Tujadili: Uwepo wa Ujamaa wa kisasa ama Ubepari

Watu mdomoni wanasema wao wajamaa
Wakati kwenye maisha yao wanaishi kibepari

Ova
Katika pitapita zangu Tanzania, Sijaona Mtanzania Pebari.

Ubepari una sifa nyingine inaitwa Ubinafsi...

Tanzania unaenda kwenye Duka la Muhaya unakuta kuna Muha anauza...
 

Kesi ya kupinga kwa mahakama gani?
 
Unaposhindwa kusema ukweli mwanzo kabisa , basi jua kila kitakachoendelea hakitakuwa sahihi
Kwa structure za mahakama zetu zilivyomezwa na katiba, nani angeweza kufungua kesi dhidi ya tume ya uchaguzi na kushinda,?
 
Shida ya ujaamaa ni kuwa ,una direct link na umasikini, ni moja ya system inayozalisha watu wavivu kirahisi sana, maana kuna watu wanaweza wakaamua wasifanye kazi kwa kuwa kuna working class
Ubepari ni mzuri kwa maana ya kuchapa kazi na kuamini juhudi ndio the only tool for survival , shida kubwa ipo kwenye kuhama kutoka ujaamaa kwenda ubepari hapa ndo pana balaa na pagumu.
Kama kuna system ya ku blend ujamaa na ubepari tupate kitu kingine nadhani ingetufaa kama taifa
 
Kesi ya kupinga kwa mahakama gani?
Unajua Tindo ua nakushangaa sana kwa kushupaz a shingo kwa vitu ambavyo ata akilini haviingii..! Tu wakweli hivi Lissu na Lowasa nani alikuwa na ushawishi? Hivi ulitegemea kweli Lissu apate kura Milion 9 toka wapi?

Nikukumbushe tu kuwa
2005 Mbowe akigombea Urais alipata kura laki 5
2010 Dr Slaa alipata kura Milion 2 na laki kama 4 hivi
2015 Lowasa anapata kura Milion 6 sote tunajua kuwa Lowasa yeye kama yeye alikuwa na base ya watu ambao walitoka CCM wengine amabao walimkubali tu na Ukumbuke kulikuwa na ile Ukawa ambayo kwa kias kikubwa pia ilichangia, Sasa bandugu Chadema kama Chadema chini ya Lissu kura Milion 9 ingezitoa wapi? Maana kila uchaguzi nyie ni watu wakulalalmika tu.
 
Unachouliza ni tofauti na nikuchokujibu

Ulidai kwenye Free enterprise economy huwezi lalamika bei ya vifurushi kupanda.

Kuwepo suku huru haimaanishi serikali haiwezi ingilia!! Ila tu inakua limited kwenye policy na regulation.

Mfano hyo blockchain tech as much as zipo kwenye soko huria lakini pia zina contradict na sheria zilizopo za money laundering, Capital markets, competition law, mfano kama kuna sheria inayotaka miamala yote iwe reflected kwenye centralized swift system, sasa if any crypto deals hazipiti huko ndio maana zinaweza kuwa blocked. But in other circumstances zisingekua blocked.

Unless ulitaka nchi kama US isiwe na sheria kabisa ili soko lijiamulie lenyewe kuanzia bei mpka market structure!!
 
Hapo kura halali ni za Mbowe tu ila Dr Slaa na Lowassa walipata zaidi ya hiyo.

Nachoweza kukubali ni kwamba Lissu hakushinda uchaguzi lakini haimaanishi JPM alipata 85%.... Realistically JPM 60-65% na Lissu 35-40%.

Jifunze US au Kenya miaka yote mshindi ni gap ya 10% au below sio 80% kwa 20% mambo hayo hayapo realistic mkuu hta kma ungefanya kila kitu.
 

Naona unatoa mifano ya nyuma ili kubeba Utetezi wako wa hiki kilichofanyika uchaguzi huu. Kwa kukusaidia tu, hata wapiga kura wote hawakufika 10m. Kama tayari hata idadi ya wapiga kura ilikuwa ya kupika, hizo kura 9m Lisu angezitoa wapi? Kwa ujumla ule haukuwa uchaguzi bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Ni bora Mungu ameamua kufanya mabadiliko bila kumwaga damu, ila Magufuli alichafua sana demokrasia ya nchi hii.

Halafu kuhusu Lowasa, ukweli ni kuwa kura walizopata cdm hata isingekuwa Lowassa au ushirikiano wa Ukawa, bado cdm ingepata kura nyingi tu. Lowassa apate kura milioni 6+ kwa kusema "Elimu, elimu, elimu"! Huyo Lowassa namfananisha na mtu aliyekuta chakula mezani kisha akaanza kugawa, halafu akapewa sifa za mpishi bora. Alaaniwe Mbowe na genge lake kwa kumleta huyo mzee tapeli wa kisiasa ndani ya cdm.
 
Ujamaa sio uvivu...

Uvivu ni tabia na unachangiwa na utamaduni

Msingi wa waendeleo yote ni Kazi.

Ukisema Ujamaa ni uvivu basi Wachina ni wavivu kuliko wote wayahudi ni wavivu, wajerumani ni wavivu.
 
Bila kujali ni ujamaa au ubepari, mfumo wowote unaodumaza uhuru, fikra, ubunifu na kuchochea woga na kutojiamini haufai hata kama utagawa maziwa kila asubuhi.
 
Ujamaa sio uvivu...

Uvivu ni tabia na unachangiwa na utamaduni

Msingi wa waendeleo yote ni Kazi.

Ukisema Ujamaa ni uvivu basi Wachina ni wavivu kuliko wote wayahudi ni wavivu, wajerumani ni wavivu.
Sijasema ujamaa ni uvivu , nimesema ni system amabayo ni rahisi sana kuzalisha wavivu, nilikuwa nimeweka bakaa hapo kwa wachina kwa muktadha wa desturi za jamii inaweza kuchangia pia uvivu
Lakini the fact kwa nini warusi ni walevi kupindukia inatokana na athari za Ujamaa
Ujamaa kuna working class , na kuna class inaweza ku take advantage of the working class
 
Asante..umetupa mchanganuo mzuri na wa ukweli kabisa. .binafsi nimekuwa nikifikiri ubepari Ni kama ubinafsi tu wa kutaka kujilimbikizia mwenyewe na familia yako ili mneemeke wenyewe..bila kujali mwenzako anakula na anaishije...bepari kiasilia hathamini asiye nacho..na mara nyingi kumkaribia huwezi..utamwonea wapi..
 
CCM mmeanzisha lini ujamaa wa kisasa? Ndiyo ujamaa gani huo? Mnataka kudandia sera ya social democrats ya ACT?

Wazembe wakubwa!!!
 
Hizo tabia unazosema jomba Ni tofauti kabisa na sera za ujamaa na Kujitegemea...hizo kiukweli Ni tabia mbovu na binafsi tu, inawezekana hata uongozi wa juu unakuwa hauna taarifa..Sheria zipo nzuri Sana zinazolinda watu na Mali zao na ndio maana unaona watu wapp na amani Sana na wanajifanyia kazi zao kwa amani kabisa. ..mahakama zipo na zinatenda haki sana
 
CCM mmeanzisha lini ujamaa wa kisasa? Ndiyo ujamaa gani huo? Mnataka kudandia sera ya social democrats ya ACT?

Wazembe wakubwa!!!
Jomba Kwan huu ujamaa uliopo Ni wa namna gani...hizo translation nyingine unazojua wewe Ni za watu weupe mzee..nadhani...tusikariri mambo..tofauti ya ujamaa wa ACT na CCM ipo wapi hasa...mi nadhan ACT ame c&p ccm.. kwa sababu tofauti ikisemwa ipo Ni ya namna ya operation tu..
 
Sasa kama warusi wavivu jomba...imekuwaje kuweza kufikia level ya dunia ya kwanza wakati wakiwa wajamaa
 
Sure..!! Nimekuelewa Sana
 
Sure..!! Nimekuelewa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…