Tuheshimu Ikulu, Tuwaheshimu viongozi wote Wateule, ni Watanzania wenzetu, Tuwaheshima kama ambavyo Baba na Mama yako anastahili heshima

Tuheshimu Ikulu, Tuwaheshimu viongozi wote Wateule, ni Watanzania wenzetu, Tuwaheshima kama ambavyo Baba na Mama yako anastahili heshima

Ndio maaana kuna viongozi wanasimamishwa, kuna wanaopelekwa mahakamani, kifupi Tanzania kuna Utawala unafuata, Sheria, haki ,utu na demokrasia, ndio maana hata ukitaka kuandamana unapewa mpaka police wakulinde
Tusimamie kwenye heshima,, kuwaona wenzako pia ni binadamu wanaohitaji fair treatment kama wao, . Wanatukosea sana, wanaoheshimu watu wataheshimiwa ,ila wasioheshimu na wao hawataheshimiwa.
 
Ni bora, vyema, uungwana na uzalendo mkubwa kila Mtanzania akajifunza kuheshimu Mamlaka zilizopo kisheria na kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muunga wa Tanzania.

Ukikaa kwenye kisimbusi chako, unatukana, unadhalilisha viongozi, ipo siku utatamani maneno unayosema na maandishi unayoandika ingekuwa tofauti, Watanzania wengi tudanganywa na Wanaharakati wanaoeneza uongo, uzushi, kupandikiza chuki, kupandikiza fitina na chuki kwa Watanzania.

Tuwakatae Wanaharakati ambao kusema uongo ni jadi yao, wanafaidika kea kusema uongo, Tuipende Tanzania yetu, tutaishi na kustawi hapa.

Tuwe Wazalendo, Serikali ipo, Mamlaka zipo, Tanzania iko salama, Wakenya, Wamalawi na wengine wengi wana tamani kuwa Watanzania.

Yupo mtu kazi yake akiamka yeye kutukana viongozi na familia zao, kea sababu anahisi yeye kuwa nje ya Tanzania ni tiketi ya kusema uongo, kudhalilisha watu na kusingizia uongo mkubwa viongozi- amesahau kuna Mungu wa mbinguni

Yupo Mwanasiasa yeye baada ya kuona wenzake hawamweli anataka nini, kufeli kwa michango(upigaji- maana ana ukwasi wa kutosha, kama ni uongo aweke wazi account yake ya benk- miezi kadhaa nyuma kamhamishia mtu kutoka account yake Tsh 500,000,000- kwa Sababu ya Sheria za JF sitataja bank)sasa ameanza kusema uongo na kusingizia vitu vya uongo,

Yupo mwingine huko X kazi ya ni kutukana Serikali hii toka enzi za Mwalimu, wakati baba yake amekuwa Waziri na anapata benefit zote mpaka sasa, ila kila siku ni kueneza chuki, kuchonganisha, kugombanisha, kufitinisha, kusingizia na kusema uongo ili kuwachafua viongozi na Serikali ya awamu ya sita- ajue tu anaowatukana ni Wazazi, wana familia, wana ndugu, ni Viongozi kama ambavyo aliwahi kuwa baba yake anaye mheshimu.

Ni vyema tukajifunza kukosoa kwa hoja na sio kwa matusi, kuchonganisha, kusema uongo, kudhalilisha viongozi na Serikali ya awamu ya sita, kuchochea ubaguzi etc

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
mafisadi hawana sehemu ya kuheshimiwa
 
Katiba yenyewe waliyoitunga hawatuheshimu alafu tunamheshimuje mtu anayetumia pesa nyiiingi kutuhudumia ujinga?
Kukiwa na viongozi wanaotumia mabilioni yapesa zetu kutuhudumia ujinga ujinga tutamheshimu vipi wakati yeye hatuheshimu.
Wewe mwalimu achukuwe kwako milioni kumi kwa mwezi alafu mwanao mdoogo alishwe kande mbichi,ashindishwe njaa,asomee chini yamti,apewe makazi yausafi shule,afundishwe ujinga nk. utamheshimu huyo mwalimu?
Akitokea mpumbafu anakwambia mweshimu kwakuwa huyo ni mwalimu utaacha kumtukana huyo mpuuzi?
 
sijasoma ila ukiwa chini na ukawa kiongozi mwizi hovyo unakula shaba
 
Back
Top Bottom