Tuhuma za Askofu Josephat Mwingira zimehanikiza umuhimu wa kuundwa haraka kwa Tume ya Ukweli na Maridhiano ya Taifa

Tuhuma za Askofu Josephat Mwingira zimehanikiza umuhimu wa kuundwa haraka kwa Tume ya Ukweli na Maridhiano ya Taifa

Kiongozi wa makanisa ya Efatha Ministries Tanzania Nabii, Mtume na Askofu Josephat Mwingira amezua taharuki na mjadala mkubwa ktk vyombo vya habari TV, redio na social media kwa sababu ya mahubiri yake ya Jana Jumapili kanisani kwake...

Baadhi ya watu na wengine viongozi wa serikali kabisa wamedai alichokiongea Askofu Mwingira ni UCHOCHEZI kwa wananchi ili watu waichukie serikali yao...!

Wengine wamefika mbali na kuiomba serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya vyombo vya habari i.e redio, TV, magazeti, YouTube channels zilizosaidia kurusha matangazo hayo ikibidi vinyang'anywe leseni, vifungiwe au vionywe...

Haieleweki specific ni kwa kigezo kipi hasa vyombo hivi vifungiwe kwa sababu Askofu Mwingira yupo na kasema hayo kwa uwazi na mchana kweupe mbele ya camera za TV huku dunia nzima ikisikia na kuona...

Hii maana yake ni kuwa, kama kuna mtu ikiwemo serikali yenyewe inahisi madai au tuhuma za Askofu huyu dhidi ya serikali ni za uongo, ni obviously kuwa wanapaswa kutumia njia sahihi za kisheria kumtaka mtu huyu athibitishe...

Na maana yake ni kuwa, kama huyu alisimama hadharani kusema haya, pia anaweza kusimama na kijitetea mwenyewe hadharani....

Maswali ni haya: Kwanza kama ni kweli serikali itafanya mini? Pili, ni kwanini mnataka waadhibiwe wasiohusika...?

Kwa maoni yangu, nadhani hoja iwe ni KWELI au SIYO KWELI yaliyosemwa na huyu askofu...?

Kwa ufupi sana ni kuwa, ameituhumu serikali ya awamu ya 5 chini ya aliyekuwa Rais Hayati John P. Magufuli kuwa;

1. Kwa kutumia ile "Task Force" chini ya vijana wake maarufu kama "wasiojulikana" ilifanya majaribio ya kumuua mara 3 lakini ikashindwa...

2. Ilifanikiwa kuua baadhi ya watu wake askofu wa karibu sana...

3. Ilikuwa inataka kumfungulia mashitaka mabaya yasiyo na dhamana kwa kuwatumia watu wake wa karibu sana...

4. Ilipora na kuharibu mali zake zenye thamani ya TZS 10bn...

5. Ilifunga biashara zake ikiwemo benki kwa sababu ambazo hazijulikani mpaka leo...

Kwa vipimo vyote, hizi ni tuhuma mbaya kwa serikali inayopaswa kuwa kinara wa kufuata na kusimamia sheria na katiba ili kulinda haki za raia wake. Hii ndiyo sababu kubwa ya taharuki hii...

Hii sasa inanileta kwenye hoja kuu ya mada yangu. Yaani umuhimu wa kuundwa kwa Tume ya Haki na Maridhiano ya Kitaifa (The National Rights & Reconcilition Commission) ili kila mwenye malalamiko ya kutendewa vibaya kwa namna yoyote na serikali ya Rais Mgufuli (marehemu) apeleke malalamiko yake huko na kisha hatua zichukuliwe kwa njia sahihi na za amani ikiwemo kusameheana na kusonga mbele wote kwa pamoja kama taifa...

Labda tutakuwa tumesahau tu. Lakini ukweli ni kwamba, wapo wengi wenye malalamiko na tuhuma kama za Askofu Mwingira....

Walianza kina Freeman Mbowe, Manji, Mo Dewji, Anthony Diallo, Tundu Lissu, Godbless Lema, Joseph Mbilinyi (Sugu), wafanyakazi wa umma, wafanyabiashara nk...

Ya akina Askofu Mwingira yana - hit kwa sbb ni mtu maarufu na ametumia chombo chake cha habari (Trenet TV kama sijakosea)...

Na ofcoz baadhi ya viongozi wametaharuki kwa sababu ya namna alivyosema, njia aliyotumia na namna lilivyosambaa, kupokelewa na kupata reaction ya kasi na kubwa kwa jamii...

Sasa Askofu Mwingira anataka kuumiza hata wasiohusika kwa kisingizio cha "UCHOCHEZI" kiasi cha serikali kuanza kufikiri kuvichukulia hatua vyombo vya habari vilivyoichukua habari hiyo, kuiandika, kuitangaza au kuandika kwenye magazeti...

Hii siyo sawa wala haki kwa sababu haitaondoa tatizo bali itaendelea kulifanya kuwa kubwa na complicated zaidi. Iko njia nzuri na salama kushughulika na malalamiko ya watu kama Askofu Mwingira ambao kiukweli wapo wengi maelfu...

Njia hiyo ni kukubali kuwa LIPO TATIZO LA CHUKI NA MGAWANYIKO KATIKA JAMII yetu lililosababishwa na serikali iliyoongozwa na Hayati John P. Magufuli...

Tukishakubali (kutubu na kukiri) kuwa tulikosea na tuna tatizo, kisha tukae chini na kufikiria njia njema ya kurekebisha ili twende mbele wote kwa pamoja kama nchi...

So far, by now, hatuwezi kuzuia watu kusema na kutoa madukuduku yao ya mayoni kuhusu serikali yao kwa namna yoyote na kwa njia zozote wanazoona wao zinafaa bila kuvunja sheria. Bishop Mwingira hajavunja sheria yoyote kusema makosa ya serikali ya Magufuli...

Jambo la muhimu ni kuwa, watu hao wahakikishe kuwa madai au malalamiko yao au tuhuma zao lazima ingalau ziwe na uthibitisho na siyo propaganda tu au chuki binafsi tu...

Haya yanaweza kufanyika vyema iwapo tu, sisi wote kama taifa tutakuwa na UTASHI na NIA safi ktk mioyo na nafsi zetu ya kutengeneza mahusiano yetu...

Kama UTASHI na NIA hii IPO, hakutakuwa na ugumu wa kuundwa kwa TUME YA HAKI NA MARIDHINO YA KITAIFA..

Mungu katika Kristo Yesu awabariki wote mtakaosoma haya. Amina...
Unakurupuka tu kusema ni awamu ya tano, unajua hizo mali zake ziliharibiwa mwaka gani?

Mkiwa waongo muwe na kumbukumbu nzuri...Maana naona kila muovu anatamani uovu wake utumike kuisulubu awamu ya tano iliyowaweka hafharani waovu wengi....
 
Kama ulidhulumiwa nenda mahaka mani taja wahusika walio kudhulumu ama kukutisha weka ushahidi wako sheria ichukue mkondowake, sio kuombaomba tensions nchi nzimaisimame kwa sababu za maneno ya kusikia tumieni akili kidogo.
Were ndio utumie akili kama ingekuwa uongo hiyo tension ya Nchi nzima ingetoka wapi?
Halafu bila aibu unasema aende Mahakama,huku unajua fika Mahakama za Tanzania zimetawaliwa na siasa za CCM.
 
Hujui chochote kuhusu historia ya wapigania haki wewe. DARASA la saba.
Mbowe hana watu wakati chama chako kupitia chakubanga kilinunua kuanzia mwenyekiti wa kijiji hadi mbunge?
Kuna viongozi wangapi wa ccm na serikali waliopitia kwenye tangu la mbowe?
Unaweza ukataja waliotoka lumumba kuja kwa mbowe???
Mbowe hatafuti pesa za kushibisha tumbo lake kama wewe unayelipwa boku 7 na kuanza kutukana watu. Mbowe kwao ni matajiri toka babako hajamuoa mamake!
Soma historia ya Tanzania umjue babake mbowe!
Hana watu wakati hata akifanya mikutano ndani kwake mnaita policcm??
Nsije nikawa naongea na form four hapa
Yani huoni aibu kusema kwamba Mbowe anawafuasi walikuwa wanajiuza kwa chakubanga.?

Ndio mnataka kuwa mbadala wa ccm? My foot!
 
Unakurupuka tu kusema ni awamu ya tano, unajua hizo mali zake ziliharibiwa mwaka gani?

Mkiwa waongo muwe na kumbukumbu nzuri...Maana naona kila muovu anatamani uovu wake utumike kuisulubu awamu ya tano iliyowaweka hafharani waovu wengi....
Watu kama nyie ndio mnafanya hii Nchi haindelei,mnatetea mpaka mashudu.

Samia mwenyewe anajua utawala wa basi wake ulikuwa wa unyang'anyi,halafu wewe uliyopo matumbi unabisha kwa hiyo unabishana na maneno ya SAMIA au??
 
Watu kama nyie ndio mnafanya hii Nchi haindelei,mnatetea mpaka mashudu.

Samia mwenyewe anajua utawala wa basi wake ulikuwa wa unyang'anyi,halafu wewe uliyopo matumbi unabisha kwa hiyo unabishana na maneno ya SAMIA au??
Kwahiyo?
 

Walinzi Wa Nabii Mwingira Wakata Masikio Wananchi Rukwa Shamba la Milonje!!!!
 

Nabii Askofu Mwingira agoma Kupima DNA, ni katika kesi ya kuzaa na mke wa mtu
 

Wananchi wavamia shamba la Nabii Josephati Mwingira Break Throw Mapinga
 
Haa yote yametokea miaka ya 2011 mpaka 2013,halafu aje mtu hapa aseme Nabii fake anaonewa,mtumishi wa mungu unatembea na walinzi unaogopa kudhuriwa na nani kama uko clean huna makandokando ya kuzaa na wake za watu,kudhurumu mashamba ya watu
 
Watu kama nyie ndio mnafanya hii Nchi haindelei,mnatetea mpaka mashudu.

Samia mwenyewe anajua utawala wa basi wake ulikuwa wa unyang'anyi,halafu wewe uliyopo matumbi unabisha kwa hiyo unabishana na maneno ya SAMIA au??
Kwahiyo?
 
Magufuli alikuwa mwovu ila alijificha kwenye kivuli cha dini
Kama ni wateule wake walikuwa wanafanya maovu na yeye analikalia kimya maana yake yeye ndio kawatuma
 
Yani huoni aibu kusema kwamba Mbowe anawafuasi walikuwa wanajiuza kwa chakubanga.?

Ndio mnataka kuwa mbadala wa ccm?
Uwezo wako wa kuelewa masuala ni mdogo sana! Kama siyo mbowe na chadema huna polite unaloweza kujadili wewe.
Sana utatukana tu
 
Mwingira aliwafanyia watu unyama sana kabla 2015






Sent using Jamii Forums mobile app
Ilishindikana vipi kumfungulia mashtaka badala ya kutaka kumuua?
 
Wewe unamwamini Mwingira?
Siyo suala la kuamini au kutomwamini mtu...

Ukiniuliza swali hili Mimi, nami naweza kukuuliza pia; Kwanini wewe usimwamini Mwingira na kuamini waliorushiwa tuhuma ni wasafi...?

Tutane mezani, kila mtu aseme grievances zake ili waamuzi waamue namna ya kusuluhishana...

Huu ndiyo uungwana..
 
Hii tabia itaendelea kujitokeza ,watu kutoa shutuma dhidi ya serikali iliyopita .
Kwa ajili ya kujipatia umaarufu .
Ni siasa zisizokuwa na mantiki Kwa taifa..
Tunatakiwa tuwe na siasa za kusema kwel.
Na sio umalaya wa kisiasa

Wewe nawe unawaza mambo ya umaarufu ili iweje..?

Huyu Askofu Mwingira atafute umaarufu gani zaidi ya huo alionao.?

Kwa taarifa yako, huyu ni maarufu ktk Ufalme wa Mbinguni/Mungu na hapa duniani tayari...!!
 
Wewe unamwamini Mwingira?
Labda tuseme hatumuamini Mwingira Je Tundu Lissu aliyepigwa risasi hadharani Hiyo imekaaje?Na walipotezwa ambao mpaka Leo hatujui wako au la Hilo nalo limekaaje?
Jukumu la kulinda raia wa nchi yeyote ni la kiongozi wa nchi ambaye ni amiri jeshi Mkuu.Sasa ikitokea raia wamepotea,wameuwawa au kupigwa risasi ,raisi anatakiwa kubeba hizi lawana zote!
 
Mwingira alichofanya ni kusemea watu wengi....kuna wengine hawakupata bahati kunusurika kuuawa, waliuawa kabisa. Kama mbunge kama Tundu Lissu alipigwa mchana wa saa 7 hadharani, wangapi wasiojulikana waliuawa? Tutasikia mengi sana
Ni kweli kabisa na nimelifafanua hili in kwa kina ktk hoja kuu hapo juu...

Ni wengi mno ambao wanawakilishwa na sauti ya Bishop Mwingira...

Ndiyo maana kuna umuhimu wa kukaa chini, tukaridhiana na kusameheheana na wanaostahili kufidiwa wafidiwe kisha twende mbele kwa pamoja...
 
Back
Top Bottom