DOKEZO Tuhuma za Mganga Mkuu Serengeti, asimamishwe na kuchunguzwa

DOKEZO Tuhuma za Mganga Mkuu Serengeti, asimamishwe na kuchunguzwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
kwa muda mrefu kumekuwa na tuhuma ambazo zinathibitika za mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya serengeti nashangaa mamlaka zake mkoa ,Tamisemi na wizara zikikaa kimya pasipo kutusaidia watumishi.

Ofisi imegeuka sehemu ya madili na kosa aonekane mtu anaenda kinyume ni anapewa uhamisho nashangaa nguvu hii anatoa wapi kwani ukipewa uhamisho hakuna sehemu utaenda usaidike.

Tumenyanyaswa sana na katibu wa afya ambaye alimuweka yeye huyu katibu ni muuguzi na wamekuwa wakitumia nguvu kubwa hata kuondoa wataaluma ambao ni makatibu ili wabaki wao.

Mwaka jana pasipo sababu yoyote watumishi kadhaa walihamishwa kwenda wilaya za rorya na bunda hawa ni wale ambao hawakuwa wakikubaliana nae kwenye mambo hasa ya upigaji, kwahiyo ikatumika nguvu ya RAS kwasababu ni rafiki yake wakahamishwa.

Hapa idara hii inachangamoto nyingi sana wao ni madili.

Tumeletewa mganga mkuu mpya akapewa 14days kujiandaa AJABU ndani ya siku hizo Dr Lusubilo amepangua uhamisho ametoa rushwa na yule mgeni hajaja tena.

Tunajiuliza kwanini abaki hapa na amepata uhamisho maana yake mtu huyu anawatu hadi tamisemi kama asemavyo na mkoani na amewashika ndiyo maana hata uhamisho huu ameupangua.

Srrengeti kuna mradi gani wake mpaka afanye juu chini kubaki,tunaomba mamlaka tuondoleeni hili tatizo DED na RAS tunawalilia sana ninyi ni chanzo kikubwa cha ukandamizaji huu kwani mnamkinga asiguswe.

HATUMTAKI TUNAOMBA UCHUNGUZI HURU TUHUMA ZA RUSHWA ZIMEJAA HAPA IDARA YA AFYA NI MADILI
 
Baada ya malalamiko ya mganga mkuu wilaya ya serengeti , Dmo wa serengeti Dr Lusubilo Adam alihamishwa kwenda Dodoma wilaya ya kongwa na Dr chacha alihamishwa kutoka Misungwi kuja serengeti akafika akariport DED madeni hakumpa ushirikiano akaenda Kwa RAS Mara naye hakumpa ushirikiano maana yake kuna coordinated communication baina ya DMO lusubilo na DED wake na RAS Mara

Wizara ikampanga Dr chacha akiyetoka Misungwi kwenda Geita vijijin

DMO wa Geita wizara ikampanga aende Serengeti DED serengeti kampokea Daktari aliyetoka Geita ila Dr. Lusubilo amegoma kukabidhi ofisi na wala Toka apewe uhamisho kwenda Kongwa hajawahi kwenda kuriport maana yake Dr Lusubilo Yuko Juu ya wizara Kwa nini anafanya anachotaka maana yake wizara iko mikononi mwake anafanya anachotaka?
Yeye anang'ang'ania kubaki ili kuendeleza madili yao?? Kama cheo ni kile kile ila mahali kwingine unawezaje kukataa kuhama? Inamaana ananufaika na hapa kwetu Serengeti?
Wizara na Tamisemi tuondoleeni huyu mtu mbona mnatuweka tukose imani kwenu
Kuna harufu ya rushwa kutoka Kwa lusubilo kwenda Kwa DED na RAS kama wao ndio hawataki ahame na hizo hela za kuwahonga anazitoa wapi kama sio fedha za Zahanati mpya zinazowekewa fedha na hazitoi huduma bado?
 
Back
Top Bottom