Tujadili mshahara wa TGS D kwa watumishi wanaoishi kwenye majiji

Hapo hapo ofsini kwenu Kuna mlinzi wenu analipwa take home
270,000
Amejenga, ana mke na anasomesha watoto watano.

My take:
Hakuna mshara mkubwa Wala mdogo, Ni suala la vipaumbele vya matumizi litakalowatofautisha mfanyakazi uyu na Yule kimaendeleo
Na mlizi huyo huyo anaweza hata kumnyandulia mke wake, tena kwa kumpeleka hadi guest za Buza Kwa Mpalange! Maisha hayapo fair
 
Yaan we unaanza kazi tu unaanza kuwa na majukumu makubwa ,familia watoto wanasoma etc...
Unafahamu Wafanyakazi walio ajiriwa kuanzia mwaka 2014 mpaka leo bado hawajapandishwa madaraja/ vyeo vya kimuundo! na hivyo kuishi kwa mshahara ule ule wa TGS D sawa na hawa walio ajiriwa 2021?

Kwa hiyo unategemea mfanyakazi aliyeanza kazi mwaka 2014 mpaka mwaka huu wa 2021 bado awe tu hana familia au mtoto anayesoma?

By the way, kuna wahitimu wengine wanamaliza shule/vyuo wakiwa tayari wana familia kutokana na ukweli kwamba umri una waruhusu kuwa na hizo familia!
 
Una undugu na Mzee Yusuph? Mbona unapenda sana Taarab! Yaani walau hiyo paragraph yako ya mwisho ndiyo kidogo umeandika point! Ila hilo liparagraph lako refu la mwanzo, limejaa vijembe tu na taarab nyingi! Aaaaaahhhh!😫😫
 
Ukisikia uchawi ndio huo anaoufanya jamaa.
 
Mara ghafla wachangiaji wote wa JF watageuka kua ni watu wanaolipwa 2mil and above/month na watampa ushauri mwny salary ya laki 5 na watashangaa ssna mwenzao anawezaje kuishi hapa mjini kwa pesa ndogo hivyo.
Wengi humu tunakunja laki 7, baada ya makato tuna laki 5 tu. Hao wa 2mill ni wateuliwa wachache sana.
 
Wanawake mnateleza nini au offer za wabunge?
Sisi wa Dodoma tusubiri uzi wetu.

Ila Dodoma wanaume wasio na kipato cha kueleweka sijui wanaishije maana mji mgumu huu.
Sisi wanawake ni mtelezo tu.
Mungu awasimamie wanaume zetu mlioko Dodoma. Tuko pamoja, hatuwaachi.
 
Achana nae huyo bado amekariri formula : kuzaliwa, kusoma, kupata kazi, kuoa, kuzaa.
Siku hizi mambo yamebadilika
 
Mlinzi akijenga chumba kimoja huku umri wake 50's unasema maendeleo?
Kwani wee ulitakaje labda?
Ajenge bangaloo au?

Au hujawaona waliostaafu (60s) hawana hata kiwanja achilia mbali hata icho chumbani kimoja alichonacho uyo mlinzi.

Tujifunze kuappreciate ata kwa vile vidogo walivyofanikiwa wenzetu.

Kwa maana hawajavipata kirahisi wamepambana Sana mpk kufika pale kwa levo yao.
 
Huyo mlinzi aliyejenga ukifatilia utakuta alikuwa askari mstaafu ila sio hawa wa miaka 20-25.
Tatizo linaanzia hapa kwa sisi vijana tunaoajiriwa. Tunataka tupate ajira Leo mwakani tuanze kujenga. Na hapo lazima mshahara uwe mdogo tu. Kujenga ni process inatohitaji muda mrefu kidogo ikitegemeana na mshahara na majukumu mengine ya lazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…