Tuisaidie Taifa Start ili nchi isipate aibu!

Team mbovu, hata sijui wanacheza nini, Nyoni ndo uchochoro kabisaa!! Jezi sijui ni za Nchi gani!! ?! Zimbabwe au?? Yaan kichefuchefu!!
 
Hawa wash**zi kazi yao ni kutubadilishia jezi kila mwaka na kuweka kambi zisizo na kichwa wala miguu
 
Nilishaachana na hiyo timu siku nyingi tu, nimebaki na Yanga na Arsenal
 
Malinzi ameharibu Soka.

Wakati wa Kim timu ilikuwa inaeleweka Hii sio bwana.

Ok hajui lolote.

Nimezima Tv
 
Tatizo ni kocha.

Timu ya Kim Poulsen ilikuwa Nzuri sana. Walimuonea bure angekuwepo saa Hii tungekuwavmbali.

Tulikuwa na uwezo wa kusumbua timu Kubwa acha Lesitho etc
 
Tumefungwa kwa kuwa timu haina jina LA kutisha ndiyo maana tunataka kubadili jina.
 
Malinzi hovyo sana huyu sijui kala maharage ya wapi huyu
 
Mtanzania toa maoni yako ni kitu gani kifanyike ili timu ya Taifa iondokane na hii aibu ya kila mwaka! Je tatizo ni kocha au? toa mawazo yako hapa ili hata Jamal Malinzi akipitia hapa aweze kuona watanzania wanasema nini juu ya timu yao ya taifa.Hii ni aibu tuisaidie timu yetu.
 
Last edited by a moderator:
na zile ndevu ka kalpeters ahhggh!!
 
Dah inatia huruma.....sana yani nikiiangalia nasikia huruma harafu kocha hana hata wasiwasi....
 
Mtapiga kelele kumtukana kocha, au Malinzi na TFF yote lakini sio suluhisho.. Ukweli tatizo ambalo lipo kwenye sekta ya michezo ndilo hilo ambalo lipo kwenye siasa na nyanja nyingine zote hapa Tanzania..

Tatizo kubwa ni watu wasio na fani kuingia na kuongoza kwenye fani ya michezo kama ilivyo na kwingineko.. Viongozi wengi wako kimaslahi zaidi kuliko kuangalia maslahi ya soka, hawana ubunifu na vile vile hawana utashi wa kuongoza soka..

Uongozi wa kisiasa nao kwa vile unashikwa na wenye maslahi binafsi ndo linakuwa tatizo kabisa kwani kuendelea kwa michezo katika nchi kunategemea na utashi wa viongozi wa kisiasa katika kuwekeza kwenye michezo..

uki-combine hizo factors mbili hapo juu utagundua kocha, TFF na wachezaji hawana sababu ya kulaumiwa kwa kuwa hii ni product mbovu ilizalishwa katika mazingira mabovu na uongozi mbovu wa kisiasa.. Na ndo maana hatuna mafanikio hata kwenye vilabu vyetu hivi vya mpira..
 
Kuna kila dalili kuwa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu inayoshiriki mashindano ya COSAFA kama mwalikwa ikapoteza mchezo mwingine leo dhidi ya Madagascar.Mpaka kipindi cha pili kinaanza Stars wapo nyuma kwa magoli 2

Katika mechi yao ya kwanza ambayo kidogo walionekana kucheza vizuri walitandikwa bao 1 bila majibu na Vijana wa Swaziland

Kwa mechi ya leo Stars wanaonekana kuwa dhaifu mbele ya Vijana wa Madagascar,na wasio na mbinu za kushinda hii mechi na kuna uwezekano wakaongezwa magoli mengine

Hivi kama tunashindwa kutoa hata droo na Swaziland na Madagascar hvi tutamfunga nani?

Nini tatizo la Stars na soka letu?
 
Cc Jamali Malinzi kuja huku ulete majibu, wewe toka umeingia hapo mjengoni ndio imekuwa hovyo kabisa timu yetu hivi una majibu kweli?
 
Last edited by a moderator:
kama ameshindwa kuifunga timu kama madagasca je hao misri na nigeri Malinz hzo pesa mnazo mlipa hyo mzungu bora mkawekeze fiesta
 
Malinzi tunaelewa unasikia na ndo hivyo mpira umeisha 2-0,mpigie simu huyo mpuuzi wenu mnamuita kocha aondoke arudi kwao haraka sana vinginevyo hapo hamtakaa nyote ..fukuza kocha kabla hakujapambazuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…