Tujadili Matokeo ya Kidato cha Nne

Tujadili Matokeo ya Kidato cha Nne

🎓 Division I to III - 35.84% (eligible for admission to government-owned A-level schools)

🎓 Division IV - 51.46%

🎓 Division 0 - 12.7%

Katika kila 10 wanafunzi 6-7 system ya elimu ishawatema halafu wanadai ufaulu umeongezeka.

Hapo kitakacho wasaidia ni aidha wazazi wao wawe na uwezo wa kuwaendeleza au Mungu awe amewabariki vipaji ambavyo huwezi kukikataa au Mungu atende miujiza tu. Na kibaya zaidi kwao kaka zao ni mwaka wa 6 huu ni jobless mtaani.
Simpo and clear upanuzi wa elimu ya juu tukianza na advanced level vyuo vya kati vya elimu na ufundi hadi vyuo vikuu serikali ya Tz ipo usingizini sana. Sekta binafsi kwenye elimu inafanya enrollement kubwa kuliko taasisi za elimu zilizo chini ya serikali. Tutegemee kuona waliopata division II wanapelekwa vyuo vya kati kingali kwenye machaguo waliomba wapelekwe advanced level na tutegemee wenye division III kukosa nafasi hata kwenye vyuo vya serikali wataangukia wengi vyuo binafsi.
 
[emoji310] Division I to III - 35.84% (eligible for admission to government-owned A-level schools)

[emoji310] Division IV - 51.46%

[emoji310] Division 0 - 12.7%

Katika kila 10 wanafunzi 6-7 system ya elimu ishawatema halafu wanadai ufaulu umeongezeka.

Hapo kitakacho wasaidia ni aidha wazazi wao wawe na uwezo wa kuwaendeleza au Mungu awe amewabariki vipaji ambavyo huwezi kukikataa au Mungu atende miujiza tu. Na kibaya zaidi kwao kaka zao ni mwaka wa 6 huu ni jobless mtaani.
Walifuta tuition hayo ndo matunda yake
 
Vp mweny division 3 ya 22 anawez kuchaguliwa?(wakiume)
Huyo mbona anaenda! Labda tu combinations zigome lakini yuko vizuri! Uzuri siku hizi kuna kurekebisha combinations mara tu matokeo yanapotoka hivyo ajitahidi kurekebisha dirisha likifunguliwa!
 
Nchi hii ina njia nyingi za kuwafanya hawa watu 6 au 7 wakaendelea vizuri na maisha, tatizo tunaishi maisha ya Kufikirika... Hivi kwanini njia zinazofanyika ya uwekezaji kwenye madini zikafanywa kwenye UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO kama ZIMBAMBWE ili watu wenye hela wafanye kilimo na wengine wanufaike kwa ajira???

Hii mikoa ya Morogoro, Mbeya, Tanga, Songwe, Iringa, Rukwa na mengine yenye ardhi na mazingira bora ya KILIMO si waje watu ambao watafanya kilimo cha uhakika na wenyeji wawe wafanyakazi ili kuwe na mzunguko na uzalishaji wa ajira???...
 
Back
Top Bottom