Tuige mfano wa Ethiopia kuhusu matumizi ya cheo cha Daktari

Tuige mfano wa Ethiopia kuhusu matumizi ya cheo cha Daktari

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,099
Reaction score
13,709
1755818821955.png

Ethiopia imepiga marufuku watu wasiosomea udaktari kuitwa au kujiita madaktari ima kwa sababu ya udaktari wa. heshima kama ule wa Jakaya Kikwete na Samia au wa kununa kama ule wa Gwajima na Msukuma. Nasi, kama taifa lenye watu wanaoona mbele hata kama tupo wachache, tupige marufuku ukilaza huu. Katika kufanya hivi, tusijali nani ni wanufaika hata kama wana mamlaka kiasi gani. Hii ni nchi yetu si yao na ithibati ya elimu si yetu pekee bali dunia nzima. Mbona hatusikii marais au mawaziri wa mataifa yanayotufadhili wakijipachika udaktari kama hawa wetu wasio na elimu yoyote zaidi ya kuungaunga? Pia, tuende mbele. Tuchunguze na kupiga marufu vyuo vya kweli hata vya mfukoni vinavyogawa shahada za heshima kama uroda ili kutafuta kuwa karibu na wenye madaraka vihiyo na vilaza wasiojua hata maana ya udaktari wanaoupwakia tokana na uzwazwa.​

Naomba kuwasilisha.​

 
Binafsi naunga mkono hoja kama itapendekezwa,
Hivi ni kweli Bab tall anapewa udaktari wa heshima, basi Diamond angekua professor
 
Kabisa na ni kama kudharaulisha Elimu sasa mtu aliyesomea u clerk .
Mtu level yake ya elimu ya darasani ni ukarani kama samia sashivi naye anaitwa daktari eti wa heshima.
Hii ni dharau kubwa sana kwa elimu yetu
 
Na huo ni utaratibu wa dunia nzima sisi hapa ushamba na uchawa tu ndiyo unasumbua eti Daktari Samia Suluhu au Daktari Jakaya Mrisho Kikwete upuuzi tupu.
 
Back
Top Bottom