Mtapiga kelele kumtukana kocha, au Malinzi na TFF yote lakini sio suluhisho.. Ukweli tatizo ambalo lipo kwenye sekta ya michezo ndilo hilo ambalo lipo kwenye siasa na nyanja nyingine zote hapa Tanzania..
Tatizo kubwa ni watu wasio na fani kuingia na kuongoza kwenye fani ya michezo kama ilivyo na kwingineko.. Viongozi wengi wako kimaslahi zaidi kuliko kuangalia maslahi ya soka, hawana ubunifu na vile vile hawana utashi wa kuongoza soka..
Uongozi wa kisiasa nao kwa vile unashikwa na wenye maslahi binafsi ndo linakuwa tatizo kabisa kwani kuendelea kwa michezo katika nchi kunategemea na utashi wa viongozi wa kisiasa katika kuwekeza kwenye michezo..
uki-combine hizo factors mbili hapo juu utagundua kocha, TFF na wachezaji hawana sababu ya kulaumiwa kwa kuwa hii ni product mbovu ilizalishwa katika mazingira mabovu na uongozi mbovu wa kisiasa.. Na ndo maana hatuna mafanikio hata kwenye vilabu vyetu hivi vya mpira..