Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,746
- 5,772
Tunaomba taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Pccb ifuatilie na kuchunguza juu ya tuhuma zilizotolewa dhidi ya mwenyekiti wa CHADEMA .
Maana hizi ni tuhuma nzito na hata pesa anazodaiwa kuzikwapua ni nyingi sana kiasi cha bil 8 sio pesa kidogo.
Mimi binafsi siamini kwamba Peter Lijualikali hana akili timamu kiasi kwamba asimame bungeni na kuanza kuongea uongo.
Kwa muda mrefu kumekuwa na tuhuma toka kwa wabunge wa CHADEMA kuwa wanachangishwa pesa ili waweze kukiendesha chama chao. Jambo hili lilishafika hata kwa spika na alishawasaidia maana walikuwa wanakatwa kwa mabavu.
Ibara ya 13 ya katiba ya JMT inasema wazi kabisa kwamba hakuna mtu ambae yupo juu ya sheria. Maana sheria ya nchi yetu haibagui. Kama mtu aliwachangisha wabunge wa CHADEMA na Bil nane hazijulikani zilipo basi hatua za kisheria zifuate mkondo.