Tuhuma inayoharibu future kwa maumivu makubwa. Je, Serikali ina la kujifunza?

Tuhuma inayoharibu future kwa maumivu makubwa. Je, Serikali ina la kujifunza?

Hii ni simulizi ya kutia huzuni mno ya mhanga wa kusingiziwa tuhuma aliyekaa gerezani mahabusu kwa miaka tisa.. Pengine katiba mpya itarekebisha haya mapungufu ya kisheria.

Kipindi cha pili na cha mwisho cha utawala wa hayati Benjamin Mkapa kulikuwa na matukio mengi sana ya uvamizi wa kwenye mabenki, taasisi za fedha na maduka mbalimbali kwa kutumia silaha.

Mojawapo ya matukio ya kukumbukwa sana ni lile la uvamizi wa ubungo gari aina ya landcruiser hard top lililokuwa limebeba pesa za bank ya NMB zikisafirishwa kwenda Morogoro nadhani.

Kwenye ule mtiti walikufa wengi wasio na hatia na walikamatwa wengi wasio na hatia pia.. Mmojawapo ndio huyu ndugu ambaye ndio kwanza harusi yake ilikuwa na mwaka mmoja huku akiwa amejaaliwa mtoto mmoja .. Wakati wa tukio mtoto alikuwa na umri wa miezi minne.

Askari kanzu walimwagwa mitaani kupeleleza wahusika wa tukio lile... Mtu mmoja asiyefahamika akamtaja huyu jamaa kuwa anamshuku kutokana na lifestyle yake.

Anasema jamaa ni mtu wa bata sana na hajulikani pesa anapata wapi na shughuli zake ni zipi.. Kama utani jamaa akadakwa yeye pamoja na mkewe na mtoto wao mchanga.. Siku wanamkamata ilikuwa tarehe 1.4 hivyo jamaa akadhani ni maskhara kutokana na tarehe husika.

Walikaa mahabusu kwa wiki nzima kisha mkewe na mtoto wakaachiwa huru akabaki jamaa.. Alijipa matumaini kuwa naye atatoka soon kwakuwa hakuwa na hatia yoyote.. Mwaka ukakata akiwa mahabusu.

Upelelezi ukaendelea na wahusika wote wakakamatwa. Lakini jamaa hakuachiwa. Huko nyumbani mambo yakazidi kuharibika.. Mkewe na mtoto wakafa kwenye ajali ya moto nyumbani kwao. Jamaa hakuweza kwenda kuzika wapendwa wake[emoji24][emoji24][emoji24]
Maumivu yakawa juu ya maumivu.

Mwaka wa tatu akiwa anasoma kitabu cha SAMEHE NA SAHAU akashukiwa na Neema ya Mungu na kuokoka..akajihisi ametua mzigo mzito sana.. Aliwasamehe wale wote waliomletea matatizo yote yale.

Mwaka wa nne watuhumiwa halisi wa ile kesi walihukumiwa wote vifungo tofauti tofauti lakini huyu ndugu bado akawa yuko ndani. Kukoleza maumivu kwenye kidonda akampoteza dadaake wa pekee ambaye ndio lilikuwa tegemeo lake la mwisho baada ya mkewe kufariki.

Mambo yalizidi kuwa magumu kule mahabusu gerezani kukiwa na matukio mengi yenye kuumiza sana. Ni baada ya miaka 9 kamili ndio aliachiwa huru baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.

Niki ni kisa cha kweli cha kuumiza na kufikirisha sana! Je tuna sheria ya kuwalinda watu wanaosingiziwa mambo mabaya? Je tuna sheria ya kuwaadhibu watu wanaosingizia wengine mambo mabaya?

Kuna watu hata sasa wako mahabusu kwa kesi za kusingiziwa.

Kuna watu hata sasa wako wanatumikia vifungo vifupi na virefu kwa kesi za kubambikiwa!

Kuna watu wamehukumiwa adhabu za vifo kwa tuhuma ambazo sio zao.. Wamesingiziwa. Wamebambikiwa!

Jeshi la Polisi na Maafisa Upelelezi kwa ujumla ni muda sasa wa kubadilika na kuanza kutumia njia za kisasa zaidi na teknolojia ya hali ya juu kwenye matukio kama haya. Hili kuondoa makando kando na haki kupatikana kati ya watuhumiwa na kuisaidia mahakama kufanya maamuzi sahihi kwenye kesi husika.

📌No One Is Above The Law.
 
Ni ile hujafa hujaumbika.

Maisha ni fumbo.

Ona Mbowe anavyotaabishwa sasa, Mungu ndiye anayejua. Swali je ni lini Mungu atapita huko magereza, wapo wengi wanateseka kifungoni ili mtu fulani afurahi tu. Je Mungu utanyamaza mpaka lini.

Tunao vijana wamepotea na mifupa ni heri hata wangefariki ili wazazi au familia wazike.

Mamndenyi unaongea mno, duuu
Mbowe ni gaidi kaz yake kuitisha maandamano alaf yeye anakimbia mwsho akamsababishia kifo aquelina huk yeye ametoka nduki ngoja akaekae ndan maana Hana ustaarabu
 
Jeshi la Polisi na Maafisa Upelelezi kwa ujumla ni muda sasa wa kubadilika na kuanza kutumia njia za kisasa zaidi na teknolojia ya hali ya juu kwenye matukio kama haya. Hili kuondoa makando kando na haki kupatikana kati ya watuhumiwa na kuisaidia mahakama kufanya maamuzi sahihi kwenye kesi husika.

[emoji419]No One Is Above The Law.
Katiba mpya inaweza kuwa suluhu ya haya yote
 
Back
Top Bottom