilia kukufanya nyumba ndogo, ooooooooh

nimeshakujibu hapo juu

dadaa mshikaji atakuwa yuko serious na wewe, natmai ndo chaguo lako lakini ndo haujashtukia tu ilo dili, ni bahati iyo usiiachie

jibu ni hilo hilo hapo juu
 

huyu mtu akipiga simu siku zote sipokei, hivi hawezi kuelewa kwamba sitaki kuongea nae?
 
kwa mtaji huu ur msg haijawa derivered kwake, ila msikilizie uwezi jua yawezekana yuko serious na izo calls zake na ikawa ndo ulopangiwa na mola awe jamaa yako wa karibu aswa apo roho yako itakapo mdondokea pia

jina lako limenikumbusha mengi mbali mkuu.
 
simu nyingi siku hizi zina system ya ku block incoming calls.Ifanyie set up simu yako kila akipiga hatakupata.
 
Pole sana bi dada, watu wengine ni wa ajabu sana anaweza kukupigia simu hata saa 8 ya usiku bila hata ya haya.Hizi balaa mimi zimekwishanikumba najua unachopsema.
 
Inawezekana kabisa sababu ukimpa mtu namba yako ya simu you'll have to expect chochote sasa asipomwambia huyo mtu msimamo wake ndio hapo tuna-conclude hapo kwenye blue

Bora ingekuwa mumepeana barabarani jitu lingine ni office mate wako au mumekutana katika masuala ya kikazi na cha ajabu usiku huo atakuuliza ishu za kiofisi
 
huyu mtu akipiga simu siku zote sipokei, hivi hawezi kuelewa kwamba sitaki kuongea nae?


1. Ulimpa namba ya nini au katika minajili ipi?
2. Kama unakereka, je ulishawahi kumwambia kuwa hupendi tabia yake ya kukupigia usiku?
3. Ulishawahi kumweleza status yako na madhara ya yeye kukupigia mida hiyo?
4. Kwa nini unapokea simu pindi anapopiga?
5. Unapoleta ujumbe humu unatarajia utamfikia mlengwa hali umesema hamjakutana humu?

Kama hayo yote yamefanyika na bado anaendelea "kukughasi":
6. Simu yako haina uwezo wa ku-block namba usiyopenda ikupigie...!!!?

Vinginevyo naungana na waungwana waliotangulia kuunga mkono hoja kuwa "wakataa, wataka".
 
Sijaelewa lengo la kuanzisha huu uzi ilhali muhusika sio memba humu jf, ataupataje huo ujumbe wako (Tuheshimiane) afu mwanaume alieoa akupigie simu sa 7 usiku? Is it? Huyo mkewe anakuwa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…