Tujadili viumbe walioumbwa kwa moto na upepo ambapo humo tunapata Malaika, majini, vibwengo, shetani wana maumbo au hadaa zetu tu?

eti Lucifer muafrika😂

kuna utata kwenye neno 'jini'

ukisoma bibilia za kiingereza zinatumia maneno 'demons' na 'devils'

hilo neno 'jini' limetolewa kwenye lugha ya kiarabu, kutokana na neno 'jinn'/'djinn'

kwahiyo nakubaliana na wewe, ila kwa sharti kwamba hilo neno lina utata
Neno Jinn kwa lugha ya kingereza ni Djinn au Jinn na sio devils au Demons..
So utata ni mkubwa
 
Habari wakuu.

Leo nimeona nilete kwenu hii hoja kwa mfumo wa swali. Kama nililivyoliweka hapo kwenye heading kuhusu taswira au umbo lionekanalo kwa macho pale inavyowezekana, hawa viumbe ambao tunaaminishwa kupitia imani zetu kwamba wameumbwa kwa moto na upepo wanabeba taswira gani?

Upepo sote tunaufehemu kwamba hauna umbo linaloonekana bali tunauona ukileta matokeo ambayo ni kutikisa ama kuhamisha vitu vinavyoonekana pale unapovipitia. Pia moto tunauona kwa macho ingawa tunasema hauna umbo maalumu wala haushikiki bali nao unapimwa kwa matokeo unayoyaacha kwa mguso ama kuvipitia.

Viumbe ninavyoviongelea, havijawahi kuwa dhahiri kwenye macho yetu kwenye ukawaida wa maisha yetu. Lakini tumekuwa katika kuamini na kujenga taswira ya namna muonekano wa viumbo hivyo vinavyotawala ulimwengu usioonekana. Ingawa kwenye kujenga taswira hizo tumeshuhudia itikadi za nyeupe ni utukufu na nyeusi ni uovu na laana ikipewa kipaumbele.

Kabla sijaendelea, napenda kuuliza jukwaa. KUNA AWAYE YEYOTE AMESHAWAHI KUONA MALAIKA AMA MAJINI? Je unaweza kushare nasi nini ulichoona? (Mimi nimewahi kuona majini na viumbe wengine) lakini kwa kuwa naandika uzi huu napenda kupata ushuhuda wa kutoka kwa wasomaji wengine. Kwenye uzi huu mbeleni nitachangia nini nilichokiona.

Tuendelee sasa.
Ufunuo wa Yohana 4: 6 anaelezea uwepo wa Wenye UHAI wanne. je ni kina nani hao na kama kuna ufafanuzi wa umbo lao ukoje?

Je, tunawezaje kumtofautisha Malaika kutoka kwa Kerubi? Tunamtambuaje Kerubi akiwa amesimama na Serafi? Je jini tunalitofautishaje na mapepo? Shetani na majini wana tofauti gani? Kama jini na mapepo na mashetani wanaweza kukaa ndani ya mtu, je malaika na jamii zao wanaweza pia kukaa ndani ya mtu?

Je viumbe hao wapo au ni illusions zetu wanadamu? Narejea taswira zilizochorwa na akina Michellangelo, Da Vinci, Raphael na wengine enzi za rennainsance?

Karibuni tukate maneno
Hizo ni illusion + Hallucinations (kwa watumiaji wa vichangamshi)

Ukweli ni kwamba hakuna jini wala pepo.

Aslimia 100% ya watu wote wanaohadithia habari za jini au pepo huwa si mashuhuda wa kwanza wa habari hizo,

Huwa wanakuwa wameambiwa,

Aliyemwambia naye kaambiwa na mwingine,

Aliye mwambia mwenzake akaenda kumwambia mwingine unakuta naye kaambiwa na mwingine.

Yaani utatengeneza chain ndefu mpaka inakuwa kama loop (mzunguko)

Hakuna awezaye kuthibitisha jini, shetani wala pepo kwasababu viumbe hivyo havipo.

Wengi wao ni udanganyifu tu na kutokuelewa phenomenona flani na kuipelekea kuwa jini /pepo.

Mtu anaweza kuona kisiki tu akaja kukuthimulia kuwa ni pepo.

That is a real definition of illusion.
 
Mkuu
Ingawa naona wengi wa wachangiaji wamejitahidi kuelezea uelewa wao na hakika wameishia kutaja nasaba ama aina za hao viumbe wasioonekana ingawa tunajulishwa kwamba wapo.

Hebu tujiulize kidogo ama tutafakari kwa nukta chache. Watu wengi tumeshuhudia baadhi ya matukio yanayoitwa kupandisha majini. Kuna jina wanalitumia kwa mtu ambaye anasadikika kuwa ana majini, anaitwa KITI. Na tumeona ama kusikia kuhusu matukio haya na kwa walioshuhudia kwa macho (nikiwemo mimi) wanaweza kuthibitisha kuwa hali fulani isiyo ya kawaida inamkumba mtu ambaye hajawahi kuwa na historia ya tatizo la akili wala ufahamu, na mtu huyo anazungumza maneno ambayo watu wengi husema ni jini ama majini yaliyomkalia mtu huyo ndiyo yanazungumza. Imetukia wakati mwingine jini ndani ya mtu linawasiliana nawe mwenye ufahamu kamili na kukuelezea matukio hususan mabaya uliyoyafanya wakati uliopita... kama vile uzinzi, wizi na kadhalika...

Hali hii tunaiitaje na nini kinatuthibitishia kuwa huyo mtu ana majini na hayo majini yapoje haswa?
Mkuu Msanii
Hilo huwa ni tatizo la Afya ya akili linaitwa dissociative disorders, na wengi huhisi kabisa kuwa kuna jini yupo kichwani..

na hizi conditions zinaweza kupelekea mtu akawa na altered perceptions of reality na mara nyingi unusual beliefs au experience Aliyowahi kuiona ndo ataielezea kama atakuwa ni mtu wa kuamini sana Uchawi bhasi atasema ameshikwa na mizimu...

Kama atakuwa ni wa kuamini Majini basi atasema yeye ni jini..
 
Ni magonjwa ya akili

Najua moja linaitwa schizophrenia, ila nahisi yatakuwa mengi

Ukisema hana historia ya kuumwa akili, unaweza kuthibitisha au ni mazoea?

Au unaweza kuta gonjwa lipo muda mrefu ila ndo limeanza kumomaa au kuna viashiria vinafanya litibuke.
 
Habari wakuu.

Leo nimeona nilete kwenu hii hoja kwa mfumo wa swali. Kama nililivyoliweka hapo kwenye heading kuhusu taswira au umbo lionekanalo kwa macho pale inavyowezekana, hawa viumbe ambao tunaaminishwa kupitia imani zetu kwamba wameumbwa kwa moto na upepo wanabeba taswira gani?

Upepo sote tunaufehemu kwamba hauna umbo linaloonekana bali tunauona ukileta matokeo ambayo ni kutikisa ama kuhamisha vitu vinavyoonekana pale unapovipitia. Pia moto tunauona kwa macho ingawa tunasema hauna umbo maalumu wala haushikiki bali nao unapimwa kwa matokeo unayoyaacha kwa mguso ama kuvipitia.

Viumbe ninavyoviongelea, havijawahi kuwa dhahiri kwenye macho yetu kwenye ukawaida wa maisha yetu. Lakini tumekuwa katika kuamini na kujenga taswira ya namna muonekano wa viumbo hivyo vinavyotawala ulimwengu usioonekana. Ingawa kwenye kujenga taswira hizo tumeshuhudia itikadi za nyeupe ni utukufu na nyeusi ni uovu na laana ikipewa kipaumbele.

Kabla sijaendelea, napenda kuuliza jukwaa. KUNA AWAYE YEYOTE AMESHAWAHI KUONA MALAIKA AMA MAJINI? Je unaweza kushare nasi nini ulichoona? (Mimi nimewahi kuona majini na viumbe wengine) lakini kwa kuwa naandika uzi huu napenda kupata ushuhuda wa kutoka kwa wasomaji wengine. Kwenye uzi huu mbeleni nitachangia nini nilichokiona.

Tuendelee sasa.
Ufunuo wa Yohana 4: 6 anaelezea uwepo wa Wenye UHAI wanne. je ni kina nani hao na kama kuna ufafanuzi wa umbo lao ukoje?

Je, tunawezaje kumtofautisha Malaika kutoka kwa Kerubi? Tunamtambuaje Kerubi akiwa amesimama na Serafi? Je jini tunalitofautishaje na mapepo? Shetani na majini wana tofauti gani? Kama jini na mapepo na mashetani wanaweza kukaa ndani ya mtu, je malaika na jamii zao wanaweza pia kukaa ndani ya mtu?

Je viumbe hao wapo au ni illusions zetu wanadamu? Narejea taswira zilizochorwa na akina Michellangelo, Da Vinci, Raphael na wengine enzi za rennainsance?

Karibuni tukate maneno
Mshana Jr Rabbon DR Mambo Jambo Pascal Mayalla
 
Mimi ninachoamini MAJINI na MIZIMU nikiiomba kwa namna fulani na kwa ingredients fulani yananijibu na kunisaidia hasa mambo ya business.

Only that
Kwahiyo tuje pm, we ni mujanja mujanja😄
 
Mitoto ya iliyozaliwa buku2 wanabisha hakuna majin ila sis tuliyowahi kushuudia haya mamb ngoja tukae kimya mpaka siku msala ukikuta ndo utajua majin hua yanafanya kazi na binadamu ndo maana wezutu white pple wanaamin uwepo wa hawa viumbe na kutafuta ways za kuwaslianano kwa nia ya kutawala dunia sis tupo tunabisha tu hata mizimu yetu hatuiyamin..........always black pple hata akisoma atabaki kua jinga flani eg kabudi
 
Ulikutana na majini wapi??
 
Automatically,malaika waasi, pepo , Ni celestial beings (yani supernatural beings) yani walmeumbwa moja kwa moja na Mungu isipokuwa Jinn (jini) Sio supernatural.( Hajaumbwa na Mungu).

Hivyo basi pepo Ni viumbe wenye roho kamili, (Very powerful) na hawana physical form kwamba pepo Ni huyu ama yule . . .

Na ili aonekane kwa macho ya kibinadamu itamlazimu aingie Human realms, kutoka kwenye ulimwengu wao japo kuwa kwao Ni risk Sana.
 
Automatically,malaika waasi, pepo , Ni celestial beings (yani supernatural beings) isipokuwa Jinn (jini) Sio supernatural.

Hivyo basi pepo Ni viumbe wenye roho kamili, (Very powerful) na hawana physical form kwamba pepo Ni huyu ama yule . . .

Na ili aonekane kwa macho ya kibinadamu itamlazimu aingie Human realms, kutoka kwenye ulimwengu wao japo kuwa kwao Ni risk Sana.
Wewe umejuaje haya!?

How can i trust you.?
 
Wewe umejuaje haya!?

How can i trust you.?
....Unavypata ugonjwa na kwenda hospital ilihali hujui Nini unaumwa, ila unagusa tu panapouma na baada ya kipimo ukiambiwa unaumwa kitu ambacho hukijui , utamwambia tabibu?
 
Mkuu Msanii
Hilo huwa ni tatizo la Afya ya akili linaitwa dissociative disorders, na wengi huhisi kabisa kuwa kuna jini yupo kichwani..

na hizi conditions zinaweza kupelekea mtu akawa na altered perceptions of reality na mara nyingi unusual beliefs au experience Aliyowahi kuiona ndo ataielezea kama atakuwa ni mtu wa kuamini sana Uchawi bhasi atasema ameshikwa na mizimu...

Kama atakuwa ni wa kuamini Majini basi atasema yeye ni jini..
Matatizo ya akili yapo!

Na hao viumbe wapo!
 
Majini ni ya kiislamu

Mapepo ni ya kikristo

Kuhusu aina za malaika, Kuna nadharia mbalimbali, ila ninachojua wanapangwa kulingana na ukaribu wao na kiti cha enzi....

Mapepo yanaweza kuvaa mtu, kuna ushahidi kwenye bibilia.
Hakuna mahali malaika amemvaa mtu kwahiyo tutahitimisha hawawezi.

Hivi viumbe ni hadithi kwasababu, utaviona endapo unaamini kwenye uwepo wao.

Utasikia sana wakristo wakisema wameona malaika, hutowasikia waislamu.

Wazungu watasema wamemuona bigfoot, watz watasema wameona kibwengo.

Nimekosa neno la kiswahili hili jambo linaitwa indoctrination.
Ulimwengu wa Roho ni kweli na dhahiri.
 
Hawajafunga ila wamebadilisha ratiba ya kula. Siku ina masaa 24 wao wameamua kutumia masaa ya kulala kula badala ya kawaida tuliyoizoea.

Kinachonikera ni pale jamii yao wanapokuwa wengi mahali fulani hutaka watu wengine nao wabadiri ratiba zao za kula pasipo sababu za msingi
 
Automatically,malaika waasi, pepo , Ni celestial beings (yani supernatural beings) yani walmeumbwa moja kwa moja na Mungu isipokuwa Jinn (jini) Sio supernatural.( Hajaumbwa na Mungu).

Hivyo basi pepo Ni viumbe wenye roho kamili, (Very powerful) na hawana physical form kwamba pepo Ni huyu ama yule . . .

Na ili aonekane kwa macho ya kibinadamu itamlazimu aingie Human realms, kutoka kwenye ulimwengu wao japo kuwa kwao Ni risk Sana.
Mkuu jini ameumbwa na nani?
 
Je yawezekana majini ni uzao wa wale Malaika wachache waasi waliozaa na binadamu wakazaliwa Wanefili Mwanzo 6:1-4, na gharika ya Nuhu ilipoua viumbe mbalimbali ikiwemo hawa Wanefili miili yao ikafa na roho zao si hawa majini?
Maana baba zao yaani malaika waasi wamefungwa shimoni hawana ruhusa kutoka huko kuja duniani hata hukumu itakapokuja, Yuda 1:6, 2 Petro 2:4.
Kama sivyo, zile roho za Wanefili walikufa kwenye gharika ziko wapi?
 
Back
Top Bottom