Tuisaidie Tume ya kuboresha taasisi za haki jinai kwa kuweka maoni yatu hapa

Tuisaidie Tume ya kuboresha taasisi za haki jinai kwa kuweka maoni yatu hapa

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Posts
3,436
Reaction score
7,955
Wadau kama tunavyofahamu Mh Rais Samia Suluhu Hassan aliteua wajumbe tisa wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha taasisi za Haki Jinai nchini inayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue.

Lengo kuu ni kuangalia kwa mapana hizi taasisi za kutoa haki ambazo ni pamoja na mahakama, Polisi, Takukuru na ofisi ya mashtaka ikiwemo DPP na DCI

JF ni kubwa na inaweza toa mchango mkubwa kwa tume hii

yapo mengi ya kuboresha tuangalie mazuri na mabaya katika hisi taasisi! ikiwemo hata namna ya kuboresha!

mimi naona JF inaweza sehemu ya suluhisho ya mambo mengi kwa Tume hii

Tuchangie kwa pamoja ili tume ipate maoni
 
mie naanza kwa kuchangia kuanza na Polisi

1. Polisi waboreshewe mishahara na mahitaji yao muhimu!
2. Polisi wapatikane kwa njia za wazi sio kunebana watoto wa jamii hiyo hiyo!

3. Polisi wafundwe na waletwe kwa jamii ili wajifunze kuzoea raia na kukaa nao ili wawe kimbilio la wanyonge wakati wa kudai haki.
 
1. Kifungo Cha gerezani kiwe Si zaidi ya miaka 25.
2. Wafungwa waliohukumiwa miaka 10 na zaidi wasio wa makosa ya mauaji na uhalifu wa silaha waachiwe baada ya kutumikia nusu ya vifungo vyao.
3. Watoto kuanzia miaka 15 na ambao wahajafikisha miaka 18 hukumu zao zisizidi miaka 3.
The lost
 
1. Mtuhumiwa yeyote wa kosa au makosa ya jinai ambayo baadaye itathibitika sio kweli i.e. atashinda kesi dhidi ya Jamhuri, Serikali iwajibike kwa lazima kumlipa mtuhumiwa fidia kwa muda aliokaa mahabusu na hasara zilizotokana/alizopata kutokana na kushikiliwa na Polisi au kukaa mahabusu.
2.Mwanamke mjamzito endapo atahukumiwa kwa haki, basi aanze kutumikia kifungo chake baada ya kujifungua na iwe ni baada ya Daktari aliyeidhinishwa na Serikali kuridhika kwamba afya yake inaruhusu.
3. Mahakama za mwanzo zizingatie Elimu, uzoefu na Weledi wa Wazee wa Mahakama.
4. Polisi wajiepushe na matumizi ya Lugha za vitisho, kejeli au kumhoji mtuhumiwa kwa mtindo wa maswali elekezi (Leading Questions) ili mtuhumiwa atoe majibu bila hiari yake yatakayo fanikisha kile wanacholenga kipatikane kwake hata kama sio cha ukweli. Aidha Polisi wasiwe na Hoja sumbufu (vexing questions)e.g. anakuja polisi anakuuliza maswali na anaondoka haandiki chochote, na punde anakuja polisi mwingine anauliza maswali yale yale ambayo mtuhumiwa alishayatolea majibu naye huyu haandiki popote, na mwishoni anakuja mwingine tena anamhoji mtuhumiwa kitu kile-kile na hatimaye anakijazia maneno(Uzushi) kwa hoja ambazo mtuhumiwa hakuzitoa pale wakati polisi huyo anapokabidhi kwa kiongozi wake kituoni.(Kumbuka msemo usemao Maswali ya kipolisi) mwishoni kabisa ndipo wanamtaka mtuhumiwa aandike au wachukue maelezo yake. ambayo yatatumika kakuandaa PH.
 
Wadau kama tunavyofahamu Mh Rais Samia Suluhu Hassan aliteua wajumbe tisa wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha taasisi za Haki Jinai nchini inayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue.

Lengo kuu ni kuangalia kwa mapana hizi taasisi za kutoa haki ambazo ni pamoja na mahakama, Polisi, Takukuru na ofisi ya mashtaka ikiwemo DPP na DCI

JF ni kubwa na inaweza toa mchango mkubwa kwa tume hii

yapo mengi ya kuboresha tuangalie mazuri na mabaya katika hisi taasisi! ikiwemo hata namna ya kuboresha!

mimi naona JF inaweza sehemu ya suluhisho ya mambo mengi kwa Tume hii

Tuchangie kwa pamoja ili tume ipate maoni
Nimefanya utafiti mdogo. Baadhi ya Taasisi za Serikali zimegeuzwa kuwa Magereza au zaidi ya Magereza.

moja wapo ni Muhimbili.

Muhumbili jmekuwa magereza kwa maiti na wagonjwa wasio na uwezo.

Urasimu uliowekwa unasababisha wagonjwa wasipate Tiba na wengine kupatwa na magonjwa mengine.

Kwa ujumla makundi haya mawili yanakosa haki za msingi za binadamu.

Sababu kuu ni kwamba serikali inawataka uongozi wa muhumbili kujiendesha kibiarasha kama hospitali nyingine binafsi

Tume ya haki za binadamu ione Haja ya kufanya uchunguzi iwapo Wagonjwa wasio na uwezo wanapata haki na thamani ya utu wao.
 
Back
Top Bottom