Tuheshimu mila za watu

Tuheshimu mila za watu

Kama inatumia sharia, iweje serekali ya Zanzibar Leo itoke kuonyesha unyanyasaji sio sahihi?
Hiyo barua ni ya kuzuga tu, serikali ndiyo inayokamata wanaokula mchana na ndio imewapiga faini kampuni ya utalii.

Ukiisoma vizuri hiyo barua haikemei chochote.
 
Kwa hiyo ni haki wahindi wanavyoua waislamu kule India
Kabla hujaanza kuwatetea look at the number of hindus killed by Muslims Invaders
1000252081.jpg
 
Inshort hiyo dini yenu mmeishiwa mbinu za ushawishi, ndio maana mnatumia mabavu kuhakikisha dini yenu inabaki na wafuasi. Dini ya kweli hufuatwa kwa nguvu yake ya ushawishi, ukishaona inatumika nguvu kubwa kulinda principle za dini hiyo hata kwa wasiohusika, ujue hamna dini humo Bali genge la ushetani.
Well said
"Truth is like a lion, you don't have to defend it, it will defend itself"
 
Mila zipo ni kawaida, lakini uwepo wa mila, desturi, na tamaduni zako, jitahidi zisiingilie uhuru wa wengine, kwasababu hata wale ambao mila zako zinaingilia uhuru wao, nao pia wana mila, desturi, na tamaduni zao.

Dawa ya hayo yote ni kuvumiliana tu, sio kuleteana ubabe kukamatana na kupelekana polisi. Zanzibar ni ya wote, wenye asili, rangi, imani tofauti, sio ya kikundi fulani cha imani moja peke yao.
Nenda india kachinje ngombe hazarini halafu useme india ya wtu wte uwone nn kitacho kutokea
Hii chuki zidi ya znz haina mana ila kuamua tu kuheshim imani za wgn na nyny imani znu zitahishimiwa, mkiheshim tamaduni za wgn na tamaduni znu zitahesimiwa bila ya shida, msilazimishe wtu ujinga ambao hauna mana bali kutumia akili tu.
 
Zanzibar ni ya Wazanzibari wa Tanganyika acheni kujitoa ufahamu
Tumeungana tukazaa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Jamhuri ambayo ni Secular ila Wananchi wake wana Dini mbalimbali na wengine hawana Dini kwa maana 'Organised Religion' wanaabudu Mizimu na wengine ndio hawana Dini kabisaa.

Ndio maana Mtu kutika Visiwani Pemba anaweza kuja Bara akajenga Msikiti na kuelekezea Spika Dirisha langu na mimi nikamvumilia.

Namimi nataka niende Visiwani nikaogelee nikichoka nitoe Bapa langu la Konyagi au Balimi ya Baridi nishishie na Samaki wa kubanika.
 
Waizrael wakiwachapa Hawa washenzi Kuna wakristo wanakuja mbio mbio kuwatetea.

Hawafai hata kidogo! Wanachuki ya ajabu sijawahi kuona, wema wanataka watendewe wao tu lkn sio wao kutenda wema.
 
Ukiona funga Yako inasumbuliwa na wanaokula! Ujue wewe ni mlafi na huna sifa ya kufunga' Umepatana na Mungu kwamba ufunge' unakutana na jaribu doogo la mtu anayekula' na wewe ukashindwa kuvumilia!! Wewe ni mpumbavu na haufungi kwa ajili ya Mungu' bali umefunga ili ujitwalie sifa tu machoni pako
Kila nchi ina silk na tamaduni zk
Si vzr ktu usicho kijua undani wk ukajibu husasan maswala ya imani mana utakachokisema hakifanan na ulaisia bora ukauliza tu tujifunze kuvumilian na kujua mipaka ya kiiman kwa wngne
 
Tumeungana tukazaa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Jamhuri ambayo ni Secular ila Wananchi wake wana Dini mbalimbali na wengine hawana Dini kwa maana Organised Religion wanaabudu Mizimu na wengine ndio hawana Dini kabisaa.

Ndio maana Mtu kutika Visiwani Pemba anaweza kuja Bara akajenga Msikiti na kuelekezea Spika Dirisha langu na mimi nikamvumilia.

Namimi nataka niende Visiwani nikaogelee nikichoka nitoe Bapa langu la Konyagi au Balimi ya Baridi nishishie na Samaki wa kubanika.
Ndio maana mmaishia kubaguliwa na kuchapwa mboko mkiwa kule Zanzibar kwa tabia zenu za ovyo 😂
 
Mila zipo ni kawaida, lakini uwepo wa mila, desturi, na tamaduni zako, jitahidi zisiingilie uhuru wa wengine, kwasababu hata wale ambao mila zako zinaingilia uhuru wao, nao pia wana mila, desturi, na tamaduni zao.

Dawa ya hayo yote ni kuvumiliana tu, sio kuleteana ubabe kukamatana na kupelekana polisi. Zanzibar ni ya wote, wenye asili, rangi, imani tofauti, sio ya kikundi fulani cha imani moja peke yao.
Kumbuka tu znz wana serikali yao wana katiba yao wana sheria zao wana haki ya kujiwekea sheria au utaratibu wowote wanaona wao kua unawafaa
 
Inshort hiyo dini yenu mmeishiwa mbinu za ushawishi, ndio maana mnatumia mabavu kuhakikisha dini yenu inabaki na wafuasi. Dini ya kweli hufuatwa kwa nguvu yake ya ushawishi, ukishaona inatumika nguvu kubwa kulinda principle za dini hiyo hata kwa wasiohusika, ujue hamna dini humo Bali genge la ushetani.
Wacha porojo hizo sheria zipo kabla wewe hujazaliwa tii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
 
Mashallah habibi bandiko zuri sana. Baadhi ya ndugu zetu Watanzania bara huwa wanatabia ya popote waingiapo hupenda kubadilisha tamaduni ya eneo hilo zifanane na kule kwao wanapotoka(Sio wote). Wanachojisahaulisha ni kuwa ukiingia kwa watu fata ya wenyeji wako ya kwako utayafanya ukiwa kwako.
Kukamatwa watu kula Mchana Zanzibar ~ Watanganyika wasio Waislamu wamezusha Mjadala.

Ni vyema tukafahamu ya kuwa MILA, DESTURI, SILKA na UTAMADUNI ni mfumo wa maisha kamili ya kila jamii. Zanzibar kwa karne nyingi imekuwa ikitajika na kusifika ikafikia kubandikwa jina Tolerance Country. Kwa miongo kadhaa iliyopita zimeanza kuja hizi nganu zenye sura ya udini kwa lengo lile lile kama unataka kumuua mbwa mpe jina baya. Hayo yamekuja kutoka kwenye kundi fulani la kisiasa na kudhani ni mtaji kwao kumbe ni kuizamisha Zanzibar.

Sina hakika kama katazo la kula HADHARI mchana wa RAMADHANI lipo kisheria au la. La muhimu, kuna watu wanadhani katazo la kula hadharani mchana wa mwenzi mtukufu wa ramadhani ni katazo makhsusi kwa Watanganyika na Wakiristo. Wasichotaka kukifahamu katazo linamlenga kila binaadamu wakiwemo Wazanzibari na Waislamu wenyewe.

Kwa faida ya anaetaka kufaidika mwanamke wa Kiisilamu hawezi kufunga mwezi mzima (29/30) kutokana na sababu za kimaumbile hivyo mwanamke huyu ndani ya nyumba yetu tumezaliwa, tumelelewa na kukua pamoja mimi huwa siijui ni lini yupo ndani ya siku zake (hedhi). Nakusudia kusema ndani ya myumba yetu wakati yeye anaudhuru wa kisheria anaruhusiwa kula siku hizo (baada ya ramadhani anakuja kuzilipa) basi pia huwa anakula kwa kujificha. Huwa hali mbele yetu tukimuona.

Kuna wagonjwa nao wanaruhusiwa kula kisheria (wakipona wanakuja kulipa na wasipopona wanatolewa fidia). Wakiwa ndani ya nyumba lakini mfumo wao wa kula unakuwa ni tofauti na miezi mengine yote.
Kuna watoto ambao hawajatimia umri wanaruhusiwa kula basi hawa watoto pia huwa hawali ovyo ovyo majiani wana utaratibu wameekewa wao wenyewe wanaifahamu na kuiheshimu ramadhani kupita kiasi.

Mfano ulio hai watoto wangu mimi binafsi wanakwenda skuli na chuoni huwa wanapewa fursa warudi myumbani kula kisha warudi tena skuli au chuoni kuendelea na vipindi, mwanangu mmoja anakwenda nyumbani kula na kurudi skuli mtoto mmoja haendi anaona aibu kuwa ataitwa KOBE (jina la utani kwa mtoto asiyefunga) jaribu kufikiria mtoto wa miaka 7 anaona aibu kugundulika kuwa hakufunga anahiyari abakie skuli asirudi nyumbani kula kwa kuchelea asijulikane kuwa ni kobe!

Tulio zaliwa na kukulia Zanzibar kwa miongo kadhaa tumewashuhudia wageni kutoka mabara ya mbali wakiuheshimu utamaduni huu. Ajabu iliyoje majirani zetu na ndugu zetu wa karibu tulitegemea wao ndio wawe sehemu kutoa elimu hii badala kuhoji kwani Zanzibar na Tanganyika ni nchi tofauti? Tanganyika kuna baadhi ya MILA na TAMADUNI hakuna Zanzibar. Kadhalika Zanzibar kuna baadhi MILA na TAMADUNI hazifanani kabisa na Tanganyika si ajabu.

Zanzibar wapo Wakiristo tumezaliwa nao na kucheza nao tumekuwa wote hakuna hata siku moja Mkiristo wa Zanzibar anaweza kufanya upuuzi wa kula hadharani mchana wa ramadhani.

Siungi mkono watu kujichukulia sheria mikononi lakini vile vile sikubaliani na watu ambao hawana tolerance ya kuheshimu utamaduni wa wengine na kudhani wao pekee wana haki ya kuingia kwenye nyumba ya mtu na kufanya anachoona yeye ni sawa kwake. Heshima ni kitu cha bure kwani mtu akichukuwa chakula chake na kuenda kula ndani kwake kuna tatizo gani? Karaha ya kula mchana wa mwezi mtukufu wa ramadhani watu wanadhani inawahusu Watanganyika na Wakiristo tu, haya yashawafika hata Wazanzibari na Waislamu. Kosa linalofanyika ni kule kujichukulia sheria mikononi na kupelekea kuumiza watu.

Sisi tulipo nchi za wamaharibi kuna mambo mengi tumezuiwa tusifanye na tunaheshimu hizo taratibu. Mfano sisi tuna msikiti lakini ni marufuku kuadhini kwa bomba (spiker) kwa hiyo tunaadhini kimya kimya na kusali kimya kimya tumepungukiwa nini kwenye imani yetu?

Assallam aleykum.
 
Ukiona funga Yako inasumbuliwa na wanaokula! Ujue wewe ni mlafi na huna sifa ya kufunga' Umepatana na Mungu kwamba ufunge' unakutana na jaribu doogo la mtu anayekula' na wewe ukashindwa kuvumilia!! Wewe ni mpumbavu na haufungi kwa ajili ya Mungu' bali umefunga ili ujitwalie sifa tu machoni pako
Mkuu ningekuwa na majina wa yale waliomchapa huyu mtu ninge watag hapa.. tatizo nikwambwa unajufanya mgumu mbele ya chai, ukiona mkate chali
 
Kukamatwa watu kula Mchana Zanzibar ~ Watanganyika wasio Waislamu wamezusha Mjadala.

Ni vyema tukafahamu ya kuwa MILA, DESTURI, SILKA na UTAMADUNI ni mfumo wa maisha kamili ya kila jamii. Zanzibar kwa karne nyingi imekuwa ikitajika na kusifika ikafikia kubandikwa jina Tolerance Country. Kwa miongo kadhaa iliyopita zimeanza kuja hizi nganu zenye sura ya udini kwa lengo lile lile kama unataka kumuua mbwa mpe jina baya. Hayo yamekuja kutoka kwenye kundi fulani la kisiasa na kudhani ni mtaji kwao kumbe ni kuizamisha Zanzibar.

Sina hakika kama katazo la kula HADHARI mchana wa RAMADHANI lipo kisheria au la. La muhimu, kuna watu wanadhani katazo la kula hadharani mchana wa mwenzi mtukufu wa ramadhani ni katazo makhsusi kwa Watanganyika na Wakiristo. Wasichotaka kukifahamu katazo linamlenga kila binaadamu wakiwemo Wazanzibari na Waislamu wenyewe.

Kwa faida ya anaetaka kufaidika mwanamke wa Kiisilamu hawezi kufunga mwezi mzima (29/30) kutokana na sababu za kimaumbile hivyo mwanamke huyu ndani ya nyumba yetu tumezaliwa, tumelelewa na kukua pamoja mimi huwa siijui ni lini yupo ndani ya siku zake (hedhi). Nakusudia kusema ndani ya myumba yetu wakati yeye anaudhuru wa kisheria anaruhusiwa kula siku hizo (baada ya ramadhani anakuja kuzilipa) basi pia huwa anakula kwa kujificha. Huwa hali mbele yetu tukimuona.

Kuna wagonjwa nao wanaruhusiwa kula kisheria (wakipona wanakuja kulipa na wasipopona wanatolewa fidia). Wakiwa ndani ya nyumba lakini mfumo wao wa kula unakuwa ni tofauti na miezi mengine yote.
Kuna watoto ambao hawajatimia umri wanaruhusiwa kula basi hawa watoto pia huwa hawali ovyo ovyo majiani wana utaratibu wameekewa wao wenyewe wanaifahamu na kuiheshimu ramadhani kupita kiasi.

Mfano ulio hai watoto wangu mimi binafsi wanakwenda skuli na chuoni huwa wanapewa fursa warudi myumbani kula kisha warudi tena skuli au chuoni kuendelea na vipindi, mwanangu mmoja anakwenda nyumbani kula na kurudi skuli mtoto mmoja haendi anaona aibu kuwa ataitwa KOBE (jina la utani kwa mtoto asiyefunga) jaribu kufikiria mtoto wa miaka 7 anaona aibu kugundulika kuwa hakufunga anahiyari abakie skuli asirudi nyumbani kula kwa kuchelea asijulikane kuwa ni kobe!

Tulio zaliwa na kukulia Zanzibar kwa miongo kadhaa tumewashuhudia wageni kutoka mabara ya mbali wakiuheshimu utamaduni huu. Ajabu iliyoje majirani zetu na ndugu zetu wa karibu tulitegemea wao ndio wawe sehemu kutoa elimu hii badala kuhoji kwani Zanzibar na Tanganyika ni nchi tofauti? Tanganyika kuna baadhi ya MILA na TAMADUNI hakuna Zanzibar. Kadhalika Zanzibar kuna baadhi MILA na TAMADUNI hazifanani kabisa na Tanganyika si ajabu.

Zanzibar wapo Wakiristo tumezaliwa nao na kucheza nao tumekuwa wote hakuna hata siku moja Mkiristo wa Zanzibar anaweza kufanya upuuzi wa kula hadharani mchana wa ramadhani.

Siungi mkono watu kujichukulia sheria mikononi lakini vile vile sikubaliani na watu ambao hawana tolerance ya kuheshimu utamaduni wa wengine na kudhani wao pekee wana haki ya kuingia kwenye nyumba ya mtu na kufanya anachoona yeye ni sawa kwake. Heshima ni kitu cha bure kwani mtu akichukuwa chakula chake na kuenda kula ndani kwake kuna tatizo gani? Karaha ya kula mchana wa mwezi mtukufu wa ramadhani watu wanadhani inawahusu Watanganyika na Wakiristo tu, haya yashawafika hata Wazanzibari na Waislamu. Kosa linalofanyika ni kule kujichukulia sheria mikononi na kupelekea kuumiza watu.

Sisi tulipo nchi za wamaharibi kuna mambo mengi tumezuiwa tusifanye na tunaheshimu hizo taratibu. Mfano sisi tuna msikiti lakini ni marufuku kuadhini kwa bomba (spiker) kwa hiyo tunaadhini kimya kimya na kusali kimya kimya tumepungukiwa nini kwenye imani yetu?

Assallam aleykum.
Mambo ya Mila na tamaduni ni mambo ya hiari kuelimishana,

Hilo Si jambo la kisheria,

Huyo polisi lazima afuate Sheria na PGO, akiulizwa unampiga mtu huyu Kwa kosa lipi kisheria, hawezi kuficha kwenye tamaduni.

By the way, hao wananchi wanaopiga wengine katikati ya mfungo ni magaidi, ndio wale walioingia Kanisa Katoliki na kuharibu Mali ya Kanisa Kisha wakasingizia ni wagonjwa wa akili, hao Si waislamu hao, Wala Hawajafunga.
 
Back
Top Bottom