Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Fikiria tuhuma nzito kama hii inatolewa ndani ya Bunge na Mheshimiwa Mbunge halafu ukimya unatanda. Bunge kimya, vyombo vya usalama kimya, chama husika kimya na wananchi wanaowakilishwa na huyo Mbunge kimya! Je ni woga, ujinga au ukondoo.
Watanzania hebu tutulie, tujitafakari na tujiulize kama kweli sisi ni binadamu kama binadamu wenzetu hapa duniani! Je huyo anayetoa vitisho hadi kwa Mbunge wa kuchaguliwa akiwakilisha maelfu ya wananchi, hiyo jeuri yake inatokana na nini?
Kwanini tuwe na Bunge kama chombo hicho kiko dhaifu kiasi hicho? Katika kipindi kifupi tumeshuhudia madaraka ya Bunge yakiporwa taratibu lakini Bunge kimya. Tumeshuhudia Bunge likiogopa kutumia mamlaka yake ya kuisimamia serikali na badala yake likitumika kama chombo cha propaganda cha serikali.
Tumeshuhudia jinsi chombo hicho cha kutunga sheria kilivyoshindwa kutekeleza majukumu yake hadi kufikia kushindwa kuwalinda na kuwatetea wabunge huku likiendeshwa kama tawi la chama tawala.
Kweli Watanzania wenzangu tumefikia hali ya Mbunge kumiminiwa risasi za kuweza kumuua tembo na Bunge lisiunde hata tume kuchunguza kulikoni? Hapana, si bure, kuna tatizo pahala na tatizo lenyewe ni kubwa zaidi ya tunavyofikiria, ni tatizo linalohitaji ufumbuzi wa haraka kama tunataka kubaki salama kama taifa.
Kama Mbunge kutoka chama tawala anatishwa kama hiyo video inavyoonesha akilalamika ndani ya Bunge na hakuna hatua inayochukuliwa wala taarifa kutolewa, basi huko mbele tunakoelekea kunatisha zaidi.