Tujadili hii kauli: Kuzaliwa Tanzania ni Mtaji

Tujadili hii kauli: Kuzaliwa Tanzania ni Mtaji

JFK wabongo

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2015
Posts
3,887
Reaction score
3,197
Hii ni moja ya nukuu iliyonigusa kwenye hotuba ya Rais Magufuli ya leo 23/10/2017. Naomba tujadiliane namna ya kutumia huu mtaji tulionao, mtaji wa kuwa wazaliwa wa Tanzania. Kama kuna vikwazo vinavyotufanya tuliowengi tushindwe kutumia huu mtaji tuvianishe.
Karibuni.
 
Hii ni moja ya nukuu iliyonigusa kwenye hotuba ya Rais Magufuli ya leo 23/10/2017. Naomba tujadiliane namna ya kutumia huu mtaji tulionao, mtaji wa kuwa wazaliwa wa Tanzania. Kama kuna vikwazo vinavyotufanya tuliowengi tushindwe kutumia huu mtaji tuvianishe.
Karibuni.
Bongo bahati mbaya....
 
Maana yake ni kwamba. Kuna Watanzania wanatumika kama mtaji kwa wanasiasa kwa ajili maslahi yao. Watu wanapewa ubwabwa tshrit khanga na kapelo wanasahau matatizo yao yote
 
[emoji23] [emoji23] Kina kichwa kimepita huko juu kichafu sana.
 
Wanainchi wa Tanzania ni mtaji mzuri sana kwa wana siasa sababu ni rahisi sana kuwaongoza vyovyote utakavyo
 
Mnapo jadili hoja za biashara katika jukwaa hili mnapaswa kuaja masihara na chembechembe za siasa.Jukwaani hili tunapeana changamoto za kijasiriamali na kibiasahara na uchumi. Ni aibu kwa jukwaa hili kujadili kauli hiyo kimasihara kiasi hiki. Kama haujui maana take bora ukae kimya au useme sijui. Ni kauli ya kisiasa lakini yenye maana pana kijasiriamali. Naomba nifafanue kwa uchache. Ili uelewe maana ya kauli ya mh Rais lazima ujenge picha ya mtu ambaye so Tanzania ambaye mnagombea fursa iliopo Tanzania. Kauli inamaanisha kuwapa Kipaonbale watanzania katika fursa zilizo chini. Mfano, wewe uliye zaliwa kando ya ziwa au Bahari hiyo ni faida muhimu kama utataka kuwa mvuvi au mfanya biashara wa samaki kwa kuwa unajua mengi zaidi ya mgeni anaetaka kufanya jambo hilohilo.Pili kuzungumza Lugha ya Kiswahili ni nyenzo muhimu kibiashara has a Africa. Mahali ilipo Tanzania kijiografia NATO ni mtaji kwa wa Tz. mifano ni mingi sana.
 
Inaweza kuwa mtaji kweli lakini sio kila mtu anaweza ku uaccess.
 
Hii ni moja ya nukuu iliyonigusa kwenye hotuba ya Rais Magufuli ya leo 23/10/2017. Naomba tujadiliane namna ya kutumia huu mtaji tulionao, mtaji wa kuwa wazaliwa wa Tanzania. Kama kuna vikwazo vinavyotufanya tuliowengi tushindwe kutumia huu mtaji tuvianishe.
Karibuni.

Kauli hiyo ina maana nzito sana! Nashukuru kwamba umekuwa ni mmojawapo Wa watu walioguswa na kauli hiyo. Mimi kuna mbili zilinigusa sana Jana. Nyingine ni ile ya kusema hakuzaliwa hata na chupi( tafsiri ni yangu) na hivi hatarudi na chochote alikotoka zaidi ya jeneza tu!

Ni hivi mwanadamu ukishajielewa kuwa hukuja hata na bukuta duniani, basi utatumia sehemu ya maisha yako kutoa na kupokea. Wengi wanaofikiri kinyume na ukweli huo ni watu Wanaotamani muda wote kupokea tu na ndio wale wanaouza rasilimali za nchi bila kujali ustawi Wa wenzao. Ndio wale walio tayari hata kupora vya wenzao.


Mintarafu hilo la kuzaliwa Tanzania kuwa mtaji, ni kwamba nchi yetu bado ina rasilimali za asili lukuki kulinganisha na wananchi Wa sehemu zingine duniani. Kuna ardhi bado kubwa sana na Unaweza kuitumia hiyo kujipatia mkopo benki. Sehemu nyingine ardhi kuipata ni taabu hata kama una pesa. Hapa Tanzania, hata nyumba ya familia, Mjomba, Rafiki na au jamaa inaweza kukupatia au kukuongezea mtaji Wa biashara.


Hapa kwetu business opportunies bado zingali nyingi sana( not fully exploited) kulinganisha na huko kwingineko Ulaya, Marekani au Asia. Ukitaka kujua hilo angalia jinsi wageni wanavyokuja tu na mtaji kiduchu lakini baada ya muda wanaondoka matajiri kiasi kwamba wengine hutamani wapewe kabisa uraia wa hapa hapa. Mifano hai ni wachina. Wachina wanavuna sana pesa hapa. Wanauza hapa Viatu, vifaa vya ujenzi, vyombo vya ndani na kadhalika.


Ni kweli kuzaliwa Tanzania ni mtaji! Natolea mfano eneo la chakula. Eneo la chakula kuna mambo mengi sana kuanzia processing hadi packaging. Hapa kwenye chakula sisi bado tunacheza makidamakida tu. Ukikaa vizuri na ukatumia Jicho la tatu utaona fursa kibao eneo hilo za kuwekeza bado zingalipo.


Kwenye mavazi nako bado kuna fursa nyingi sana za kuweza kutajirika. Ukiangalia nguo kibao bado zinatoka nje. Sawa tunaweza kusema hatuna viwanda vya kuzalisha Nguo. Lakini Hii kwangu ni false excuse. Watu wanafikiria nguo zote zinazoletwa toka nje zinatoka katika viwanda vikubwa tu. Tekinolojia imerahisishwa sana siku hizi. Unaweza kukuta mtu analo eneo mfano wa sitting room lakini anazalisha hapo Kontena na Kontena za Nguo.


Nashangaa bado baadhi ya watu kule Kariakoo wanang'ang'ana kuuza nguo za kutoka nje bila kufikiria kuziongezea thamani.Loh! Niseme nini tena? Mtaji kweli kuzaliwa Tanzania. Tena ni mtaji Wa kweli nyakati hizi za Magufuli.
 
Kuzaliwa Tanzania ni mtaji.

Lakini mtajiwa nani?

Wa viongozi. Wakienda nje kuomba misaada waseme tuna wananchi milioni kadhaa wanahitaji msaada, wakipewa misaada wanaichikichia mifukoni mwao.

Kwa hiyo kweli, kuzaliwa Tanzania ni mtaji.

Wa viongozi.
 
Back
Top Bottom