Hii ni moja ya nukuu iliyonigusa kwenye hotuba ya Rais Magufuli ya leo 23/10/2017. Naomba tujadiliane namna ya kutumia huu mtaji tulionao, mtaji wa kuwa wazaliwa wa Tanzania. Kama kuna vikwazo vinavyotufanya tuliowengi tushindwe kutumia huu mtaji tuvianishe.
Karibuni.
Kauli hiyo ina maana nzito sana! Nashukuru kwamba umekuwa ni mmojawapo Wa watu walioguswa na kauli hiyo. Mimi kuna mbili zilinigusa sana Jana. Nyingine ni ile ya kusema hakuzaliwa hata na chupi( tafsiri ni yangu) na hivi hatarudi na chochote alikotoka zaidi ya jeneza tu!
Ni hivi mwanadamu ukishajielewa kuwa hukuja hata na bukuta duniani, basi utatumia sehemu ya maisha yako kutoa na kupokea. Wengi wanaofikiri kinyume na ukweli huo ni watu Wanaotamani muda wote kupokea tu na ndio wale wanaouza rasilimali za nchi bila kujali ustawi Wa wenzao. Ndio wale walio tayari hata kupora vya wenzao.
Mintarafu hilo la kuzaliwa Tanzania kuwa mtaji, ni kwamba nchi yetu bado ina rasilimali za asili lukuki kulinganisha na wananchi Wa sehemu zingine duniani. Kuna ardhi bado kubwa sana na Unaweza kuitumia hiyo kujipatia mkopo benki. Sehemu nyingine ardhi kuipata ni taabu hata kama una pesa. Hapa Tanzania, hata nyumba ya familia, Mjomba, Rafiki na au jamaa inaweza kukupatia au kukuongezea mtaji Wa biashara.
Hapa kwetu business opportunies bado zingali nyingi sana( not fully exploited) kulinganisha na huko kwingineko Ulaya, Marekani au Asia. Ukitaka kujua hilo angalia jinsi wageni wanavyokuja tu na mtaji kiduchu lakini baada ya muda wanaondoka matajiri kiasi kwamba wengine hutamani wapewe kabisa uraia wa hapa hapa. Mifano hai ni wachina. Wachina wanavuna sana pesa hapa. Wanauza hapa Viatu, vifaa vya ujenzi, vyombo vya ndani na kadhalika.
Ni kweli kuzaliwa Tanzania ni mtaji! Natolea mfano eneo la chakula. Eneo la chakula kuna mambo mengi sana kuanzia processing hadi packaging. Hapa kwenye chakula sisi bado tunacheza makidamakida tu. Ukikaa vizuri na ukatumia Jicho la tatu utaona fursa kibao eneo hilo za kuwekeza bado zingalipo.
Kwenye mavazi nako bado kuna fursa nyingi sana za kuweza kutajirika. Ukiangalia nguo kibao bado zinatoka nje. Sawa tunaweza kusema hatuna viwanda vya kuzalisha Nguo. Lakini Hii kwangu ni false excuse. Watu wanafikiria nguo zote zinazoletwa toka nje zinatoka katika viwanda vikubwa tu. Tekinolojia imerahisishwa sana siku hizi. Unaweza kukuta mtu analo eneo mfano wa sitting room lakini anazalisha hapo Kontena na Kontena za Nguo.
Nashangaa bado baadhi ya watu kule Kariakoo wanang'ang'ana kuuza nguo za kutoka nje bila kufikiria kuziongezea thamani.Loh! Niseme nini tena? Mtaji kweli kuzaliwa Tanzania. Tena ni mtaji Wa kweli nyakati hizi za Magufuli.