Cloudsmedia wamefungia baadhi ya wasanii kwenye vituo vyao ikiwemo Diamond. Awapigi kabisa nyimbo zao kwa sababu za maelewano ya kibiashara japo wao wanaita 'jeuri ' ya msanii.
Waziri amefungia nyimbo za baadhi wasanii kwa madai zimekosa maadili, japo hajaweka wazi maadili kwa tafsiri ipi.
Cloudsmedia wanakuja na shutuma nzito kwamba Waziri anaua muziki sababu anafungia nyimbo za wasanii. Wakati wanalalamika haya wao bado wamefungia wasanii wengi tu.
Waziri anaenda kutoa ufafanuzi wa kufungia nyimbo zikiwemo za Diamond kwenye radio iliyofungia nyimbo za Diamond lakini inamlaumu waziri Kwa kufanya walilofanya.
Waziri anaongeza ukali wa adhabu kwa Diamond akiwa kwenye radio yenye ugomvi na Diamond.
Mashabiki wa Diamond wanamshambulia waziri kuwa anahusika kwenye mpango wa kummaliza kisanii na kibiashara Diamond.
Wengine kufikia kusema anatafuta kiki kupitia kwa Diamond.
Nani aliyeelewa hii sarakasi vizuri?