Tuijue Katiba: Rais akifia madarakani, basi makamu wake aliyegombea naye akapigiwa kura anarithi. Je, vipi kama makamu hakupigiwa kura?

Tuijue Katiba: Rais akifia madarakani, basi makamu wake aliyegombea naye akapigiwa kura anarithi. Je, vipi kama makamu hakupigiwa kura?

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Kuna ibara kwenye Katiba ya Tanzania kwamba endapo Rais aliyeko madarakani akakosa uwezo wa kuendelea kuongoza, basi Makamu wake ambaye amepigiwa kura na wananchi wakati wa uchaguzi mkuu atachukua nafasi yake!

Tuelimishane hapa! Vipi Kama Makamu wake alipatikana bila kupigiwa kura na wananchi yaaan hakuwa mgombea mwenza, alafu aliyekomadarakani akapoteza sifa za kuwa Rais, nani anaongoza nchi kwa mujibu wa Katiba?

Swali hili unaweza kuja kichwa kichwa kumbe kuna mambo mengi ndani ya kujifunza.

Naomba mods wasiondoe Uzi huu ni kwa ajili ya mafunzo kujua sheria za utawala na hapo baadae unaweza kufufuliwa miaka tata 40 ijayo kwakuwa maandishi uishi sana.

Britanicca
 
Huu ni mtazamo wangu.

Kwa kuwa katiba imesema makamu wa Rais atakuwa Rais baada ya Rais kufariki au mengineyo hivyo haijalishi ni makamu wa namna gani ,kama katiba imemkubali kama makamu wa Rais basi atakuwa Rais.

Lakini kwa upande mwingine katika mazingira hayo makamu wa Rais na Rais wote watakuwa hawachaguliwa Wala kupigiwa kura popote ,hapo ndio katiba inabidi iseme zaidi nchi kuwa na viongozi ambao hawakuchaguliwa madhara yake na faida zake ni zipi
 
Kuna sehemu kwenye katiba inasema 'makamu aliyepigiwa kura'?

Katiba inasema, naomba kunukuu;
"Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano..."

Ukisoma hiyo ibara ya 37 kifungu cha 5, haitanabaishi kuwa awe makamu aliyepigiwa kura.

Awe aliyekuwa mgombea mwenza ama aliyepatikana kwa njia za kikatiba baada ya aliyekuepo kutangulia, kujiuzulu, au kuondoka kwa namna yeyote ile.
 
Kuna ibara kwenye Katiba ya Tanzania kwamba endapo Rais aliyeko madarakani akakosa uwezo wa kuendelea kuongoza, basi Makamu wake ambaye amepigiwa kura na wananchi wakati wa uchaguzi mkuu atachukua nafasi yake!

Tuelimishane hapa! Vipi Kama Makamu wake alipatikana bila kupigiwa kura na wananchi yaaan hakuwa mgombea mwenza, alafu aliyekomadarakani akapoteza sifa za kuwa Rais, nani anaongoza nchi kwa mujibu wa Katiba?

Swali hili unaweza kuja kichwa kichwa kumbe kuna mambo mengi ndani ya kujifunza.

Naomba mods wasiondoe Uzi huu ni kwa ajili ya mafunzo kujua sheria za utawala na hapo baadae unaweza kufufuliwa miaka tata 40 ijayo kwakuwa maandishi uishi sana.

Britanicca
Advocate Pascal Mayalla, Adv Allen Killewela watatuelimisha kwa jambo hili.
 
Back
Top Bottom