Kijana wa Ifoza
JF-Expert Member
- Oct 31, 2025
- 1,180
- 2,302
Baada ya uchafuzi wa Kongo uliomuweka Kabila Mdogo madarakani, wakongo waishio Ulaya waliojiita Les Combattants walihakikisha wale waote waliosapoti na kumpigia kampeni Kabila hawafanyi show Ulaya.
Waliopatwa na hiyo dhahama walikuwa Koffi Olomide na wengineo. Kosa lao kubwa lilikuwa kupokea Pesa kutoka chama cha Kabila na kutunga nyimbo za Kampeni kama hawa wetu kina Hamornize na Diamond walivyofanya. Hizi zilikua Kampeni za mwaka 2011 za Kongo ambazo wengi hakukubaliana nazo.
Kwa muda wa miaka 10 mpaka 12 walipojaribu kufanya show Ufaransa ama Ubelgiji hata Uingereza walifanyiwa vurugu mpaka Polisi walizuia ma concert yao.
Sasa ni wakati wetu kuwafanya hawa walipe kwa kutusaliti Watanzania. Iwe Tanzania ama nje ya Tanzania tuhakikishe hawafanyi show yoyote mpaka turidhike kama wamejitambua kuwa wao pia ni watanzania na wanatakiwa kuungana na Watanzania wenzao kukemea uonefu siyo kulala kitanda kimoja na wanyonyaji na wezi wa mali zetu za Umma
Mungu Ibarikia Tanzania
Nawasilisha