Nadhani hakuna kitu ambacho kinafit mahali kote na muda wote. Kila taifa,ni lazima
Li-craft aina ya utawala unaofaa kulingana na muda na mazingira. Iwe ni mfumo wa kidemokrasi au mfumo wa kiuchumi, ni lazima uchongwe meticulously ili kutosha kulingana na mazingira na wakati husika. Ukivaa suruali na ikakutosha leo sio lazima ikutoshe miaka 10 ijayo, suruali ikinitosha mimi sio lazima ikutoshe na wewe. Na hili ndio tatizo linalofanya wengi tupingane na mambo (ideologies) ya kuletewa jumla jumla toka magharibi. Nadhani nimejieleza vizuri;
Ila sasa, balaa tunalokutana nalo ni pale tunapojaribu kuchonga mifumo yetu wenyewe ya kiutawala na kiuchumi, basi tunaanza kulalamikiwa kwamba hatufuati demokrasi, as if demokrasi ni sare ya shule na yenye size moja, hakuna kutumia vazi la aina nyingine kulingana na mazingira yako, na hapo ndio wanaanza kuleta vikwazo vya kiuchumi nk; Samia must stand strong.