Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Vipi, msajili wa vyama ameshakifuta CHADEMA kwakutumia katibafake?
Kwako Pascal Mayalla
Mkuu Bigirita , msajili wa vyama na yeye ni kilaza tuu kama wale vilaza wengine wa serikali, Bunge na Mahakama!, hadi hapa ninapoandika, wala hajui kuwa katiba ya Chadema ni feki kwasababu ofisi ya Msajili ina maofisa vilaza tuu kama vilaza wengine wote, hakuna hata mtu mmoja aliye note hiyo omission!.
Kama Dr. Slaa aliyekuwa KM, alikuwa hajui uwepo wa kipengele hicho,
What about hao mburumatata wa ofisi ya Msajili?!.
P
 
Nimeona hii habari huko Twitter. Inasema kuwa Mbowe alikuwa mwenyekiti wa CDM mwaka 2004. Wakati huo katiba ya chama ilikuwa imezungumza kuwa kutakuwa na ukomo wa miaka kumi kwa mwenyekiti.
Mkuu Wakili wa shetani , haya maswali yako akina sisi tuliwahi kuyauliza, ni kweli Mbowe alipoingia kuwa Mwenyekiti wa Chadema, katiba ya Chadema ilikuwa na ukomo wa uongozi mwisho ni vipindi 2 vya miaka 5 jumla ni miaka 10.
Mwaka 2006 yalifanyika mabadiliko ya katiba. Lakini suala la ukomo wa uongozi halikuzungumzwa kwenye mkutano.
Ni kweli 2006 Chadema walifanya mabadiliko ya katiba na ni kweli kipengele hicho hakikujadiliwa.
Inasema kuwa katiba ilipoendwa kuchapwa, Mbowe akaondoa kipengele cha ukomo wa uongozi kinyemela. Hii ndiyo hadi leo mwaka wa 20 bado ni mwenyekiti.

Madai haya yanaukweli wowote?
Ni kweli katiba ilipoenda kuchapwa, hicho kipengele hakikuwepo, kiliyeyuka ila aliyekiyeyusha sio lazima awe ni Mbowe.

Hili jambo tuliisha lijadili humu kwa kirefu, Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa
Dr. Slaa alikuwa KM na alichangia Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

na JJ Mnyika akiwa Mkurugenzi wa Habari wa Chadema pia alichangia Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa
Nyuzi nyingine zinazohisiana na hili ni hizi Hatma ya Freeman Mbowe CHADEMA Elections 2015 - CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu! ila juzi kati hapa hili jambo Lissu kalifafanua vizuri kabisa Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA

P
 
Mkuu Pascal Mayalla nimesoma post yako kwa kina. Inamaana Dr Slaa na Mnyika waliongopa waziwazi kuwa kipengele cha ukomo hakikuwepo kwenye katiba ya 2004!!? Na kwamba mwaka 2006 waliunda katiba mpya, na katiba yenyewe inasema ni marekebisho ya katiba ya 2004?!!

Wanasiasa ni watu wa hovyo sana. Hawajui aibu.
 
No Dr. Slaa kwanza hakujua hata uwepo wa kipengele hicho!. Mnyika ndio akasema hakikujadiliwa. Hivyo hata hao hawakujua kiliondokaje!.
Aliyekiondoa sio Mbowe atakuwa ni Lissu kwa maelekezo ya mtu!.
Hivyo the final version ikaja kikiwa hakipo!, just vanished into thin air!.
Wanasiasa ni watu wa hovyo sana. Hawajui aibu.
Politics is a dirty game!.
P
 

Ukiitwa kwenye kamati ni juu yako tu.
 
Kwa maelezo yake Slaa amesema hakikuwepo. Na anakazia kwa kusema anayesema kipo alete katiba ya 1992, 2004 waangalie. Alikuwa anajua anachosema. Aliamua kudanganya waziwazi. Wote Slaa na Mnyika walijua wanachokifanya. Wote hawa si watu wa maana hata kidogo.
 
Kudanganya ni mtu anayejua ukweli, lakini Dr alikuwa hajui na hajui kuwa hajui hadi JJ.Mnyika alipoiweka sawa.

Take it from me Mnyika knew nothing!. Ni kama kwenye hili sakata la wabunge 19, Mnyika hakujua chochote!. Alipofuatilia ndio akaujua ukweli na kunyamaza.

P
 
Jiwe alijaribu Kupambana na CHADEMA akafa, kuwa Makini Paskali
 
​Ili kukata ngebe za baadhi ya wachangiaji wa mada hii ni vema kipengele hicho cha katiba kikawekwa hapa jamvini!
Hawana...!

Ishu hapa wala sio "kipengere cha ukomo wa uongozi" kunyofolewa kwenye katiba..

Ishu ni kwanini Freeman Mbowe awe mgombea wa Uenyekiti taifa na hatuna uwezo wa kumshinda? Tumbebeshe gari bovu tu kuwa alinyofoa kipengere cha ukomo wa uongozi....!!

Mimi nadhani ni kweli "katiba haina ukomo wa uongozi" lakini hakatazwi mtu kugombea nafasi yeyote ya uongozi ikiwemo nafasi ya Uenyekiti - Taifa..

Kama Kuna mtu anadhani ana uwezo wa kushindana na freeman Mbowe, agombee tu..!!
 
Mzee aliahidi kabisa kuwa na ataendelea kuwepo.
 
Hv Pascal Mayala ni kwamba ww ufahamu wako uko juuu sana kuliko msajiri aliyewekwa na ccm kuvi control vyama vya upinzani?? Yaani chadema iwe inatumia katiba fake Alafu msajiri asijue ??? Basi fanya jambo moja tu kumsaidia huyo msajiri unayemwita kilaza kwa kwenda mahakamani kuipinga katiba ya chadema kuwa ni fake...si huwa unajinasibu kuwa ww ni mwana sheria???? Acha uongo bhana, kama vp nenda makahamani ... tunakujua kuwa ww ni sukuma gang hivyo chadema unaiombeaga mabaya anytime
 
Zitto
 
JPM alijaribu Kupambana na CHADEMA akafa, kuwa Makini Paskali
Mkuu Bramo , kwanza asante kwa angalizo, mimi sipambani na Chadema, ninachofanya ni kuisaidia tuu Chadema ikae kwenye mstari kwa kuyaangazia makando kando yao yote.
P
 
Bwana P jitahidi kupambana na CHADEMA ukiwa ndani ya taasisi nyingine, usipambane kama wewe, kuna siku hii Chadema itakuumiza, kama si wewe ni kizazi chako.
Ni angalizo tu.
 
Mkuu Bramo , kwanza asante kwa angalizo, mimi sipambani na Chadema, ninachofanya ni kuisaidia tuu Chadema ikae kwenye mstari kwa kuyaangazia makando kando yao yote.
P
Mkuu Paskali, hata wakati Jiwe anapambana kuifuta CHADEMA, alikuwa kajiweka kwenye Kichaka cha kutengeneza uzalendo na kutokomeza wanaotumiwa na ma Beberu, narudia tena, Kuwa Makini
 
Mkuu Paskali, hata wakati Jiwe anapambana kuifuta CHADEMA, alikuwa kajiweka kwenye Kichaka cha kutengeneza uzalendo na kutokomeza wanaotumiwa na ma Beberu, narudia tena, Kuwa Makini
Asante sana hili nitalizingatia maana ni kweli kuna watu sio watu wa mchezo mchezo mfano ni huu Dr. Reginald Mengi vs Prof. Sospeter Muhongo: Nani ni Dalali? hivyo nitakuwa makini maana kama ni kweli ule Mbuyu umekwenda chini kwasababu ya Chadema, then who would dare stand up against?.
P
 

Na bado kuna watu wanasema Mbowe amekaa sana katika uenyekiti wakati CCM hata mwenyekiti Taifa hashindanishwi na yeyote!
Mkuu Yoda, karibu mitaa hii ushuhidie unatetea nini!.
Pamoja na yote, mwisho ni miaka 10!. Chadema katiba original iliweka ukomo wa miaka 10, kwenye marekebisho ya katiba ya Chadema ya mwaka 2006, hicho kipengele kiliyeyushwa na watu 2, huku aliyekuwa Katibu Mkuu, Dr. Wibroad Slaa hajui, wala John Myika hajui!. Angalia michango yao kwenye hoja hii Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa
P
 
Bwana P jitahidi kupambana na CHADEMA ukiwa ndani ya taasisi nyingine, usipambane kama wewe, kuna siku hii Chadema itakuumiza, kama si wewe ni kizazi chako.
Ni angalizo tu.
Mkuu Nyabutoro, hii post ndio nimeiona leo!, mimi sipambani na Chadema!, kila siku napita ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa, na sijawahi kuiulizia hiyo inventory!, unajua ni kwanini?.
P
 
Dr. Slaa amaanisha "literal translation" imeongeza udambwi kwenye toleo la kiswahili. Nani aliongeza huo udambwi na kwa dhumuni lipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…