Na kama angeamua kuyasemea hayo kwenye stand ya mabasi pale Mbezi kituo kile kingefungwaWengine wamefika mbali na kuiomba serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya vyombo vya habari i.e redio, TV, magazeti, YouTube channels zilizosaidia kurusha matangazo hayo ikibidi vinyang'anywe leseni, vifungiwe au vionywe
Umetaka akakuambia hana?Hili ni swali zuri sana. Uthibitisho wa madai ya mwingira uko wapi?
Na kama angeamua kuyasemea hayo kwenye stand ya mabasi pale Mbezi kituo kile kingefungwa
Kama hukuathirika na utawala wa Magufuli, huwezi kuelewa maana na mantiki ya hoja hii...Huu ujinga wa kutaka nchi isimame eti kufanyike maridhiano na misamaha sijui msingiwake ni nini, naona ni mtego uchwara tu.
Mnataka kupata gia ya kuitangazia dunia kwamba kuna tatizo kubwa kiasigani linalo hitaji maridhiano!!!.
Kama huyo mwingira anaona hakutendea haki na anaushahidi kwa anayoyasema siaende mahakamani akadai hakiyake ilichombo husika kidhibitishe madaiyake!!.
Kulalamika lalamika bila stepu ni kuichokoza serikali tu iliakizinguliwa aanze kutia huruma, ama akimbie nchi alafu apate kiki na sababu za kukimbia wauminiwake.
Mimi naamini ni kweli tupu kwa sababu ya circumstantial evidence ya aina ya uongozi na utawala wake...!Kwa Tabia alokuwanazo Magufuli, kuna uwezekano mkubwa Mwingira anasema ukweli. Kama Tundu lissu alipigwa na mgambo wa wahuni then Magu ndo alikuwa kiongozi wa wahuni mwenyewe.
Halafu kukatokea nini...?Mwingira aliwafanyia watu unyama sana kabla 2015
MLINZI WA MTUME MWINGIRA WA EFATHA AUAWA...
Josephat Mwingira. Mlinzi wa shamba la mifugo la Shirika la Efatha Ministry linaloongozwa na Joseph Mwingira, ameuawa na wengine wawi...ziro99.blogspot.com
Wananchi wavamia shamba la Nabii Josephati Mwingira Break Throw Mapinga
Wananch wa Bagamoyo eneo la Mapinga Wamevamia Shamba la Nabii na Mtume Josephati Mwingira. Juzi Mwingira alikwenda huko akiwa na walinzi wa Kimasai walioambatana Na Mabounce na kuendesha operation ya kuwaondoa kwa nguvu wananchi hao na kuzua mapigano makali ambapo leo kuna kikao cha ulinzi na...www.jamiiforums.com
Walinzi Wa Nabii Mwingira Wakata Masikio Wananchi Rukwa Shamba la Milonje
Bi Nuru Togwa(30) alikamwatwa na walinzi wa Nabii Mwingira baada ya kupita karibu na Shamba hilo na kupelekwa katika kambi yao na kukatwa Masikio yote mawili na kunajisiwa. Bi Alesi Maarifa (77) naye alikamatwa na kuunguzwa na upanga wa moto sehemu za Siri na hadi leo matukio hayo...www.jamiiforums.com
Mwingira wa EFATHA awaita Viongozi ya Serikali ni washenzi
Haya anayasema saa hii wakati anatoa mahubiri yake hapa kanisani. Anadai ameonyeshwa serikali wamemtuma mtu aje hapa kanisani ku spy ndipo alipoanza wewe uliyetumwa ni mshenzi na mambo yako ni ya kishenzi sababu waliokutuma ni washenzi. Haya ngoja nirudi kupata mahubiri nitarudi tenawww.jamiiforums.com
Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani tusitishane na Sheria...Zilikuwepo sheria na watu walizitumia kwa kujilinda wao, lakini leo hawapo Duniani na Dunia inaendelea. Watuhumiwa wa masuala haya nao waje hadharani kujibu hoja moja baada ya nyingine. Atakaye shindwa na mjadala wa hoja hizo akae kimya.Kiongozi wa makanisa ya Efatha Ministries Tanzania Nabii, Mtume na Askofu Josephat Mwingira amezua taharuki na mjadala mkubwa ktk vyombo vya habari TV, redio na social media kwa sababu ya mahubiri yake ya Jana Jumapili kanisani kwake...
Baadhi ya watu na wengine viongozi wa serikali kabisa wamedai alichokiongea Askofu Mwingira ni UCHOCHEZI kwa wananchi ili watu waichukie serikali yao...!
Wengine wamefika mbali na kuiomba serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya vyombo vya habari i.e redio, TV, magazeti, YouTube channels zilizosaidia kurusha matangazo hayo ikibidi vinyang'anywe leseni, vifungiwe au vionywe...
Haieleweki specific ni kwa kigezo kipi hasa vyombo hivi vifungiwe kwa sababu Askofu Mwingira yupo na kasema hayo kwa uwazi na mchana kweupe mbele ya camera za TV huku dunia nzima ikisikia na kuona...
Hii maana yake ni kuwa, kama kuna mtu ikiwemo serikali yenyewe inahisi madai au tuhuma za Askofu huyu dhidi ya serikali ni za uongo, ni obviously kuwa wanapaswa kutumia njia sahihi za kisheria kumtaka mtu huyu athibitishe...
Na maana yake ni kuwa, kama huyu alisimama hadharani kusema haya, pia anaweza kusimama na kijitetea mwenyewe hadharani....
Maswali ni haya: Kwanza kama ni kweli serikali itafanya mini? Pili, ni kwanini mnataka waadhibiwe wasiohusika...?
Kwa maoni yangu, nadhani hoja iwe ni KWELI au SIYO KWELI yaliyosemwa na huyu askofu...?
Kwa ufupi sana ni kuwa, ameituhumu serikali ya awamu ya 5 chini ya aliyekuwa Rais Hayati John P. Magufuli kuwa;
1. Kwa kutumia ile "Task Force" chini ya vijana wake maarufu kama "wasiojulikana" ilifanya majaribio ya kumuua mara 3 lakini ikashindwa...
2. Ilifanikiwa kuua baadhi ya watu wake askofu wa karibu sana...
3. Ilikuwa inataka kumfungulia mashitaka mabaya yasiyo na dhamana kwa kuwatumia watu wake wa karibu sana...
4. Ilipora na kuharibu mali zake zenye thamani ya TZS 10bn...
5. Ilifunga biashara zake ikiwemo benki kwa sababu ambazo hazijulikani mpaka leo...
Kwa vipimo vyote, hizi ni tuhuma mbaya kwa serikali inayopaswa kuwa kinara wa kufuata na kusimamia sheria na katiba ili kulinda haki za raia wake. Hii ndiyo sababu kubwa ya taharuki hii...
Hii sasa inanileta kwenye hoja kuu ya mada yangu. Yaani umuhimu wa kuundwa kwa Tume ya Haki na Maridhiano ya Kitaifa (The National Rights & Reconcilition Commission) ili kila mwenye malalamiko ya kutendewa vibaya kwa namna yoyote na serikali ya Rais Mgufuli (marehemu) apeleke malalamiko yake huko na kisha hatua zichukuliwe kwa njia sahihi na za amani ikiwemo kusameheana na kusonga mbele wote kwa pamoja kama taifa...
Labda tutakuwa tumesahau tu. Lakini ukweli ni kwamba, wapo wengi wenye malalamiko na tuhuma kama za Askofu Mwingira....
Walianza kina Freeman Mbowe, Manji, Mo Dewji, Anthony Diallo, Tundu Lissu, Godbless Lema, Joseph Mbilinyi (Sugu), wafanyakazi wa umma, wafanyabiashara nk...
Ya akina Askofu Mwingira yana - hit kwa sbb ni mtu maarufu na ametumia chombo chake cha habari (Trenet TV kama sijakosea)...
Na ofcoz baadhi ya viongozi wametaharuki kwa sababu ya namna alivyosema, njia aliyotumia na namna lilivyosambaa, kupokelewa na kupata reaction ya kasi na kubwa kwa jamii...
Sasa Askofu Mwingira anataka kuumiza hata wasiohusika kwa kisingizio cha "UCHOCHEZI" kiasi cha serikali kuanza kufikiri kuvichukulia hatua vyombo vya habari vilivyoichukua habari hiyo, kuiandika, kuitangaza au kuandika kwenye magazeti...
Hii siyo sawa wala haki kwa sababu haitaondoa tatizo bali itaendelea kulifanya kuwa kubwa na complicated zaidi. Iko njia nzuri na salama kushughulika na malalamiko ya watu kama Askofu Mwingira ambao kiukweli wapo wengi maelfu...
Njia hiyo ni kukubali kuwa LIPO TATIZO LA CHUKI NA MGAWANYIKO KATIKA JAMII yetu lililosababishwa na serikali iliyoongozwa na Hayati John P. Magufuli...
Tukishakubali (kutubu na kukiri) kuwa tulikosea na tuna tatizo, kisha tukae chini na kufikiria njia njema ya kurekebisha ili twende mbele wote kwa pamoja kama nchi...
So far, by now, hatuwezi kuzuia watu kusema na kutoa madukuduku yao ya mayoni kuhusu serikali yao kwa namna yoyote na kwa njia zozote wanazoona wao zinafaa bila kuvunja sheria. Bishop Mwingira hajavunja sheria yoyote kusema makosa ya serikali ya Magufuli...
Jambo la muhimu ni kuwa, watu hao wahakikishe kuwa madai au malalamiko yao au tuhuma zao lazima ingalau ziwe na uthibitisho na siyo propaganda tu au chuki binafsi tu...
Haya yanaweza kufanyika vyema iwapo tu, sisi wote kama taifa tutakuwa na UTASHI na NIA safi ktk mioyo na nafsi zetu ya kutengeneza mahusiano yetu...
Kama UTASHI na NIA hii IPO, hakutakuwa na ugumu wa kuundwa kwa TUME YA HAKI NA MARIDHINO YA KITAIFA..
Mungu katika Kristo Yesu awabariki wote mtakaosoma haya. Amina...
Sema upande wako vipi?Wewe unamwamini Mwingira?
Unakurupuka tu kusema ni awamu ya tano, unajua hizo mali zake ziliharibiwa mwaka gani?
Mkiwa waongo muwe na kumbukumbu nzuri...Maana naona kila muovu anatamani uovu wake utumike kuisulubu awamu ya tano iliyowaweka hafharani waovu wengi....
Nakubaliqna na wewe...Nadhani tusitishane na Sheria...Zilikuwepo sheria na watu walizitumia kwa kujilinda wao, lakini leo hawapo Duniani na Dunia inaendelea. Watuhumiwa wa masuala haya nao waje hadharani kujibu hoja moja baada ya nyingine. Atakaye shindwa na mjadala wa hoja hizo akae kimya.
Kungekuwa na uovu kama huo mnao jisemesha wabunge na viongozi wenu wangeunga mkono juhudi??.Kama hukuathirika na utawala wa Magufuli, huwezi kuelewa maana na mantiki ya hoja hii...
Lakini kudhulumu haki na uhai wa watu ni kosa ambalo halikosi kuwa na hukumu ya adhabu kubwa sana kwa kiongozi yeyote mwenye mamlaka toka kwa Yehova Mungu mwenyewe....
Wenye akili hutubu (hukukiri au hukubali) makosa, wakatengeneza na kujenga mahusiano mapya...
Wasio na akili hushapaza shingo na mwisho z8kavunjika.
Kati ya Kassim majaliwa na Mwingira nani anatakiwa kuaminiwa ?Hili ni swali zuri sana. Uthibitisho wa madai ya mwingira uko wapi?
Wewe unamwamini Mwingira?
Anza wewe sema ulizulumiwa nini, pengine hapo ulipo unafuata mkumbotu hata hujui wanao lalamika malalamikoyao msingi wake ni nini,we unaunga telatu bilakujua unakokwenda mbaka ukitumbukia bondeni ndio akili inakukaa.Nakubaliqna na wewe...
Na hii ndiyo mantiki ya hoja yangu kuu ktk andiko langu...
Kwamba, suluhu hapa ni kukaa chini wote wanaolalamika/tuhumu na wanaolalamikiwa/tuhumiwa na kila mtu ajibu tuhuma zake na kisha kama ni kusameheana, tunasameheana...
Na kama kuna wa kuwajibika kwa mujibu wa sheria watawajibishwa na kama kuna wa kufidiwa, wafidiwe...
Huu ndiyo utaratibu wa ki Mungu kumaliza matatizo...
Kungekuwa na uovu kama huo mnao jisemesha wabunge na viongozi wenu wangeunga mkono juhudi??.
Mlivyo na akili fupi utasema walinunuliwa.
Ukiulizwa unaushahidi utakodoa mimacho tu.
Yani mtuakitoka chadema kwenda ccm amenunuliwa, yani mnaamini mtuhawezi kwenda chama kingine kwa maamuziyake binafsi bila kununiliwa.
Hebu nikuulize!.
Lowasa na sumaye walivyo hamia chadema kutoka ccm mliwanunua sh, ngapi????.
Hii tabia itaendelea kujitokeza ,watu kutoa shutuma dhidi ya serikali iliyopita .
Kwa ajili ya kujipatia umaarufu .
Ni siasa zisizokuwa na mantiki Kwa taifa..
Tunatakiwa tuwe na siasa za kusema kwel.
Na sio umalaya wa kisiasa
Hili ni swali zuri sana. Uthibitisho wa madai ya mwingira uko wapi?
Kwahiyo Lowasa alikuja na pesa akalipia hiyo nafasi ya uraisi ndio akaruhusiwa kugombea urais??.Lowassa alihamia CDM akalipa ili apewe nafasi ya kugombea urais maana aliikosa CCM. Sumaye alizira na akaona pa kujifichia ni CDM. Ila zaidi ya 90% ya walioenda kuunga juhudi walinunuliwa ama kutishwa, japo waliahidiwa nafasi hizo hizo iwapo watahamia CCM. Pale ndio tuliona chaguzi za kishenzi na kihayawani kupata kutokea hapa nchini. Ukweli huu hata mtumie nguvu kiasi gani hamuwezi kuuondoa.
Kwahiyo Lowasa alikuja na pesa akalipia hiyo nafasi ya uraisi ndio akaruhusiwa kugombea urais??.
Nawewe ndio aina ya wapigakelele humu mnaetaka kupewa nchi muogoze watu???
Ndio aina ya watukama wewe mnataka serikali iache kazizake isikilize maombi uchwara haya ya maridhiano yasiyo eleweka??.
Ngoja mwenyekiti wenu na miga aionehii comments yako.