"TUVIACHIE VYOMBO VYA USALAMA! OOH SORRY, VYOMBO VYA DOLA"
-------------------------------------------------------------
Hii sio kauli mpya. Na kwa kumbukumbu zangu sikumbuki ni lini vyombo vinavyoitwa vya usalama vilitoa majibu panapotokea matukio ya uhalifu dhidi ya watu wanaokosoa serikali au wanaharakati wengine.
Tumeviachia vyombo vya usalama tukio la kutekwa, kuteswa na kutupwa porini ili afe, Dr. Steven Ulimboka.
Tumeviachia vyombo vya usalama tukio la mauaji ya Dr. Senghondo Mvungi.
Tumeviachia vyombo vya usalama kutekwa na kuteswa kwa Absalom Kibanda.
Tumeviachia vyombo vya usalama tukio la mauaji ya Prof. Mwakyusa
Tumeviachia vyombo vya usalama tukio la kumwagiwa tindikali Mh. Saed Kubenea
Tumeviachia vyombo vya usalama tukio la kupotea Ben Saanane
Tumeviachia vyombo dola miili ya watu saba iliyokuwa kwenye mifuko, iliyotupwa mto Ruvu.
Tumeviachia vyombo vya usalama kumwagiwa tindikali wazungu kule Zanzibar
Tumeviachia vyombo vya usalama mauaji kwa kuchinjwa, Alphonse Mawazo
Tumeviachia vyombo vya usalama kulipuliwa mikutano ya Chadema kwa mabomu ya Arusha.
Tumeviachia vyombo vya usalama tukio la kulipuliwa kwa mabomu ofisi za IMMMA
Leo Lissu anapigwa risasi nyingi kwa lengo la kuuawa, kauli ni ileile! Tuviachie vyombo vya usalama.
Nikumbusheni ni matukio mangapi kati ya hayo hapo juu yaliyotolewa majibu na hivyo vinavyoitwa vyombo vya usalama!
Sijawahi kuona kitu kinachoitwa chombo cha usalama katika nchi yangu. Kuna vyombo vya dola! Kwa hiyo kauli rasmi iwe "TUVIACHIE VYOMBO VYA DOLA".
Maana yake ni kwamba tusitegemee kuwe na majibu yoyote ya kuridhisha kama dola ndio linahusika na matukio ya uhalifu. Chombo cha dola hakiwezi kukamata dola!
Kuna nchi zina vyombo vya usalama. Kwa mfano CIA ya Marekani. Ndio maana CIA wanaweza kumchunguza Rais wa nchi yao ya Marekani. Kwa sababu ni chombo cha usalama kwa ajili ya wamarekani. Hata pale CIA wanapotuhumiwa kufanya uhalifu, mara nyingi huwa kwa nguvu zingine, sio Marekani.
Sisi huku tunafanya vyombo vya dola kwa ajili ya kulinda dola, sio vyombo vya usalama kwa ajili ya usalama wa taifa lote/raia wote. Tuna vyombo vya dola kwa ajili ya dola na watu wanaopenda na dola, na wanoonekanekana kushabikia dola.
TUVIACHIE VYOMBO VYA DOLA kama tulivyoacha huko nyuma, na bahati nzuri watanzania ni watu wa kuacha.
Lakini ole wetu, wanyonge watakapochoka na kuamua kurudisha ngumi! OLE WETU.
Sent using
Jamii Forums mobile app