Tuhuma za Askofu Josephat Mwingira zimehanikiza umuhimu wa kuundwa haraka kwa Tume ya Ukweli na Maridhiano ya Taifa

Tuhuma za Askofu Josephat Mwingira zimehanikiza umuhimu wa kuundwa haraka kwa Tume ya Ukweli na Maridhiano ya Taifa

Wengine wamefika mbali na kuiomba serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya vyombo vya habari i.e redio, TV, magazeti, YouTube channels zilizosaidia kurusha matangazo hayo ikibidi vinyang'anywe leseni, vifungiwe au vionywe
Na kama angeamua kuyasemea hayo kwenye stand ya mabasi pale Mbezi kituo kile kingefungwa
 
Hili ni swali zuri sana. Uthibitisho wa madai ya mwingira uko wapi?
Umetaka akakuambia hana?

Amesema mashamba yake na trekta zake ziliharibiwa, hilo linahitaji uthibitisho wa macho tu...

Kuna akina Freeman Mbowe nao mashamba yao na mali zao ziliharibiwa chini ya usimamizi wa kiongozi mteule wa Rais Magufuli (Mkuu wa wilaya - Hai - Kilimanjaro) mchana kweupe huku kesi ikiwa mahakamani....

Kuna uthibitisho gani unataka kama hata macho yenu hayaoni...??
 
Bado hawa hawajaibuka na kusema waliyotendewa
Mo Dewji
Askofu Kakobe
Roma Mkatoliki
Zakaria Tarime
Endeleza.......
 
Huu ujinga wa kutaka nchi isimame eti kufanyike maridhiano na misamaha sijui msingiwake ni nini, naona ni mtego uchwara tu.
Mnataka kupata gia ya kuitangazia dunia kwamba kuna tatizo kubwa kiasigani linalo hitaji maridhiano!!!.
Kama huyo mwingira anaona hakutendea haki na anaushahidi kwa anayoyasema siaende mahakamani akadai hakiyake ilichombo husika kidhibitishe madaiyake!!.
Kulalamika lalamika bila stepu ni kuichokoza serikali tu iliakizinguliwa aanze kutia huruma, ama akimbie nchi alafu apate kiki na sababu za kukimbia wauminiwake.
Kama hukuathirika na utawala wa Magufuli, huwezi kuelewa maana na mantiki ya hoja hii...

Lakini kudhulumu haki na uhai wa watu ni kosa ambalo halikosi kuwa na hukumu ya adhabu kubwa sana kwa kiongozi yeyote mwenye mamlaka toka kwa Yehova Mungu mwenyewe....

Wenye akili hutubu (hukukiri au hukubali) makosa, wakatengeneza na kujenga mahusiano mapya...

Wasio na akili hushapaza shingo na mwisho z8kavunjika...!
 
Kwa Tabia alokuwanazo Magufuli, kuna uwezekano mkubwa Mwingira anasema ukweli. Kama Tundu lissu alipigwa na mgambo wa wahuni then Magu ndo alikuwa kiongozi wa wahuni mwenyewe.
Mimi naamini ni kweli tupu kwa sababu ya circumstantial evidence ya aina ya uongozi na utawala wake...!
 
Mwingira aliwafanyia watu unyama sana kabla 2015

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu kukatokea nini...?

Kwa lugha nyingine ni kuwa kila ulichopost hapa kwa madai ya kutendwa na Mwingira, ni makosa ya jinai...

Kama ni kweli alifanya hivi, alishtakiwa? Na mwisho hukumu ilikuwaje..?

Kumbuka jinai hushughulikiwa na serikali...
 
Kiongozi wa makanisa ya Efatha Ministries Tanzania Nabii, Mtume na Askofu Josephat Mwingira amezua taharuki na mjadala mkubwa ktk vyombo vya habari TV, redio na social media kwa sababu ya mahubiri yake ya Jana Jumapili kanisani kwake...

Baadhi ya watu na wengine viongozi wa serikali kabisa wamedai alichokiongea Askofu Mwingira ni UCHOCHEZI kwa wananchi ili watu waichukie serikali yao...!

Wengine wamefika mbali na kuiomba serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya vyombo vya habari i.e redio, TV, magazeti, YouTube channels zilizosaidia kurusha matangazo hayo ikibidi vinyang'anywe leseni, vifungiwe au vionywe...

Haieleweki specific ni kwa kigezo kipi hasa vyombo hivi vifungiwe kwa sababu Askofu Mwingira yupo na kasema hayo kwa uwazi na mchana kweupe mbele ya camera za TV huku dunia nzima ikisikia na kuona...

Hii maana yake ni kuwa, kama kuna mtu ikiwemo serikali yenyewe inahisi madai au tuhuma za Askofu huyu dhidi ya serikali ni za uongo, ni obviously kuwa wanapaswa kutumia njia sahihi za kisheria kumtaka mtu huyu athibitishe...

Na maana yake ni kuwa, kama huyu alisimama hadharani kusema haya, pia anaweza kusimama na kijitetea mwenyewe hadharani....

Maswali ni haya: Kwanza kama ni kweli serikali itafanya mini? Pili, ni kwanini mnataka waadhibiwe wasiohusika...?

Kwa maoni yangu, nadhani hoja iwe ni KWELI au SIYO KWELI yaliyosemwa na huyu askofu...?

Kwa ufupi sana ni kuwa, ameituhumu serikali ya awamu ya 5 chini ya aliyekuwa Rais Hayati John P. Magufuli kuwa;

1. Kwa kutumia ile "Task Force" chini ya vijana wake maarufu kama "wasiojulikana" ilifanya majaribio ya kumuua mara 3 lakini ikashindwa...

2. Ilifanikiwa kuua baadhi ya watu wake askofu wa karibu sana...

3. Ilikuwa inataka kumfungulia mashitaka mabaya yasiyo na dhamana kwa kuwatumia watu wake wa karibu sana...

4. Ilipora na kuharibu mali zake zenye thamani ya TZS 10bn...

5. Ilifunga biashara zake ikiwemo benki kwa sababu ambazo hazijulikani mpaka leo...

Kwa vipimo vyote, hizi ni tuhuma mbaya kwa serikali inayopaswa kuwa kinara wa kufuata na kusimamia sheria na katiba ili kulinda haki za raia wake. Hii ndiyo sababu kubwa ya taharuki hii...

Hii sasa inanileta kwenye hoja kuu ya mada yangu. Yaani umuhimu wa kuundwa kwa Tume ya Haki na Maridhiano ya Kitaifa (The National Rights & Reconcilition Commission) ili kila mwenye malalamiko ya kutendewa vibaya kwa namna yoyote na serikali ya Rais Mgufuli (marehemu) apeleke malalamiko yake huko na kisha hatua zichukuliwe kwa njia sahihi na za amani ikiwemo kusameheana na kusonga mbele wote kwa pamoja kama taifa...

Labda tutakuwa tumesahau tu. Lakini ukweli ni kwamba, wapo wengi wenye malalamiko na tuhuma kama za Askofu Mwingira....

Walianza kina Freeman Mbowe, Manji, Mo Dewji, Anthony Diallo, Tundu Lissu, Godbless Lema, Joseph Mbilinyi (Sugu), wafanyakazi wa umma, wafanyabiashara nk...

Ya akina Askofu Mwingira yana - hit kwa sbb ni mtu maarufu na ametumia chombo chake cha habari (Trenet TV kama sijakosea)...

Na ofcoz baadhi ya viongozi wametaharuki kwa sababu ya namna alivyosema, njia aliyotumia na namna lilivyosambaa, kupokelewa na kupata reaction ya kasi na kubwa kwa jamii...

Sasa Askofu Mwingira anataka kuumiza hata wasiohusika kwa kisingizio cha "UCHOCHEZI" kiasi cha serikali kuanza kufikiri kuvichukulia hatua vyombo vya habari vilivyoichukua habari hiyo, kuiandika, kuitangaza au kuandika kwenye magazeti...

Hii siyo sawa wala haki kwa sababu haitaondoa tatizo bali itaendelea kulifanya kuwa kubwa na complicated zaidi. Iko njia nzuri na salama kushughulika na malalamiko ya watu kama Askofu Mwingira ambao kiukweli wapo wengi maelfu...

Njia hiyo ni kukubali kuwa LIPO TATIZO LA CHUKI NA MGAWANYIKO KATIKA JAMII yetu lililosababishwa na serikali iliyoongozwa na Hayati John P. Magufuli...

Tukishakubali (kutubu na kukiri) kuwa tulikosea na tuna tatizo, kisha tukae chini na kufikiria njia njema ya kurekebisha ili twende mbele wote kwa pamoja kama nchi...

So far, by now, hatuwezi kuzuia watu kusema na kutoa madukuduku yao ya mayoni kuhusu serikali yao kwa namna yoyote na kwa njia zozote wanazoona wao zinafaa bila kuvunja sheria. Bishop Mwingira hajavunja sheria yoyote kusema makosa ya serikali ya Magufuli...

Jambo la muhimu ni kuwa, watu hao wahakikishe kuwa madai au malalamiko yao au tuhuma zao lazima ingalau ziwe na uthibitisho na siyo propaganda tu au chuki binafsi tu...

Haya yanaweza kufanyika vyema iwapo tu, sisi wote kama taifa tutakuwa na UTASHI na NIA safi ktk mioyo na nafsi zetu ya kutengeneza mahusiano yetu...

Kama UTASHI na NIA hii IPO, hakutakuwa na ugumu wa kuundwa kwa TUME YA HAKI NA MARIDHINO YA KITAIFA..

Mungu katika Kristo Yesu awabariki wote mtakaosoma haya. Amina...
Nadhani tusitishane na Sheria...Zilikuwepo sheria na watu walizitumia kwa kujilinda wao, lakini leo hawapo Duniani na Dunia inaendelea. Watuhumiwa wa masuala haya nao waje hadharani kujibu hoja moja baada ya nyingine. Atakaye shindwa na mjadala wa hoja hizo akae kimya.
 
Unakurupuka tu kusema ni awamu ya tano, unajua hizo mali zake ziliharibiwa mwaka gani?

Mkiwa waongo muwe na kumbukumbu nzuri...Maana naona kila muovu anatamani uovu wake utumike kuisulubu awamu ya tano iliyowaweka hafharani waovu wengi....

Kumbe kwa usahihi wako wewe, hizo mali ziliharibiwa mwaka na awamu gani eti...?

Na unapojibu kumbuka, tangu Uhuru hadi sasa TANU/CCM ndiyo wenye awamu zote...

So whatever "awamu is", it doesn't make any difference kwa sababu CCM ni CCM tu na serikali ni ileile...
 
Nadhani tusitishane na Sheria...Zilikuwepo sheria na watu walizitumia kwa kujilinda wao, lakini leo hawapo Duniani na Dunia inaendelea. Watuhumiwa wa masuala haya nao waje hadharani kujibu hoja moja baada ya nyingine. Atakaye shindwa na mjadala wa hoja hizo akae kimya.
Nakubaliqna na wewe...

Na hii ndiyo mantiki ya hoja yangu kuu ktk andiko langu...

Kwamba, suluhu hapa ni kukaa chini wote wanaolalamika/tuhumu na wanaolalamikiwa/tuhumiwa na kila mtu ajibu tuhuma zake na kisha kama ni kusameheana, tunasameheana...

Na kama kuna wa kuwajibika kwa mujibu wa sheria watawajibishwa na kama kuna wa kufidiwa, wafidiwe...

Huu ndiyo utaratibu wa ki Mungu kumaliza matatizo...
 
Kama hukuathirika na utawala wa Magufuli, huwezi kuelewa maana na mantiki ya hoja hii...

Lakini kudhulumu haki na uhai wa watu ni kosa ambalo halikosi kuwa na hukumu ya adhabu kubwa sana kwa kiongozi yeyote mwenye mamlaka toka kwa Yehova Mungu mwenyewe....

Wenye akili hutubu (hukukiri au hukubali) makosa, wakatengeneza na kujenga mahusiano mapya...

Wasio na akili hushapaza shingo na mwisho z8kavunjika.
Kungekuwa na uovu kama huo mnao jisemesha wabunge na viongozi wenu wangeunga mkono juhudi??.

Mlivyo na akili fupi utasema walinunuliwa.
Ukiulizwa unaushahidi utakodoa mimacho tu.
Yani mtuakitoka chadema kwenda ccm amenunuliwa, yani mnaamini mtuhawezi kwenda chama kingine kwa maamuziyake binafsi bila kununiliwa.

Hebu nikuulize!.

Lowasa na sumaye walivyo hamia chadema kutoka ccm mliwanunua sh, ngapi????.
 
Nakubaliqna na wewe...

Na hii ndiyo mantiki ya hoja yangu kuu ktk andiko langu...

Kwamba, suluhu hapa ni kukaa chini wote wanaolalamika/tuhumu na wanaolalamikiwa/tuhumiwa na kila mtu ajibu tuhuma zake na kisha kama ni kusameheana, tunasameheana...

Na kama kuna wa kuwajibika kwa mujibu wa sheria watawajibishwa na kama kuna wa kufidiwa, wafidiwe...

Huu ndiyo utaratibu wa ki Mungu kumaliza matatizo...
Anza wewe sema ulizulumiwa nini, pengine hapo ulipo unafuata mkumbotu hata hujui wanao lalamika malalamikoyao msingi wake ni nini,we unaunga telatu bilakujua unakokwenda mbaka ukitumbukia bondeni ndio akili inakukaa.
 
Kungekuwa na uovu kama huo mnao jisemesha wabunge na viongozi wenu wangeunga mkono juhudi??.

Mlivyo na akili fupi utasema walinunuliwa.
Ukiulizwa unaushahidi utakodoa mimacho tu.
Yani mtuakitoka chadema kwenda ccm amenunuliwa, yani mnaamini mtuhawezi kwenda chama kingine kwa maamuziyake binafsi bila kununiliwa.

Hebu nikuulize!.

Lowasa na sumaye walivyo hamia chadema kutoka ccm mliwanunua sh, ngapi????.

Lowassa alihamia CDM akalipa ili apewe nafasi ya kugombea urais maana aliikosa CCM. Sumaye alizira na akaona pa kujifichia ni CDM. Ila zaidi ya 90% ya walioenda kuunga juhudi walinunuliwa ama kutishwa, japo waliahidiwa nafasi hizo hizo iwapo watahamia CCM. Pale ndio tuliona chaguzi za kishenzi na kihayawani kupata kutokea hapa nchini. Ukweli huu hata mtumie nguvu kiasi gani hamuwezi kuuondoa.
 
Hii tabia itaendelea kujitokeza ,watu kutoa shutuma dhidi ya serikali iliyopita .
Kwa ajili ya kujipatia umaarufu .
Ni siasa zisizokuwa na mantiki Kwa taifa..
Tunatakiwa tuwe na siasa za kusema kwel.
Na sio umalaya wa kisiasa

Kwa taarifa yako ikitokea tume huru kudhibitisha uovu uliofanywa na awamu ya tano, kila kitu kitawekwa peupe. Usidhani vitisho ndio vitazuia huo ukweli wa uovu uliofanywa na Magufuli. Mnaweza kutishia watu leo au kesho maana serikali hii imepatikana kwa uovu wa utawala wa Magufuli, lakini ukweli huo utakaa wazi tu taka msitake. Namna pekee ni kuunda tume ya maridhiano, na tufunge ukurasa wa uovu ule kisha tusonge mbele. Uzuri uovu ule tumeshuhudia kwa macho yetu na kuusikia.
 
Hili ni swali zuri sana. Uthibitisho wa madai ya mwingira uko wapi?

Hivi mnadhani uovu ule ilikuwa siri sana, ama kwakuwa watu waliingia hofu ya kusema ukweli kwa kuogopa kutekwa na kuuwawa, hivyo mnadhani hakuna udhibitisho?
 
Lowassa alihamia CDM akalipa ili apewe nafasi ya kugombea urais maana aliikosa CCM. Sumaye alizira na akaona pa kujifichia ni CDM. Ila zaidi ya 90% ya walioenda kuunga juhudi walinunuliwa ama kutishwa, japo waliahidiwa nafasi hizo hizo iwapo watahamia CCM. Pale ndio tuliona chaguzi za kishenzi na kihayawani kupata kutokea hapa nchini. Ukweli huu hata mtumie nguvu kiasi gani hamuwezi kuuondoa.
Kwahiyo Lowasa alikuja na pesa akalipia hiyo nafasi ya uraisi ndio akaruhusiwa kugombea urais??.
Nawewe ndio aina ya wapigakelele humu mnaetaka kupewa nchi muogoze watu???
Ndio aina ya watukama wewe mnataka serikali iache kazizake isikilize maombi uchwara haya ya maridhiano yasiyo eleweka??.
Ngoja mwenyekiti wenu na miga aionehii comments yako.
 
Naona unafikiri mimi ni wa kubahatisha, pitia nyuzi zangu zote kuhusu ujio wa Lowassa ndani ya CDM. Nilisema kabisa kuwa Lowassa alitoa pesa kwa viongozi wa CDM chini ya Mbowe, wakafanya maamuzi ya kipuuzi kabisa kumpa nafasi ya kugombea kupitia CDM, wakati hakuwa na imani, wala hatakuwa na imani au mapenzi na CDM. Na kama ni pesa viongozi wote hutoa kwa makundi ya wapambe wao ili kuwasadia kwenye propaganda na kampeni. Ukimtoa Nyerere, ni kiongozi gani aliwahi kuwa muadilifu, kiasi kwamba ushangae Lowassa kupewa nchi?

Inaonekana ukiongea kwa kupanick utafanikiwa kututoa kwenye hoja yetu ya maridhiano. Ukweli mchungu ni kuwa Magufuli alikuwa rais muovu, na hakustahili kukalia kiti cha urais, bali alipaswa kuishia kwenye uwaziri mkuu, kwani hakuwa na busara ya kiti cha urais. Kwahiyo usitake kuongea kwa jazba na kuchanganya changanya sijui Lowassa, sijui serekali iache kazi zake as if serikali ina watu special sana, kiasi kwamba hawana muda na kushughulikia ukweli wa uovu ule.

Kinachowafanya muuongee kwa jazba ni ukweli wa uovu wa Magufuli kuwekwa hadharani, hivyo muushughukie ili tupate maridhiano au muache hilo mtajua nyie, lakini hamuwezi kuzuia sisi kusema ukweli wa uovu ule.
 
Back
Top Bottom