Tujadili: Mtu kujitambulisha kama Mzanzibari ni halali, lakini kujitambulisha kama Mtanganyika ni haramu!!

Tujadili: Mtu kujitambulisha kama Mzanzibari ni halali, lakini kujitambulisha kama Mtanganyika ni haramu!!

Kama kuna wazanzibari, watanganyika pia wapo!! haipo namna ya kuwapotezea!
 
Christopher Mtikila ndio mpinzani pekee aliyewahi kutokea nchini Tanganyika.
Tanganyika na Zanzibar ziliungana kupatikana Tanzania.

Sisi ni Watanganyika halisi.
RIP Mtikila.
Ila wahuni sio watu, huyo dingi na uanaharakati wake wote lkn alikua Ni Chakula ya wahuni, wahuni wamepiga sana Ile 'express yourself' yake.
 
Hii ni kero namba moja ya muungano ya muda wote!! Kwa bahati mbaya haijaorozeshwa wala hakuna mpango wa kuiorodhesha miongoni mwa kero za muungano.

Juzi juzi tumefanya sherehe ya kumbukizi la miaka 60 ya uhuru wa "Tanzania", au wakiona aibu wanasema kumbukizi la uhuru wa "Tanzania bara"!! Lakini ukiwauliza Tanzania au Tanzania bara ilikuwa inatawaliwa na mkoloni gani?
hawana jibu!!!! watakuambia huo ni uchochezi.

Tumeamua kuificha historia yetu kwa kuifunika kwa kioo!!! Tumeifunika lakini inaonekana wazi.

Binafsi naukubali muungano, lakini hii kero ishughulikiwe.

Najivunia Utanganyika wangu kama wanavyojivunia Uzanzibari wao kabla ya wote kujivunia Utanzania wetu!!
Tanganyika Taifa langu
 
Tatizo letu tunaachia wanasiasia watujengee mitazamo yetu, na wanasiasa wenyewe ambao pia wao wenyewe hawajitambui wanapelekeshwa na ari na viburi vya ushindani, muungano wa nchi na nchi ni muungano wa kisiasa kwa hio haupaswi hata kidogo kuua asili za watu na majivuno ya asili zao.

Kwa nini muungano huu unakimbilia sana kuua asili za watu na majivuno ya asili zao?
kama binadamu inabidi tukae tujitathmini kwa makini sana,Na tujujengee uwezo wa kujiamulia mambo yanayoingia akilini na sio kupelekeshwa na siasa tulizorithishwa na wakoloni.

Maneno haya yamenitafakarisha sana
Ni jana tu nilikuwa naongea na jamaa wenzangu kuhusu Mila na Tamaduni za mtu mweusi zilivyosambazwa na kupotezwa na wazungu
Hawa tuliokuwa tunawaongelea ni watumwa waliopelekwa [emoji631] na Europe na visiwa vya mbali

Najua halihusiani kabisa na mjadala huu ila kuna uwiano kiasi na sisi kupotezewa mila na uasilia wetu

Imagine leo hata Eddy Murphy au Denzel Washington ukamuambia asili yako ni wapi? Ghana? Senegal? Gambia? Tz ? Wapi hajui na hataki kujua ingawa wanajua ukweli

Asante kwa maneno haya kuntu na wanasiasa ndio wanafanya ishu kubwa na unaweza kuchukuliwa hatua kwa kilijadili hadharani

Utasikia nitaulinda kwa nguvu zote
 
Back
Top Bottom