Tujenge shule za michezo kila mkoa tuachane na kuandaa AFCON

Tujenge shule za michezo kila mkoa tuachane na kuandaa AFCON

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Nawashauri Watanzania tuwekeze katika kujenga shule za michezo kila mkoa.

Kila tunapofanya mashindano yale ya shule za msingi tunawachukua wale best students katika kila mchezo na kuwahamishia katika shule hizi za mikoa za michezo. Hapo wawekewe facilities zote, na walimu.

Kila mwaka shule hizi za michezo tutakazojenga kila mkoa ziwe zinafanya mashindano yao ya kitaifa kushindana wao kwa wao na kuwa na washindi wa kitaifa.

Hawa washindi wa kitaifa ndiyo tuwapeleke katika mandalizi ya mashindano ya kitaifa.
 
Kama veta kila mkoa haipo itawezekana kwa shule ya kucheza cheza?

Tuhimize kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda na ujenzi.

Michezo ni talanta.
Hizi fikra zimedumaza maendeleo yetu kwa mda mrefu.

Naomba ninukuu

"

Do Olympic athletes get paid?​

Olympic athletes do not get paid by just attending the Olympic Games.

However, if an athlete earns a medal, there is a medal bonus attached to it. A gold medal is worth $37,500, a silver medal is worth $22,500 and a bronze medal is worth $15,000. So, not only is there an incentive to stand on the pedestal in order to have your name etched in Olympic history, but the athletes also look forward to the cash prize that comes with it."

Tunaona wachezaji wanasajiliwa kwa milioni 200, mpaka 800 mchezaji mmoja wa mpira.

Mchezaji analipwa mpaka milioni 23 kwa mwezi huku msomi mwenye degree analipwa milioni 2

ni kwa nini jamii zetu zinakumbatia ujinga na kuacha kuwaza kwa fikra mgando za mtoto kuingia kwenye michezo ni uhuni.

hatuna wanamichezo matajiri kwa sababu hatuandai watoto wadogo tangu udogoni kuja kuwa wanamichezo.

Swala la veta umelipotosha kwa maana veta ipo kila mkoa ila haijafika kila wilaya.
 
Back
Top Bottom