Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Vizuri sanaa..
Hoja zote za kuwatetea au na wewe ni msukuma mkuu..

Kiukweli wasukuma ni watu wakabila kila mahali wanapokuwa ..hata wawe wawili katika halaiki ya watu watafanya jambo kwa kuanza na ukabila bila kujali uwezo na vigezo vinavyohitajika....

ni watu waliojaliwa ubinafsi sana na ubishi wa kiwango chau juu sana ..hii inathibitika hata kwa mkuu wetu wa kaya kwa anavyofanya maaumuzi yake
 
Kwa hiyo wateule wote kwenye ngazi za juu walioteuliwa hakuna kabila lingine ambalo lilikuwa na sifa na uwezo isipokuwa ukanda wa huko kwake? Ameteua ndugu mpwa zake wawili kwenye wizara moja ndo hao walikuwa na sifa tuu? acheni kutetea upuuzi.
Kwenye nafasi za uteuzi hawakuangalia flani ni nani au kabila gani. kilichoangaliwa na kuzingatiwa ni sifa, ikiwemo taaluma na uzoefu wa kazi. Ni aibu pia kwa kumnyima mtu nafasi ambayo amekidhi vigezo kisa tu ana ndugu yake ni kiongozi. Mtu hachaguliwi au kutochaguliwa katika nafas flani sababu ya mtu flani .
 


Pamoja na yote uliyosema, huu utawala umebadhilisha kabisa dhana ya Wasukuma kutokuwa wakabila. Haijawahi kutokea.
 
Kwa hiyo wateule wote kwenye ngazi za juu walioteuliwa hakuna kabila lingine ambalo lilikuwa na sifa na uwezo isipokuwa ukanda wa huko kwake? Ameteua ndugu mpwa zake wawili kwenye wizara moja ndo hao walikuwa na sifa tuu? acheni kutetea upuuzi.
Makamu wa Rais - Zenje
Waziri Mkuu - Lindi
Spika - Dodoma
Naibu Spika - Mbeya
Mawaziri wandamizi ;
Lukuvi - Iringa
Mwakyembe - Mbeya
Simbachaweni - Dodoma
Makamba - Tanga
Ummy Mwalimu - Tanga
Maghembe - Kilimanjaro
Kairuki - Kilimanjaro
Mpango - Kigoma
Ndalichako - Kigoma
Mwigulu - Singida
Mbarawa - Zenji
Kabudi - ???
Nape - alikuwa Lindi
Muhongo - Mara
Mahiga - Iringa
Lwenge - Iringa
Mhagama - Ruvuma
Mwinyi - Zenji

Huu ukabila na ukanda upo wapi hapo, Lissu atavuna tu chuki anayopanda 2020
 

Kwani Kikatiba Kavunja Sheria ipi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wasukuma wangekua na tabia ya ukabila nchi ingechafuka ,lakini ujumbe wowote ule ni fundisho. KAMA KUNATABIA YA UPENDELEO MUHUSIKA MKUU, PAUL POGBA AACHE MARA MOJA.
 
Unashauri wamakonde waendelezwe kwenye sekta ya uchongaji vinyago na Wairaqw/wabarbaig waendelezwe kwenye riadha hata kama wanataaluma ya kutosha lakini wasukuma ambayo kimsingi nao pia ni wakulima wa majaruba ya mpunga nawafugaji wakubwa waendelee kuteuliwa katika nafasi zote nyeti serikalini.

Kwa nini wapewe upendeleo maalum namna hiyo? Kwanini nao wasiendelezwe kwenye Kilimo na ufugaji badala yake wakamate ofisi muhimu za umma? Nini kinawapa huo upendeleo maalum? Hii ni dalili ya ulevi wa ukabila hasa usukuma!!!
 
nimeishi na wasukuma kwa kipindi kirefu sana, tangu nasoma mwanzoni mwa miaka ya 2000 hadi sasa nikiwa kazini naendelea tu kuishi nao.....kusema haki, sijaona ukabila wao kwa kiasi cha kusemwa hivi na sitaki kuamini hilo sasa. kama kuna kitu kama hicho kimeanza kujionyesha kwa huyu mtu basi ni ushamba wake mwenyewe tu na ujinga.......lakini mimi naona kitu kitu tofauti kwa huyu jamaa, UDINI!! jamaa ni mdini sana kusema ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…