Umenikumbusha zamani tulivyokuwa wadogo, mgeni akitutembelea nyumbani siku hiyo lazima achinjiwe kuku hata kama nyumbani hamfugi kuku basi mzazi ataenda hata kukopa pesa amnunue huyo kuku, kikubwa tu mgeni ale vizuri na aondoke huku amefurahi...
Unachosema ni kweli kabisa hii kasumba imeanzia kwenye malezi... na sasa imeshakomaa mpaka imetufanya tumekuwa wapuuzi na watu wakujipendekeza pendekeza ovyoo.
Leo hii wewe na muhindi mkienda pale Kurasini kushughulikia suala la passport, huyo muhundi anaweza asichukue hata siku tatu akawa akapewa passport yake, ila wewe mbongo halisi unaweza ukazungushwa hata miezi mitatu... inaudhi kwakweli hii kasumba.
Ukienda taifa kam Misri au Morocco huko kwenye ligi hata ufunge goli 100 kama wewe sio mzawa hakuna media yoyote itakayokuimba.. Mayele huyo hapa huwa analalamika pamoja na kuwa yeye ni striker tegemeo wa Pyramid na anafunga sana, lakin hapewi ile King treatment aliyokuwa anapewa hapa Bongo. Kiufupi huko wanamuona ni mtu wa kawaida sana.
Binafsi huwa kuna muda nachukia hata kuzaliwa kwenye hili taifa, maana huwa naona ni kama aina fulani ya laana yaani kuzaliwa Tanzania ni moja wapo ya adhabu ambayo Mungu amekupa... Mungu kama anakupenda basi ungezaliwa kwenye mataifa yanayoeleweka na sio hili