Mkuu umetoa somo la kutosha hapo kwa mfano huo; hata kama umeurahisisha sana.
Ninakubaliana kabisa na maneno ya mwanzo uliyoweka kwenye mstari wako wa mwisho.
Mwisho: hebu cheki hii ya hao hao wamarekani uliowachambua hapa>
Janga la COVID-19 - Trump anasema "Go Big" yaani wananchi wapewe pesa kiasi kikubwa zaidi ya zile $400 walizopewa kwenye awamu yake. Na Trump, ni CAPITALIST as CAPITALISTS come!
Halafu akaingia Biden, Democrat (pengine liberal); yeye akagawa kwa wananchi wake na watoto $1400.
Na mwanzo watu hao hao walipewa $1,200, ili kusaidia kuendesha maisha yao wakati wa corona.
Marekani ndio mfano wa juu kabisa, inapozungumziwa capitalism!
Lengo langu la kuyaandika haya hapa, ni hii kasumba tunayo okoteza bila hata kujua maana ya mifumo hii ya kiuchumi.
Ukimkuta mTanzania anayejinadi yeye anafurahia zaidi Ubepari, utadhani ni yeye aliyeuvumbua; kumbe maskini wa mtu hajui kitu.