Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Matukio, mwenendo na mitazamo ya wengi kwa sasa yamejikita kwenye mchakato wa kupata Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA. Tunachokiona kwa sasa nimnyukano mkali ambao ulianza kama tetesi na hususan michakato mirefu ya chaguzi kuanzia ngazi za chini hadi sasa kwenye nafasi ya juu ya uongozi wa chama.
Nimeshawishika kuandaa uzi huu mahususi kujadili yanayojiri hususan mchakato wa kidemokrasia ndani ya chama hiko kikuu cha Upinzani nchini.
Pascal Mayalla, Yericko Nyerere Retired johnthebaptist Chief TAJIRI MKUU WA MATAJIRI Lucas Mwashambwa MtuKwao figganigga
Nimeshawishika kuandaa uzi huu mahususi kujadili yanayojiri hususan mchakato wa kidemokrasia ndani ya chama hiko kikuu cha Upinzani nchini.
- Mchakato wa Uchanguzi ndani ya CHADEMA kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya Kanda, umeshawishika kwamba demokrasia ndani ya CHADEMA inakua au inadumaa?
- Sisi wadau wa Demokrasia kwenye ngazi za chaguzi za Kitaifa, tumekosoa na kushauri sana namna bora ya kuboresha chaguzi za serikali, je ndani ya CHADEMA kuna mfanano au utofauti linapokuja suala la chaguzi ndani ya chama?
- CCM imetawala nchi hii kwa imla zaidi ya miaka 60 tangu uhuru, Watanzania walio wengi tunaona kwa facts hakuna maendeleo mtambuka yaliyoletwa na chama hiki, je Katiba ya CHADEMA inaweka viwango gani kwenye eneo la kung'ang'ania madarakani kama CCM inavyolifanyia Taifa letu?
- Tunajifunza nini kwenye hili la Uchaguzi wa ndani wa CHADEMA kulinganisha na michakato ya chaguzi za kiserikali?
Pascal Mayalla, Yericko Nyerere Retired johnthebaptist Chief TAJIRI MKUU WA MATAJIRI Lucas Mwashambwa MtuKwao figganigga