Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Unajua Paskal kuna kanda flani imeendesha siasa za ukanda na ukabila kwenye Nafasi za kazi kwa muda mrefu Sana, Sasa revolution ya serikali ya awamu ya Tano inaondoa hicho kitu, hivyo wanapata maumivu Sana.

Kwani mkuki kwa nguruwe kwa binadamu ni mchungu.
Sasa basi wawe wapole kidogo.

Sasa wameamua kumtumia Lissu kama kichaka cha kufikisha salam zao kwa Rais Magufuli. Pia Lissu akijua kabisa Magufuli ana Neutralise hiyo kitu ilio dumu kwa muda mrefu lakini anajitoa ufahamu ili aridhishe mabwana waliomtuma.

Lakini Paskal nakuhakikishia udhalimu huu hautashinda na kupenya popote ndani ya serikali hii.
Wananchi taratibu wanaanza kuelewa dhamira ovu ya Baadhi ya wanasiasa waovu waliojificha kwenye kichaka cha demokrasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukweli lazima usemwe wazi kuwa Rais anafanya teuzi kwa kigezo cha ukabila na ukanda!! Miradi mingi ya maendeleo sasa inapamba moto kanda ya ziwa!!!!! ni hatari kwa ustawi wa nchi na amani
 
Analysis yako ungeitoa kuanzia enzi za Nyerere mpaka sasa. Ungeonyesha tokea enzi za Nyerere wasukuma walikua wangapi katika nyadhifa mbalimbali kadharika kwa Mwingi, mkapa, JK na JPM. Ina maana wamezaliana hasa ktk kipindi hiki cha 2015 na kuendelea? Vipi kuutelekeza uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe na kuanzisha uwanja mpya wa kimataifa CHATO.
 
Unajua Paskal kuna kanda flani imeendesha siasa za ukanda na ukabila kwenye Nafasi za kazi kwa muda mrefu Sana, Sasa revolution ya serikali ya awamu ya Tano inaondoa hicho kitu, hivyo wanapata maumivu Sana.

Kwani mkuki kwa nguruwe kwa binadamu ni mchungu.
Sasa basi wawe wapole kidogo.

Sasa wameamua kumtumia Lissu kama kichaka cha kufikisha salam zao kwa Rais Magufuli. Pia Lissu akijua kabisa Magufuli ana Neutralise hiyo kitu ilio dumu kwa muda mrefu lakini anajitoa ufahamu ili aridhishe mabwana waliomtuma.

Lakini Paskal nakuhakikishia udhalimu huu hautashinda na kupenya popote ndani ya serikali hii.
Wananchi taratibu wanaanza kuelewa dhamira ovu ya Baadhi ya wanasiasa waovu waliojificha kwenye kichaka cha demokrasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tangu tupate uhuru hii nchi imetawaliwa na ccm, kama hilo tatizo lipo kweli lawama ni kwa ccm, na ufumbuzi hauwezi kuletwa na watu haohao walioleta tatizo, dawa ni kuiondowa ccm madarakani hiki chama ni mkosi kwa Taifa letu.
 
Wanabodi,
Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila mbaya!.

Sisi wanamitandao ya kijamii lazima tufanye a responsible social networking ikiwemo kulisaidia taifa lisiangamizwe na sentiments zozote za ubaguzi au kibaguzi ziwe ni za Ukanda, Ukabila au Udini.

Kwanza tukubaliane sote in principle kuwa siasa zozote za Ukanda, Ukabila na Udini ni tatizo na ni detrimental, ni ugonjwa mbaya Kabisa kwa taifa letu and infact ni sumu!, a very poisonous Vernon!.

Watu wanaizungumza sasa kwa vile imezungumzwa na Lissu, lakini tukubali tukatae, ukanda upo, ukabila upo na udini upo na ni tatizo.

Hatua ya kwanza ya kuondokana na ubaguzi huu, kwanza ni by acceptance kwa kulikubali tatizo na kuwa ni kweli lipo na sio by denial, kama siku zote tunavyofanya. Dawa ya tatizo ni kulikabili kwa kulichimba kiini chake hadi kwenye mizizi kisha kuling'oa.

Mimi naomba kukiri wazi kabisa kuwa ni miongoni mwa wana jf ambao tulibaini tangu siku nyingi kuwa taifa letu linanyemelewa na sumu za siasa za ukanda, udini na ukabila na nilisema wazi hapa.

Mwezi August Mwaka 2014, nilipotajiwa kwa mara ya kwanza, jina la mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015, kuna kitu kama nilikisikia na nikakisema hapa

Hivyo ni kweli kabisa kuna udini mzuri na udini mbaya, kuna ukanda mzuri na ukanda mbaya na pia kuna ukabila mzuri na ukabila mbaya, lets make good use ya ukanda mzuri, ukabila mzuri na udini mzuri kwa maendeleo ya taifa letu.

Mfano, kabila la Wamakonde ndio mabingwa wa kuchonga vinyago, wachongaji mabingwa kabisa ni Wamakonde walioko Tanzania, Wakenya, Waganda, Rwanda na Burudi, wanakuja kununua vinyago Tanzania na kuvi export, hivyo kama tunataka kumiliki soko la vinyago, tuwaendeleze Wamakonde, na sio kabila jingine lolote!.

Miaka ya 70s Tanzania ilisifika sana kwa kutoa wakimbiaji bora, wakimbiaji wazuri ni watu wa makabila ya wafugaji na wawindani wa milimani, hivyo kina Filbert Bayi, Suleiman Nyambui, Gidamish Shahanga, Juma Ikangaa, Zebedayo Bayo, Zakaria Barie, John Steven Akwaari, Restituta Joseph, Simon Naali etc, wote hawa ni watu wa kabila moja au jamii za wafugaji wa milimani, hivyo Tanzania tukitaka kujenga timu imara ya riadha, timu ya ushindi, lazima tuwaendeleze watu wa kabila hilo au jamii hizo.

Wakati wa Nyerere, watu wa makabila fulani walifanya vizuri kwenye maeneo fulani kuliko makabila mengine, mfano Jeshini na polisi ni watu wa Musoma/Mara.

Ukabila Mzuri Katika Uteuzi.
Kufuatia kabila la Wasukuma kuwa ndilo kabila kubwa kabisa nchini Tanzania, ndilo kabila lenye watu wengi zaidi, hivyo automatically, tukifuata principals of proportionality, Wasukuma ni lazima wawe wengi kila mahali, hii ni halali yao na sio upendeleo!.

Ukitokea wewe ni mteuzi, ukaletewa majina matatu wote wenye sifa sawa na mmoja wao ni Msukuma, jee utaogopa kumteua huyo Msukuma kwa sababu ya kuchelea utaonekana ni mkabila?, zikitokea nafasi, halafu kati ya walioomba wote, wenye sifa zaidi ni Wasukuma, then let it be, hata Wasukuma wakijazana sana, as long as ndio wenye sifa, then huu ni ukabila mzuri, hivyo natoa wito kwa JPM, endelea kuteua Wasukuma, wajaze kila mahali as long as ni watu wenye sifa na ni wachapa kazi, then wewe teua tuu, wanaosema waache waseme, watasema mchana msiku watalala.

Ukabila Mbaya Katika Uteuzi.
Ikitokea kuna nafasi za uteuzi, then ukaamua kwa makusudi kutafuta mtu wa kabila lako, ambaye hana sifa, lakini kwa vile ni kabila lako, unampa

Inaendelea....
TATIZO kubwa la Wasukuma lilikuwa ni kuwa WENGI walikuwa Watu wa MIFUGO sana na hawakujali mambo ya masomo.. WAZAZI walijali Ng'ombe kuliko elimu hiyo ikawafanya ku kubaki nyuma.
PAMOJA na hayo UTAWALA wa kati huo HAUKUWAPA nafasi SAWA KIELIMU kama ilivyokuwa kwa makabila mengine kwa sa babu ya HOFU zilizokuwa hazina misingi.

HOFU ikiyokuwepo ilikuwa ni kuwa waliwaogopwa kuwa ni Kabila kubwa na hivyo KUAMKA kwao kungeleta POLITICAL REALIGNMENT/ mabadiliko makubwa ya KISIASA Hofu ambayo haikuwa na MSINGI.

Kwanza Vyama vya Ushirika vilivyowaunganisha Wasukuma kama vile NYANZA CO Union AKAVIDHOOFISHA sana ili kuwa DISORIENT Wasukuma/Wasishikane.

Na wale WACHACHE waliosoma kama vile watoto wa MACHIEF/WATEMI na wengine wachache ndo walioweza kupata REASONABLE education na employments. SABABU ya WAKOLONI.

Hata hivyo nao WALIWEKEKEWA LIMITATION /KIWANGO ambacho WASINGEKIVUKA.
Ka UWAZIRI kidogo , Ka UBALOZI kidogo mkuu wa ka Tume kidogo nk.

Mzee kama Marehemu Meja jenerali Mayunga ambaye alikuwa SHUJAA wa kumwondoa Idd Amin wa Uganda katika VITA vya KAGERA alikuwa AMEFIKIA KIWANGO cha kuwa Mkuu wa MAJESHI.Nini kilimtokea?

Cha kushangaza ni kuwa alipokikaribia tu AKATEULIWA kuwa BALOZI.
Hilo lilimuumiza sana nad that was UNFAIR to him and more so to the Sukuma community.

Namalizia kwa kusema kwa SASA WENGI WAMESOMA na WANASOMA hamna namna ya kuwanyima NAFASI as long as ni mtu ANAYESTAHILI na ni qualified kushika wadhifa wowote.

Ili nao waliodharauliwa wajisikie ni Watanzania kama Wengine na si Bushmen.

Ninaposema hivyo siungi mkono UKABILA ila KILA mtu wa kabila lolote aliye qualified/ ALIYEHITIMU anahitaji kupewa HAKI SAWA bila kujali ANATOKA WAPI.
 
Pasco umeamka na akili za usingizini.
Yaani mtu anateua wapwa zake wawili kwenye wizara moja, tena vyeo vya juu kabisa tumnyamazie tu kisa eti wana sifa??
akina nani hao? wapo wizara moja na wapwa zake ?isije ikawa ni uchochezi, au tupe link
 
Wanabodi,
Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila mbaya!.

Sisi wanamitandao ya kijamii lazima tufanye a responsible social networking ikiwemo kulisaidia taifa lisiangamizwe na sentiments zozote za ubaguzi au kibaguzi ziwe ni za Ukanda, Ukabila au Udini.

Kwanza tukubaliane sote in principle kuwa siasa zozote za Ukanda, Ukabila na Udini ni tatizo na ni detrimental, ni ugonjwa mbaya Kabisa kwa taifa letu and infact ni sumu!, a very poisonous Vernon!.

Watu wanaizungumza sasa kwa vile imezungumzwa na Lissu, lakini tukubali tukatae, ukanda upo, ukabila upo na udini upo na ni tatizo.

Hatua ya kwanza ya kuondokana na ubaguzi huu, kwanza ni by acceptance kwa kulikubali tatizo na kuwa ni kweli lipo na sio by denial, kama siku zote tunavyofanya. Dawa ya tatizo ni kulikabili kwa kulichimba kiini chake hadi kwenye mizizi kisha kuling'oa.

Mimi naomba kukiri wazi kabisa kuwa ni miongoni mwa wana jf ambao tulibaini tangu siku nyingi kuwa taifa letu linanyemelewa na sumu za siasa za ukanda, udini na ukabila na nilisema wazi hapa.

Mwezi August Mwaka 2014, nilipotajiwa kwa mara ya kwanza, jina la mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015, kuna kitu kama nilikisikia na nikakisema hapa

Hivyo ni kweli kabisa kuna udini mzuri na udini mbaya, kuna ukanda mzuri na ukanda mbaya na pia kuna ukabila mzuri na ukabila mbaya, lets make good use ya ukanda mzuri, ukabila mzuri na udini mzuri kwa maendeleo ya taifa letu.

Mfano, kabila la Wamakonde ndio mabingwa wa kuchonga vinyago, wachongaji mabingwa kabisa ni Wamakonde walioko Tanzania, Wakenya, Waganda, Rwanda na Burudi, wanakuja kununua vinyago Tanzania na kuvi export, hivyo kama tunataka kumiliki soko la vinyago, tuwaendeleze Wamakonde, na sio kabila jingine lolote!.

Miaka ya 70s Tanzania ilisifika sana kwa kutoa wakimbiaji bora, wakimbiaji wazuri ni watu wa makabila ya wafugaji na wawindani wa milimani, hivyo kina Filbert Bayi, Suleiman Nyambui, Gidamish Shahanga, Juma Ikangaa, Zebedayo Bayo, Zakaria Barie, John Steven Akwaari, Restituta Joseph, Simon Naali etc, wote hawa ni watu wa kabila moja au jamii za wafugaji wa milimani, hivyo Tanzania tukitaka kujenga timu imara ya riadha, timu ya ushindi, lazima tuwaendeleze watu wa kabila hilo au jamii hizo.

Wakati wa Nyerere, watu wa makabila fulani walifanya vizuri kwenye maeneo fulani kuliko makabila mengine, mfano Jeshini na polisi ni watu wa Musoma/Mara.

Ukabila Mzuri Katika Uteuzi.
Kufuatia kabila la Wasukuma kuwa ndilo kabila kubwa kabisa nchini Tanzania, ndilo kabila lenye watu wengi zaidi, hivyo automatically, tukifuata principals of proportionality, Wasukuma ni lazima wawe wengi kila mahali, hii ni halali yao na sio upendeleo!.

Ukitokea wewe ni mteuzi, ukaletewa majina matatu wote wenye sifa sawa na mmoja wao ni Msukuma, jee utaogopa kumteua huyo Msukuma kwa sababu ya kuchelea utaonekana ni mkabila?, zikitokea nafasi, halafu kati ya walioomba wote, wenye sifa zaidi ni Wasukuma, then let it be, hata Wasukuma wakijazana sana, as long as ndio wenye sifa, then huu ni ukabila mzuri, hivyo natoa wito kwa JPM, endelea kuteua Wasukuma, wajaze kila mahali as long as ni watu wenye sifa na ni wachapa kazi, then wewe teua tuu, wanaosema waache waseme, watasema mchana msiku watalala.

Ukabila Mbaya Katika Uteuzi.
Ikitokea kuna nafasi za uteuzi, then ukaamua kwa makusudi kutafuta mtu wa kabila lako, ambaye hana sifa, lakini kwa vile ni kabila lako, unampa

Inaendelea....
Paskali ni sawa kwamba ukichukulia only population tribal proportions lakini si kweli kwamba katika uteuzi lazima wajitokeze wengi katika uteuzi kwasababu uteuzi unakuwa na vigezo, na vigezo hivi ndivyo vinavyo ondoa usahihi wa hoja yako.ukweli mwingine kwa jicho la tatu naliona tatizo la msingi Naona unajalibu kutetea Usukuma kwa maana ileile kwe vile nawe ni msukuma vinginevyo usingejitokeza na hoja dhaiifu kama hii,wasukuma kuwa wengi haina uhusiano na wasomi wengi ni wa kabila la wasukuma.
 
Wanabodi,
Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila mbaya!.

Sisi wanamitandao ya kijamii lazima tufanye a responsible social networking ikiwemo kulisaidia taifa lisiangamizwe na sentiments zozote za ubaguzi au kibaguzi ziwe ni za Ukanda, Ukabila au Udini.

Kwanza tukubaliane sote in principle kuwa siasa zozote za Ukanda, Ukabila na Udini ni tatizo na ni detrimental, ni ugonjwa mbaya Kabisa kwa taifa letu and infact ni sumu!, a very poisonous Vernon!.

Watu wanaizungumza sasa kwa vile imezungumzwa na Lissu, lakini tukubali tukatae, ukanda upo, ukabila upo na udini upo na ni tatizo.

Hatua ya kwanza ya kuondokana na ubaguzi huu, kwanza ni by acceptance kwa kulikubali tatizo na kuwa ni kweli lipo na sio by denial, kama siku zote tunavyofanya. Dawa ya tatizo ni kulikabili kwa kulichimba kiini chake hadi kwenye mizizi kisha kuling'oa.

Mimi naomba kukiri wazi kabisa kuwa ni miongoni mwa wana jf ambao tulibaini tangu siku nyingi kuwa taifa letu linanyemelewa na sumu za siasa za ukanda, udini na ukabila na nilisema wazi hapa.

Mwezi August Mwaka 2014, nilipotajiwa kwa mara ya kwanza, jina la mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015, kuna kitu kama nilikisikia na nikakisema hapa

Hivyo ni kweli kabisa kuna udini mzuri na udini mbaya, kuna ukanda mzuri na ukanda mbaya na pia kuna ukabila mzuri na ukabila mbaya, lets make good use ya ukanda mzuri, ukabila mzuri na udini mzuri kwa maendeleo ya taifa letu.

Mfano, kabila la Wamakonde ndio mabingwa wa kuchonga vinyago, wachongaji mabingwa kabisa ni Wamakonde walioko Tanzania, Wakenya, Waganda, Rwanda na Burudi, wanakuja kununua vinyago Tanzania na kuvi export, hivyo kama tunataka kumiliki soko la vinyago, tuwaendeleze Wamakonde, na sio kabila jingine lolote!.

Miaka ya 70s Tanzania ilisifika sana kwa kutoa wakimbiaji bora, wakimbiaji wazuri ni watu wa makabila ya wafugaji na wawindani wa milimani, hivyo kina Filbert Bayi, Suleiman Nyambui, Gidamish Shahanga, Juma Ikangaa, Zebedayo Bayo, Zakaria Barie, John Steven Akwaari, Restituta Joseph, Simon Naali etc, wote hawa ni watu wa kabila moja au jamii za wafugaji wa milimani, hivyo Tanzania tukitaka kujenga timu imara ya riadha, timu ya ushindi, lazima tuwaendeleze watu wa kabila hilo au jamii hizo.

Wakati wa Nyerere, watu wa makabila fulani walifanya vizuri kwenye maeneo fulani kuliko makabila mengine, mfano Jeshini na polisi ni watu wa Musoma/Mara.

Ukabila Mzuri Katika Uteuzi.
Kufuatia kabila la Wasukuma kuwa ndilo kabila kubwa kabisa nchini Tanzania, ndilo kabila lenye watu wengi zaidi, hivyo automatically, tukifuata principals of proportionality, Wasukuma ni lazima wawe wengi kila mahali, hii ni halali yao na sio upendeleo!.

Ukitokea wewe ni mteuzi, ukaletewa majina matatu wote wenye sifa sawa na mmoja wao ni Msukuma, jee utaogopa kumteua huyo Msukuma kwa sababu ya kuchelea utaonekana ni mkabila?, zikitokea nafasi, halafu kati ya walioomba wote, wenye sifa zaidi ni Wasukuma, then let it be, hata Wasukuma wakijazana sana, as long as ndio wenye sifa, then huu ni ukabila mzuri, hivyo natoa wito kwa JPM, endelea kuteua Wasukuma, wajaze kila mahali as long as ni watu wenye sifa na ni wachapa kazi, then wewe teua tuu, wanaosema waache waseme, watasema mchana msiku watalala.

Ukabila Mbaya Katika Uteuzi.
Ikitokea kuna nafasi za uteuzi, then ukaamua kwa makusudi kutafuta mtu wa kabila lako, ambaye hana sifa, lakini kwa vile ni kabila lako, unampa

Inaendelea....
Asante Pasco kwa hoja nzito. Kwa maoni yangu, neno UKABILA peke yake haliwezi kuwa na maana nzuri, kwa hiyo hakuna kitu kama UKABILA MZURI. Ukiisha kusema tu hapa pana UKABILA, maana yake kuna upendeleo kwa misingi ya ukabila. na hiyo siyo nzuri asilani. ni kweli kwamba tunatakiwa hasa kuangalia uwezo wa utendaji, kustahili kwa mtu kwa maana ya kuwa na vyeti vinavyothibitisha elimu ya kiwango cha kutosha, nk. lakini katika kujenga taifa, katika kuimarisha utangamano na umoja wa kitaifa, na katika kuleta amani na utulivu wa nchi, huwa kuna mambo inatakiwa kuyazingatia.

Kwa mfano, kwa sababu za kihistoria, mojawapo uwepo wa wamisionari wenye wepesi wa kuwekeza katika elimu, afya na mafunzo ya ufundi, maeneo fulani kama Kilimanjaro yalipata kiwango kikubwa cha mashule na hospitali, kulinganisha na maeneo mengine katika Tanzania, mfano Lindi au Kigoma na, Yes! Usukumani! kwa hiyo kama ukiangalia tu uwezo wa mtu na elimu yake, ungelazimika kuteua wachaga wengi sana, na hii itavunja misingi ya umoja wa kitaifa, na kupanda sumu kali katika taifa letu. hapo zilitakiwa jitihada na mikakati kuhakikisha kwamba maeneo yote ya Tanzania yanafaidika na keki ya taifa, na kupata nafasi sawa katika kulijenga taifa.

Wasukuma (pamoja na wanyamwezi), hata kama ni wengi sana, lakini hawana idadi kubwa ya watu waliondaliwa kwa ajili ya nguvu kazi ya taifa kwa maana ya elimu. Wasukuma wamelima pamba miaka mingi sana. Wachaga wamelima kahawa kwa miaka mingi sana. lakini nenda vijiji vya usukumani, hutaona dalili yoyote kwamba familia nyingi zimelima na kuuza pamba kwa miongo na miongo. lakini ukienda uchagani, utaona matokeo ya jitihada za wachaga. hii huwa inaniumiza sana. maana hata ukienda Bukoba, utaona dalili ya watu kufaidika na ulimaji wa kahawa kwa miaka mingi iliyopita. Kwa nini wasukuma wameshindwa kutumia fursa walizopata kujiletea maendeleo? ni kwa sababu ya "laana ya mifugo"? kwamba msukuma hamruhusu mtoto kwenda shule kwa sababu anahitaji kuchunga ng'ombe na mbuzi? ni kwa sababu msukuma akipata fedha ya mauzo ya pamba yake, anaongeza wake, ananunulia watu pombe, na kuzifuja? huo ni mjadala mwingine.

Tatizo linakuja pale ambapo wasukuma watachomoza kwa sababu msukuma amekaa ikulu. inawezekana wakahamasika tu wenyewe, lakini mimi nadhani jitihada za kurekebisha mapungufu ya usukumani yanatakiwa kufanyika muda wote bila kujali nani yuko ikulu
 
Hizi kelele za ukabila zimeanza kusikika katika awamu ya tano, kaka Tundu Lissu kaamua kwenda petrol station akiwa na kipande cha sigara, kaamua kukoleza moto.

Tabora, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita, ni mikoa mitano ambayo wenyeji wake kwa asilimia 95 ni wasukuma. Hakuna kabila ambalo lina wenyeji wanaoishi katika mikoa mitano zaidi ya kabila la Wasukuma. Halafu eti hawa watu wakipewa nafasi serikali watu wanalalamika uwepo wa ukanda!!.

Hii ni roho mbaya na ubinafsi wa hali ya juu, kwa hiyo wasukuma hata wakisoma mpaka kufikia ngazi ya uprofesa na udaktari wa falsafa wasipewe vyeo kwa sababu itaonekana kuwa upo upendeleo!!.

Enzi zile pale TRA walipokuwepo mabosi zaidi ya saba wanaotoka mkoa mmoja, haukuwa ni upendeleo wa ukabila na ukanda!!. Mpaka kuna bosi mmoja wa pale TRA akalazimika kuliongelea suala hili kwa ukali, akitetea professionalism ya mabosi wale waliolalamikiwa kupewa vyeo kiupendeleo.

Wanaotaka status quo iendelee ni wale wale waliozoea maisha ya upigaji ya Dar, maisha ya mission town. Bado mpaka leo hii hawaamini kwamba jana imeshaondoka na iliyopo ni leo hii. Pole maalum kwao.
 
Ana maana hakuna msukuma aliye mkabila. Ila wao wako wengi na wengine hawajui. Mbona wabongo hamuelewi.?!.
 
Ukiona MTU anaongelea ukabila bila shaka ni mkabila. Na waote wanaomtazama JPM kwa ukabila nao pia ni wakabila. Hivi unawezaje kuona tofauti ya binadamu mwenzio bila kujitazama wewe kwanza? Hivyo Pascal Mayala una elements za ukabila au ukanda, pamoja na kuwa na Mimi ni msukuma sijawahi kujinasibu kwa kabila hii, wala sijisifu zaidi ya utani. Ila bango lako nakipuuza kwa nguvu zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wasukuma wamesoma kumzidi naniii mbona mnaleta
ukizungumzia watu wengi kwenye elimu unazungumzia

wahaya
wachagga
wanyakyusa

ao ndo waliosoma shule na si kwa bahati mbaya ni sababu missionary zilijengwa kwao
wasukuma ni wengi lakini weni hawajaelimika yaani kundi la watu ambao hawajaenda shule wengi ni wasukuma ukubali ama ukatae

kitendo cha mtu kumpa cheo kikubwa mtoto wa dadake manake ni Nepotism/upendeleo na hiki lazima tukiseme

kwani mkapa ana kikwete walikua hawana ndugu waliosoma ...?
uifanya upenedeleo lazima tuseme
 
Makamu wa Rais - Zenje
Waziri Mkuu - Lindi
Spika - Dodoma
Naibu Spika - Mbeya
Mawaziri wandamizi ;
Lukuvi - Iringa
Mwakyembe - Mbeya
Simbachaweni - Dodoma
Makamba - Tanga
Ummy Mwalimu - Tanga
Maghembe - Kilimanjaro
Kairuki - Kilimanjaro
Mpango - Kigoma
Ndalichako - Kigoma
Mwigulu - Singida
Mbarawa - Zenji
Kabudi - ???
Nape - alikuwa Lindi
Muhongo - Mara
Mahiga - Iringa
Lwenge - Iringa
Mhagama - Ruvuma
Mwinyi - Zenji

Huu ukabila na ukanda upo wapi hapo, Lissu atavuna tu chuki anayopanda 2020
Kabudi - Singida.

Mkuu safi sana kwa kuonyesha jinsi gani baraza la mawaziri lilivyo na watu kutoka kila kona ya Tanzania.

Wanasema kuna mtu anaitwa Dotto ambaye ndiye mshika fedha wa hazina kwa sasa, wanasema huyu ni mtoto wa dada yake JPM.

Wanataka kutuongopea kwamba iwapo mzee ENL angepewa ikulu mwaka 2015, mwanae Fred na marafiki zake wasingepewa nafasi nyeti za uongozi.

Ukiona mtu anapewa urais halafu hana ndugu yake angalau mmoja ambaye ni mtu wake wa karibu kwenye masuala ya urais basi ujue huyo mtu hajielewi.

RIP Nyerere alikuwa na mzee Butiku, kama msiri wake. Donald Trump anaye mkwe wake Jared Kushner kama mmoja wa wasiri wake.

Tundu Lissu analeta siasa ambazo madhara yake ni makubwa kuliko ule umaarufu wa muda mfupi anaoutafuta.
 
It's our turn to eat imebisha hodi Tanzania. Wasukuma siyo wapole tena, kiburi kimewatawala.Sehemu za burudani wapo noisy and boisterous. Humility imewatoka. Wamesahau ukweli mmoja- 2020 will be one against makabila mengine ya Tanzania.Huu ndio ukweli.
 
Back
Top Bottom